Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
- Tukiwa wadogo tulitembelewa na binamu yetu kutoka kijijini. Tulimpokea vizuri na kwasababu tulikuwa rika moja tukalala pamoja. Usiku ule tulikula chips na nyama za kukaangwa. Ndugu yangu yule alishangaa tunaweka tomato sauce, akadhani damu.
Kesho yake tukaenda Imalaseko supermarket, Zamani ndio ilikuwa mpango mzima. Baba akasema Kila mtu achukue anachotaka. Jamaa akabeba tomato sauce tatu, kufika kwenye gari kaanza kunywa Kama soda.
- Ndugu yetu mwingine wa kike alikuja kututembelea from bush na ilikuwa ni mara yake ya Kwanza kufika mjini. Akapewa chumba chake self contained, choo Cha kuchuchumaa, akaelekezwa namna ya kukitumia.Akaelekezwa pia namna ya kutumia jiko.