Utatoa maamuzi gani?

tz1

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2011
Posts
2,121
Reaction score
536
Kuna jamaa alikuwa na kesi mahakamani,na wakili wake alimshauri kwamba ategemee fine au akishindwa
kulipa atapelekwa jela,na hukumu imebaki siku 2.
Jamaa alikuwa hana hela,akamkopa boss wake na boss akasema hana.
Alipo rudi nyumbani alimweleza mkewe na mkewe akasema atajaribu kutafuta.
Kesho yake mkewe alipata hela na fine ikalipwa.
Usiku wake jamaa hakupata usingizi,akachungulia simu ya mke wake.
Akaona sms inasema,nisipo kusaidia wewe mpenzi nitamsaidia nani?
Namba ni ya boss wake na yeye ni dereva.
Mke wake alikuwa hajui mumewe anamwendesha nani na boss inasemekana hajui kama ni mke wa dereva wake.
Kama wewe je uta muuliza mkewe au boss wako?
Au uta endelea kufanya kazi au utaacha?
Pagumu hapo.
 
kumbe nawe unajua kuwa ni pagumu?
 
Hapo kwanza boss hana kosa coz hakujua ni mke wa mfanya kazi wake. labda hajui hata kama ni mke wa mtu. Kwa hiyo haina maana kuacha kazi.
Imebaki kati ya mtu na mke wake sasa.
 
Hapo kwanza boss hana kosa coz hakujua ni mke wa mfanya kazi wake. labda hajui hata kama ni mke wa mtu. Kwa hiyo haina maana kuacha kazi.
Imebaki kati ya mtu na mke wake sasa.

Kwa hiyo jamaa ale bati kama vile haja ona sms?
 
Basi aamue kama anataka kuendelea kufadhiliwa na bosi anyamaze ,kama hataki amweke kati huyo mke wake.

Amweke kati ki vipi,Amdunde ngumi au amwache?
 
Kwa nini, wakati anaibiwa?
Kweli kabisa unaibiwa halafu huchukui hatua yoyote!!!!!!
Haya swali lako hili,Hiyo avatar yako ni picha yako?Sijaona mrembo kama huyo.
 
Kweli kabisa unaibiwa halafu huchukui hatua yoyote!!!!!!
Haya swali lako hili,Hiyo avatar yako ni picha yako?Sijaona mrembo kama huyo.
Tumesha maliza kujibu mada?
Picha ya avatar sio mimi.
 
Hapo pagumu, uamuzi ni mdogo huyo mwanaume ampee freedom boss wake na mke wake waishi kwa mapendo na yeye atafute mwingine.

Sababu wote wamemsaidia-Mke kamuokoa asiende jela na boss ndo kalipa deni lake..
 
Mahari atarudishiwa
 
Kwa ufupi mimi ndio huyo boss......................Tu,eanza na Nkeo siku nyingi tu, kuna siku mshahara ulicheLewa nikakata pochi la menu, kuna siku mtoto aliugua nikatoa pesa ya matibabu, kuna siku Nkeo alikuaga anakwenda Moro, Nilikua naye, NA MIMI NDIYE NILIYESUKA ZNEGWE UFUNGWE...ILI NILE KWA KUPONI.........n.k, cha msingi kula BATI kama vipi niachie au kama unayaweza kwa mama watoto wangu, POA,
 
Jamaa ana umeme yeye na mke wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…