Utatuzi wa wamachinga ilikuwa ni kuwatoza kodi. Hiyo ndo ingeleta Win-Win kwa machinga na Serikali

Utatuzi wa wamachinga ilikuwa ni kuwatoza kodi. Hiyo ndo ingeleta Win-Win kwa machinga na Serikali

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Niliwahi kuleta uzi wangu hapa kuhusu hili suala mwezi August, kwenye stories of change kwa lengo la kutoa ushauri kwa serikali wa namna bora ya kukabiliana na hili suala.



Suala la 'Machinga Economy' lina pande mbili zenye uhalisia na ukweli.


1) Uhalisia wa kwanza ni kwamba, hawa machinga kuna kipato fulani walikuwa wanakitengeneza na ambacho kilikuwa kinawawezesha kuendesha maisha yao na familia zao. Huu ni ukweli dhahiri, ambao kila mmoja anaweza ku prove.

2) Uhalisia wa pili ni kwamba, ni kweli pia shughuli za wamachinga zilikuwa na sifa ya kufanyika bila utaratibu, hivo pia zilikuwa zinachangia pakubwa kwenye kuharibu taswira ya miji, majiji, na kuchafua pia mazingira.

Kwenye uchumi wowote ule, unavokuwa na two conflicting truths, kama hizo hapo juu, maana yake lazima kuwe na planning mechanism na decision making ambayo italeta mambo kwenye equilibrium.

Ndio tunachukia shughuli za wamachinga kwasababu zinaharibu mazingira, lakini kwani shughuli hizi za wamachinga si zimeajiri pia maelfu ya vijana na kupitia umachinga huu wameweza na wao kupata vipato vya kuendesha familia zao??

Kati ya mambo hayo mawili, kuna kimoja kinatengeneza positive externality (kipato na ajira) na kingine kinaleta negative externality (uchafuzi wa mazingira kutokana na hizi shughuli za umachinga)

Kwenye hali kama hii, ndipo sasa wachumi huwa tunatoa ushauri wetu.

Na mimi ushauri wa kwanza ilikuwa ni kwanza kufanya uhakiki na usajili wa shughuli zote za wamachinga, kisha baada ya hapo kuleta kodi ambayo ndiyo ingetuleta kwenye equilibrium.

Wazo langu mimi ilikuwa ni kwamba hawa wamachinga wangekuwa wanatakiwa kuanza kulipa kodi ama tozo kali sana ambazo hizo kodi zingetumika kurekebisha negative externality inayotokana na shughuli zao.

So, machinga ambaye angeshindwa kulipa kodi, ina maana anakuwa tayari anakosa sifa za kuendelea kufanya biashara kwa mujibu wa sheria.

So, in the long run, kwa kipindi hata cha miaka mitano hizi shughuli lazima zingekuwa automatically stabilized.

Na hapa ndipo tunaposema, kodi inaweza kutumika ku discourage baadhi ya shughuli.

*****
Yote nnayoshuhudia kwa sasa kuwaondoa kwa nguvu, naona itakuwa ni conter productive na inaweza kuleta violence au hata kusababisha vitendo vya kihalifu kuongezeka, kitu ambacho kitazidisha negative externalities.

Kwa hiyo itoshe tu kusema, sijafurahishwa na namna hili zoezi likivotekelezwa.

N.Mushi
 
Kodi ni wazo jema tu. Naamini hata serikali ingetamani kupata kodi. Ila zingatia hili: Ni kazi ngumu sana sana kukusanya kodi kutoka kwenye sekta isiyo rasmi. Sasa haina maana serikali itumie shilingi 100 kukusanya shilingi 10.

Ukweli mchungu ni kuwa hata sasa sheria za kodi zipo na hazitoi msamaha kwa hao tunaoita machinga lakini its has been practically impossible (inefficient?) kwa mamlaka za kodi kukusanya kodi. Hata hiyo Sh20,000 ni kizungumkuti tu. Halafu zikiingizwa na siasa za "wanyonge" hapo ndio kabisa, huwezi kukusanya kodi.

