Transistor
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 1,061
- 1,637
Habari wanajamvi,
Kumekuwa na dhana tofauti tofauti juu ya tatizo hili la kuongezeka kwa bili ya umeme.Japo ongezeko la ziada la bili kubwa ya umeme lina sababu za kitaalamu nyingi lakini sababu mojawapo ambayo baadhi ya mafundi wamekuwa wakitatua ni kukabiliana na leakage kwa kubadilisha earth load.
Je kitaalamu ubadilishaji wa earth load unaondoa tatizo hili la leakage inayopelekea ongezeko la bili kubwa ya umeme?
Kama nyumba yako kweli ina leakage katika earth,baada ya kuboresha mfumo wako wa earth na kubadilisha earth load kinacho takiwa kitokee ni kujizima kwa RCD(Residual Current Divice).
Hivyo ubadilishaji wa earth load siyo tiba ya kuondoa leakage bali ni sehemu mojawapo yakutambua uwepo wa leakage katika nyumba.
Ukweli ni kwamba kama nyumba yako ina leakage katika waya wa earth harafu earth load ikawa mbovu RCD itashindwa kuitambua leakage hiyo,hivyo kwa kubadilisha earth load kutasaidia earth system yako iwe safi hivyo RCD itaitambua leakage hiyo na kujizima.
Kama nyumba yako haina Circuit breaker ya RCD wala ya ya ERC,endapo nyumba yako ina leakage ukibadilisha earth load utasababisha tatizo kuwa kubwa zaidi.
Kwa nini RCD inatakiwa ijizime?
Kama waya wa earth una leakage maana yake una kiwango flani cha electrons ndani yake,hivyo kama ukibadilisha earth load mfumo huo wa earth utashikana vizuri na ardhi,hiyo itakuwa ni short circuit.
Tambua kuwa ardhi ni mfano mzuri wa neutral wire hivyo kama earth inavujiwa umeme na earth hiyo ikagusana vizuri na ardhi kitakacho takiwa kutokea hapo ni short circuit ndo maana RCD inatakiwa ijizime.
hivyo kubadilisha earth load kunafanya ardhi ishikane vizuri na earth system yako hivyo hapo utakuwa unatengeneza short circuit,ndiyo maana kama earth system ina leakage baada ya kuufanya mfumo wake kuwa mzuri RCD inabidi ijizime mara tu bada ya kubadilisha earth load yako.
Nyumba ambayo mfumo wake wa earth ni mzuri mara nyingi kama inakuwa na leakage utakuta RCD au ERC yake inajizima mara kwa mara hiyo ni dalili kuwa kuna uwezekano wa uwepo wa leakage katika nyumba.
TATIZO LA LEAKAGE INAYO SABABISHA ONGEZEKO LA ZIADA LA BILI YA UMEME INAONDOLEWAJE?
Kuna vipimo vikuu vinne vinavyo takiwa kufanywa katika nyumba yako ili kutambua kama nyumba yako ina leakage ambayo inasababisha bili ya umeme kuwa kubwa au la,vipimo hivyo ni.
1.Earth continuity tester
2.Live and Neutral continuity tester
3.Neutral and Earth Continuity tester
4.Live and Earth continuity tester
Baada ya kufanya vipimo hivi mtaalamu wa umeme atajua kama nyumba yako ina tatizo la leakage iletayo ongezeko la bili kubwa ya umeme au la!
Vipimo hivi vinne kila kimoja kina kiwango chake cha usomaji hivyo majibu ya vipimo ndiyo yatakayo toa majibu harisi kuhusiana na afya ya wirering yako.
Tatizo la bili kubwa ya umeme katika nyumba yako linaweza kusababishwa na mambo mengi pengine ni zaidi ya leakage ya umeme;
Ni busara kufanya check-up itakayo ondoa tatizo na sio kuongeza tatizo.Kama unadhani unalipa bili ya umeme kubwa zaidi ya matumizi yako unaweza kuwasiliana nasi kwa ushauri zaidi wa kitaalamu kwa namba 0657-115587.