Utatofautisha vipi gari ya Dizeli na Petroli?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Mambo vp wakuu?

Kwa mtu wa kawaida anawezaje kutofautisha kati ya gari inayotumia petroli na ile ya dizeli hasa kwa gari hizi ndogo kama haikuandikwa?

Kuna mahali nimesoma kuna mtu kasema kwamba gari zinazotumia diesel kwenye Kipimo cha rpm ule mstari mwekundu huanzia kwenye 4,500 kwa maana haiwezi kuzidi 5000 lkn kwa upande wa Petroli mstari mwekundu huanzia karibu kwenye 6000 hadi 8000 kumaanisha kwamba rpm ya gari za petroli ipo juu.(angalia picha)

Je wewe unadhani una mbinu gani mbadala ya kujua tofauti kati ya gari ya petroli na dizeli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hiyo mizunguko achana nayo, ina maana tofauti kabisa katika kuliendesha gari,
mfano hapo kwenye Red kabisa usitumie ni kwamba umeivuta /vumisha injini sana km utazoea utajasababisha ringi za oil na compression kuchoka mapema
ukiona kwenye hiyo dashboard X1000 (maana yake ni kuwa mzunguko wa injini flywheel. crankshaft au piston imezunguka mara 1000 kwa dk sasa ukiweka 5 X 1000 ni 5000 kwa dk moja lazima utatakiwa uwe umeenda umbali mkubwa sana au gari imevuta kitu kwa nguvu kubwa saba hivyo ukawekewa njano, kijani mwisho nyekundu
kutambua hii gari ni ya Diesel au Petrol ni mgurumo
Diesel ina mngurumo mkubwa katika injini kuliko a petrol
Diesel hutoa angalau Moshi mweusi kuliko Petrol
Diesel injini uchomaji wake ni wa kubana mvuke wa hayo mafuta unaoletwa na nozzel na kutokea mlipuko wakati Petrol wanatumia Plug kuchoma (cheche za moto) na hutokea mlipuko
Diesel inachelewa kung'oka ilipo mpaka ichanganye mafuta wakati Petrol inachomoka inapowashwa mafuta yake
 
Mkuu asante kwa ufafanuzi wa kina, ila pale kwenye mshale nilimaanisha kwamba ukiingia kwenye gari ya petrol,kile kipimo cha rpm(tachometer)maximum/ukomo wake unafikia had 8000 wakati gari za dizeli ukomo wako ni 6000.lakini nashukuru kwa ufafanuzi nimekuelewa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diesel nyingi utazijua tu na milio yake likiwa idle/silencer ina sauti kama Canter ama Mitsubishi Pajero..."Kara-kara-kara-kara-kara-kara-kara-kara-kara-kara" kelele nyingii. Zile za kizamani zinatoa moshi mweusi au blue unapoiwasha tu na ukirev gear ya kwanza na ya pili. Diesel chache ndio zenye milio ya tofauti kama 12B, 1HZ na 1HD ya Landcruiser, TD42 ya Nissan..hawa ni "Beeeeehp...mmm...beeeehp....mmmm" mlio mzito sana. Hizi ndio diesel engine ntaendesha anyday.
Petrol zina sifa kuu ya kuwa silent zikiwa idle, yani ukikuta engine ya petrol hata ikiwa V8 kama hujarev/ kukanyaga mafuta huwezi isikia ikipiga kelele kama zilivyo diesel. Ukiona engine ya petrol ina sauti ujue imetanuliwa muffler au wameitune tu itoe sauti. Petrol haitoi moshi kabisa mafuta huungua vizuri. Ukiona inatoa moshi ujue kuna hitilafu kwenye mfumo wa uchomaji!
NB: Kama una pua nzuri unaweza kutofautisha engine kwa harufu ya moshi. Petrol moshi wake uko strong puani kuliko ule wa diesel.
 
Asante kwa elimu hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mimi natumia gari ya diesel rpm yake ni sawa na ya petrol tu, labda uje na hoja nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…