But nakubaliana na wewe kuwa tunahitaji kurudi kwenye drawing board ili kushughulika na wamachinga vizuri. Ni tatizo ambapo lina sura nyingi na hivyo solution yake inahitaji mapana na marefu katika kufikiri.
 
Solution sahihi ni kuwapanga kwenye maeneo yao sahihi na kuwawekea huduma zote muhimu kulingana na idadi yao... Jiji la Dar es salaam liwe na kanda kadhaa zenye maeneo makubwa yenye miundombinu yote ya kisasa na machinga wote wasajiliwe huko kwa kulipa tozo fulani fulani..
Hili lifanyike kwa mikoa yote na ziwe zinafanyika sensa za mara kwa mara ili maeneo yasizidiwe pia...

Kuwaacha Machinga kuvamiavamia kila mahala ni kero ambayo itakuwa inakua kila mara na population yao inaweza kuzidi hayo maeneo na kukwamisha mambo mengine maana hayo maeneo sio designed areas kwa machinga...
mfano eneo kama kariakoo ni kama lilikuwa limezidiwa na matokeo yake shughuli nyingine zilikuwa haziendi, mitaro kufulika uchafu, huduma ya usafiri kuwa ngumu, vyoo kuzidiwa, taswira ya mji kuharibika..

Wakati hiyo option ya kwanza inafanyika, Serikali pia ikune kichwa kutengeneza uchumi kwa hawa vijana kuwa wazarishaji baada ya kuendekeza huu uchuuzi, Uchumi wakimachinga unapaswa kuwa na limitations sio kuachia taifa lote kuwa na vijana wenye nguvu wamachinga..
 
Kwa ukweli wamachinga wametapakaa kila kona ya nchi sio Dar tu
Na kuwaondoa maana yake ni maelfu ya watu watakosa ajira

Wapo wengi ambao wamefanya hii biashara kwa miaka mingi na wana hela nzuri tu hata za kuweza kufungua duka kubwa tu ila kwa sababu system ndio imewabeba basi nao hawana budi kuwa machinga hata miaka 50

Kama Serikali inataka kukusanya kodi au hata ushuru inabidi pawe na sehemu nyingi za wao kufanyia kazi na hata sehemu zingine wanaweza kuwa wanafunga sehemu kwa siku hata 2 kwa wiki ili tupate mahitaji na wao pia wapate Riziki

Kuna sehemu za wazi pia
Njia zipo nyingi mbona ulaya biashara kama hizo zipo na wanapatikana hata kwenye parking za magari ambapo jumapili huwa wanapanga wao tu

Ila kama serikali imeamua kuwatimua tu tutegemee mengi
 
Utatuzi wa machinga ni kuufanya uchumi wetu usizalishe wamachinga, ziko sekta nyingi za uzalishaji na huduma ambazo zingechochewa na kuwekewa mazingira wezeshi tungeondoa hadi robo tatu ya wamachinga.

Tusifikirie kuligeuza taifa letu kuwa wachuuzi wa bidhaa za Kichina, maji, peremende na leso badala yake tufikirie kulifanya taifa hili la uchumi wa viwanda, utalii, kilimo, ujenzi, mitambo, mashine n.k
 
Nimekuja kuona kumbe machinga walivyokuwa maeneo ya mijini walikuwa wanapata chochote kwa urahisi kwa sababu walikuwa scattered, mfano Bagamoyo road; walikuwepo kuanzia Mwenge, Tangi bovu, Afrikana, Mbuyuni, hadi Tegeta, hapa utaona hawa walikuwa wanagawana riziki zao.

Kitendo cha kuwakusanya wote hao na kuwapeleka sehemu moja wakafanyie biashara zao mfano Bunju, hapa tayari patakuwepo na kugombania wateja na mostly naamini kipato chao cha siku wengi kitapungua na umasikini utaongezeka.

