SoC03 Utawala bora jamii itapona

Stories of Change - 2023 Competition

Msaleta mjt

New Member
Joined
Jun 6, 2023
Posts
1
Reaction score
0
1. Utangulizi
Utawala bora ni mfumo wa kisiasa, kiuchumi, kitamaduni na kijamii unaofuata kanuni za kisheria uliojaa uwazi, uwajibikaji na uwazi wenye kuleta tija katika jamii. Katika andiko hili nitazungumzia matatizo yanayoikumba jamii ya kitanzania mambo halisi ambayo hufanywa na viongozi na mbinu ambazo zinatakiwa zitumike ili kuyafikia mahitaji ya wananchi katika jamii.

Watanzania wanapata changamoto nyingi sana katika maisha ya kila siku tatizo kubwa likiwa ni umasikini na ukosefu wa huduma bora katika jamii zao ikiwemo elimu, afya, maji na kadharika. Hivyo katika andiko hili tutaangalia namna jinsi utawala ukiwa bandia huzidisha matatizo mengi katika jamii lakini kama utawala utafata misingi bora basi jamii itapona katika wimbi la umasikini na mengine mengi.

2. Madhara na sifa za utawala usio bora
Hapa chini ni baadhi ya madhara na sifa za utawala usio bora nchini yaletwayo na viongozi.
(a) Rushwa: Katika jamii zetu za kitanzania tafta nyingi na uhalisia vinaonyesha jinsi viongozi wengi hupenda rushwa ili kufikisha huduma kwa watu. Kwa maana nyingine wananchi hukosa huduma bora katika taasisi mbalimbali kwa sababu hawawezi kuwapa viongozi kitu chochote. Ukienda mashuleni, maofsini, mahospitalini rushwa zimeshamiri sana.

(b) Ubadhirifu.
Ni dhahiri kuwa viongozi wengi ni wabadhirifu sana katika mali za umma. Kila siku vyombo vya habari huripoti matukio mbalimbali kuhusiana na ubadhirifu wa fedha na mali nyingi za umma, jambo ambalo hupunguza ufanisi wa kuitawala ndani ya nchi. Matokeo yake ni kwamba wananchi wanashindwa kupata haki zao katika kutumia mali za nchi yao ili kufanya maendelea badala yake huzidi kuishi katika maisha duni na umasikini ulioshamiri.

(c) Kutowashirikisha wananchi katika mambo mbalimbali yanayowahusu: Ukweli usiopingika katika utawala wakileo ni kutowashirikisha watu katika mambo yanayohusu maisha yao ikiwemo uchumi, afya, elimu na mambo kadha wa kadha ambayo ni muhimu sana. Jambo hili limekuwa ni tatizo kubwa sana hasa pale ambapo serikali huamua jambo na kuhitaji wanachi walitekeleze badala yake wananchi kukataa kabisana kuwa na mwamko hafifu katika kutekeleza mipango iliyowekwa na serikali.

(d) Kutopeleka mamlaka na haki ya kufanya maamuzi katika ngazi za chini: Hili pia limekuwa ni changamoto kubwa katika halmashauri nyingi Tanzania. Viongozi wanakuwa na nguvu zote na mamlaka yote ya kufanya na kuamua mambo wao wenyewe bila ya kutoa nafasi katika ngazi za chini kama vile serikali za mitaa ili kuona, kujadiri na kuamua mambo yao wenyewe na kuwasilisha katika serikali kuu. Jambo hili linazidi kuleta utata kwa wananchi kwani viongozi ndio hufanya maamzi bila kujali watu wanataka nini.

(e) Kunyanyasa wananchi: Yapo mambo mengi sana yafanywayo na viongozi wakidhani tenda haki kwa kivuli cha sheria badala yake huwanyanyasa wananchi. Viongozi wengi hufanya vitendo vya kikatili wawapo maeneo yao ya kazi lakini pia kutojali haki zao za msingi kama raia wa nchi yao. Wengi wao hukosa huduma zao bora na kuishia kukadhamizwa na viongozi wenye nguvu.

(f) Kutowajibika na kukosa uwazi: Serikali yetu ya Tanzania ina viongozi wengi wasiotambua na kutimiza majukumu yao, sambamba na hilo sio wawazi. Hili hutokana na ubinafisi wao wenyewe na kukidhi mahitaji ya familia zao lakini waanashindwa kutambua jukumu la kuwa kiongozi ni kuwatumikia watu. Viongozi wengi katika ngazi tofauti tofauti hawatamizi wajibu piaa ni waongo. Yapo mambo mengi sana ambayo serikali yetu hukumbana nayo na hayo ni baadhi tu.

3. Mbinu na njia ambazo zikifuatwa zinaweza kuleta matokeo chanya na tija katika jamii za kitanzania. Kwa uelewa wangu kam mtanzania napendekeza mambo yafuatayo;

(a) Kupeleka madaraka katika ngazi za chini za uongozi: Serikali inatakiwa kuwapa viongozi wa chini zikiwemo serikali za mitaa uhuru wa kufanya uamuzi wao wenyewe katika mambo yanayowahusu. Hili litasaidia kuimarisha mfumo bora wa ushirikiano kati ya wananchi na serikali katika kufanikisha mingango bora na mahisusi.

(b) Viongozi kusikiliza mambo yanayowahusu wananchi moja kwa moja. Kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari na mikutano ya hadhara itakuwa rahisi sana kwa viongozi kutambua matatizo yanayokumba jamii za watanzania na kupata mwongozo bora wa kuyatatua.

(c) Kuimarisha mifumo mizuri ya kushirikiana na wananchi. Serikali inatakiwa kuunda programu ambazo zitawezesha kukutana na watu katika mambo mbalimbali ili kuimarisha ushirikiano mzuri baina ya watu na serikali. Hili litawezesha jamii kuwa wepesi katika kutekeleza mambo yatokayo katika serikali na utekelezaji huu utakuwa wa kiufanisi wa hali ya juu.

(d) Serikali kwa kushirikiana na wananchi waweke mfumo mzuri kwa kupambana na kuwaondo viongozi wasio bora: Lengo kubwa ni kuwafanya viongozi watambue majukumu yao na kuwajibika, kutetea watu, kukimbia rushwa na kijan mali za umma. Hili likiwa limefanikishwa basi mfumo wa utawala utakuwa bora na matatizo mengi ya wananchi yatatatuliwa kiufasaha zaidi.

(e) Serikali inatakiwa kuboresha mifumo ya kiuchumi ikiwemo masoko kisiasa, kijamii na kukagua huduma za kijaa kama vile mawasiano, teknolojia na science, elimu, umeme, afya na kadharika. Hili litasaidia watu kujikita zaidi katika uzalishaji na biashara pia watu wataelimika na kuingiliana ili kufanikisha malengo yao na kuondokana na uchumi. Lakini pia itasaidia serikali kukuza uchumi na mapato ya nchi yatakuwa ya juu pia utawala utaimarika.

Pia katika andiko hilo nimeorodhesha sifa za viongozi na utawala bora na mifano ya kivitendo. Hapa chini ni baadhi ya sifa za uongozi bora na mifano ya vitendo ambavyo viongozi bora hufanya:

Uwazi na Uaminifu: Viongozi bora wanajenga uaminifu na uwazi katika uongozi wao. Wao hufanya maamuzi kwa uwazi na hutoa maelezo yanayoeleweka kuhusu mchakato wa maamuzi na sababu zilizopelekea uamuzi huo. