Utatu wa Dkt. Magufuli, Eng. Kijazi na Eng. Mfugale katika ujenzi wa barabara nchi nzima tutaukumbuka milele

Kazi hizo zingeweza kufanywa na yoyote yule maana hela ya wananchi ilikuwepo tu.

Hawa jamaa wamekufa kwa kufuatana kwa muda mfupi sana...sio kawaida.

Walipiga sana hela kwenye hiyo miradi kwa kujipendelea tenda kinyume na taratibu. Waliua sana kampuni pinzani,as a result....
 
Inaumiza sanaaaa
 
Hawafai wote wale, walikuwa wanazua miradi mingi mingi haraka haraka ile wapige mkwanja mrefu haraka haraka; sasa Mungu fundi akwaua wote kwa haraka haraka pia!

na ufundi wake ukadhihirike kwako pia.
 
Utatu huo unaozungumza pole pole utajagundua ndio walikuwa wapigaji kupita kiasi katika historia ya nchi hii. CAG alionyesha upotevu wa matrilioni ya hela karibu kipindi chote cha hao watu wako wa utatu. Ununuzi wa ndege ukahamishiwa Ikulu why nini walichokificha kuna shina bora tuwaache wapumzike kwa amani tusiwasumbue.
 
Hizi slogans za watu wa mwendazake, utafikiri walikuta nchi haina barabara hata moja Magufuli kajenga zote. Looh.
 
Nakubaliana na wewe ila usimlinganishe na Mkapa ndie alijenga foundation ya Taifa hili kiuchumi. Amini usiamini Legacy ya Mkapa ni kubwa sana baada ya Nyerere.
Naelewa, kwa mkapa ni in general. Kikwete km nyingi ni utawala wake, sasa tukaanza potoshwa cjui barabara ni awamu ya gwara tena πŸ˜‚
 
Mungu ni fundi sana.
Anajua kuwafuta machozi wanaoonewa.
Hakuna tena:-
Wakuu wa wilaya na mikoa miungu watu.
Hakuna kutekwa na kupotezana
Hakuna kutumbuana kwa ajili ya misifa
Hakuna maiti kwenye viroba ufukweni.
Hakuna kufilisi wafanyabiashara kwa kutumia Task Force.
Hakuna kunyang'anya fedha za Bureau de Change.
Hakuna na kutishana.
Hakuna na kwenda kwenye ibada kwa mbwembwe na kudai mic.
Hakuna kutisha majaji na mahakimu.

Kwa kifupi kumetulia!!

Asante Mungu.
Wewe hujaribiwi!!
 
Cc, kinuju njoo huku πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…