Nachokiona sasa, baadhi yao wameamua kuweka mabanda yao katikati ya mitaa, kwenye njia za ndani sio main road, ili angalau waendelee kubaki karibu na yale maeneo waliyokuwepo mwanzo yenye wateja wao, hivyo tutegemee baada ya muda mfupi, njia za kwenye mitaa nazo zitakuwa hazipitiki kwa urahisi, machinga watahamia huko.

Solution yako ya kukusanya kodi ni nzuri, lakini hujasema hiyo kodi itakusanywa kwa mtindo upi, kama ni ule wa Magufuli na zile elfu ishirini ambazo mwisho wa siku kelele zilikuwa zinapigwa pesa haijulikani zinakwenda wapi naona ule ulifeli.

Lakini pia, muhimu zaidi watafutiwe sehemu sahihi za kufanya biashara zao ili iwe rahisi kwa serikali kukusanya hizo kodi, mfano kule Machinga complex, kuna vizimba havina watu miaka yote kwasababu hapakuwepo na wateja wafanyabiashara wakapakimbia.
 
Tukipata kodi nyingi kabisa lakini magonjwa ya kuhara, kipindupindu na malaria vikawa sugu taifa litafaidi nini.

Uchafuzi wa mazingira ni hatari kwa afya ya mtu na nchi kwa ujumla, kodi ya machinga haiwezi kuzidi mapato ya watalii na wenye biashara halali
 
Nimekuja kuona kumbe machinga walivyokuwa maeneo ya mijini walikuwa wanapata chochote kwa urahisi kwa sababu walikuwa scattered, mfano Bagamoyo road; walikuwepo kuanzia Mwenge, Tangi bovu, Afrikana, Mbuyuni, hadi Tegeta, hapa utaona hawa walikuwa wanagawana riziki zao.

Kitendo cha kuwakusanya wote hao na kuwapeleka sehemu moja wakafanyie biashara zao mfano Bunju, hapa tayari patakuwepo na kugombania wateja na mostly naamini kipato chao cha siku wengi kitapungua.

Nachokiona sasa, baadhi yao wameamua kuweka mabanda yao katikati ya mitaa, kwwnye njia za ndani sio main road, ili angalau waendelee kubaki karibu na yale maeneo waliyokuwepo mwanzo, hivyo tutegemee baada ya muda mfupi, njia za kwenye mitaa nazo zitakuwa hazipitiki kwa urahisi, machinga watahamia huko.

Solution yako ya kukusanya kodi ni nzuri, lakini hujasema hiyo kodi itakusanywa kwa mtindo upi, kama ni ule wa Magufuli na zike elfu ishirini ambazo mwisho wa siku kelele zilikuwa zinapigwa pesa haijulikani zinakwenda wapi naona ule ulifeli.
Wamachinga wanachafua miji, hawatakiwi kuwepo barabarani hata wakilipa kodi kiasi gani.
Huko mitaani watakakoenda nako washugulikiwe, waende maeneo watakayopangwa
 
Mkuu mbona machinga walishaanza kulipa tangu enzi za magufuli ile elf 20 ya ujasiriamali, au ulimaanisha wakamuliwe kodi zaidi.

Serikali inadhani machinga ndo wanakwamisha wao kukusanya kodi stahiki kwa wafanyabiashara, lakini ukweli ni kwamba wafanyabiashara wa nchi za ulimwengu wa tatu ni wakwepaji wakubwa wa kodi ukilinganisha na wazungu.

Serikali watafute mbinu ya kukusanya kodi kwenye bidhaa na huduma bila kuathiri ufanyaji biashara wa makundi mbalimbali ya watu.

Ukiwaondoa wamachinga utakuwa umeathiri kundi kubwa la watu wenye kipato cha chini na kati wanaopata huduma zao kwa urahisi, haraka na nafuu mbali na kuondoa kundi kubwa la watu wanaopata vipato vyao kupitia biashara ndogo ndogo......​
 
Nyie ndiyo wasomi ambao mmeshindwa kutatua matatizo ya nchi hii. Yaani katika 'solution' zote hii ndiyo umekuja nayo?

Turudi kwenye utawala wa sheria. Sheria za kodi zinatakiwa kutaja kiwango cha mapato ambacho chini ya hapo mtu hatakiwi kulipa. Hili halifuatwi na mamlaka husika. Kwanza tunalipishwa kodi kabla ya mapato na hili halijawahi kuwa jambo sahihi.

Baada ya hapo kodi inapangwa kulingana na jinsi kipato kinavyoongezeka. Sasa wewe unataka serikali ijitungie tu kodi ili tu kuwakomoa hawa watu na mategemeo yako watatoweka?

Nasemaga kila siku, wasomi wa nchi hii wameathiriwa na elimu mbovu na siasa zetu. Hawana tena uwezo wa kutatua matatizo yetu.

Tukirudi kwenye utawala wa sheria, mambo yote yatakaa kwenye 'equilibrium' kama unavyotaka.
 
Hata mimi sifurahishwi na namna Serikali yangu inavyodili na Machinga. Baadhi yao wanadiriki kusema kuwa wanakomolewa kwasababu Rais Magufuli "aliwapenda".
 
Kwa ukweli wamachinga wametapakaa kila kona ya nchi sio Dar tu
Na kuwaondoa maana yake ni maelfu ya watu watakosa ajira

Wapo wengi ambao wamefanya hii biashara kwa miaka mingi na wana hela nzuri tu hata za kuweza kufungua duka kubwa tu ila kwa sababu system ndio imewabeba basi nao hawana budi kuwa machinga hata miaka 50

Kama Serikali inataka kukusanya kodi au hata ushuru inabidi pawe na sehemu nyingi za wao kufanyia kazi na hata sehemu zingine wanaweza kuwa wanafunga sehemu kwa siku hata 2 kwa wiki ili tupate mahitaji na wao pia wapate Riziki

Kuna sehemu za wazi pia
Njia zipo nyingi mbona ulaya biashara kama hizo zipo na wanapatikana hata kwenye parking za magari ambapo jumapili huwa wanapanga wao tu

Ila kama serikali imeamua kuwatimua tu tutegemee mengi
Utaratibu lazima ufuatwe
 
Utatuzi wa machinga ni kuufanya uchumi wetu usizalishe wamachinga, ziko sekta nyingi za uzalishaji na huduma ambazo zingechochewa na kuwekewa mazingira wezeshi tungeondoa hadi robo tatu ya wamachinga. Tusifikirie kuligeuza taifa letu kuwa wachuuzi wa bidhaa za Kichina, maji, peremende na leso badala yake tufikirie kulifanya taifa hili la uchumi wa viwanda, utalii, kilimo, ujenzi, mitambo, mashine n.k
Hii ndio hoja
 
Kilichoanza kufanyika ni maandalizi ya kuelekea huko.

Wanavyopangwa huko mbeleni maeneo yao yatajengwa vizuri na watawekewa vigezo na masharti ikiwemo kulipa kodi
 
Ukitoka hapo utasema bangi na madawa ya kulevya vitozwe Kodi maana ni biashara tamu
 
Utatuzi wa machinga ni kuufanya uchumi wetu usizalishe wamachinga, ziko sekta nyingi za uzalishaji na huduma ambazo zingechochewa na kuwekewa mazingira wezeshi tungeondoa hadi robo tatu ya wamachinga. Tusifikirie kuligeuza taifa letu kuwa wachuuzi wa bidhaa za Kichina, maji, peremende na leso badala yake tufikirie kulifanya taifa hili la uchumi wa viwanda, utalii, kilimo, ujenzi, mitambo, mashine n.k
Umeandika Point za maana.


Uzi ufutwe
 
Back
Top Bottom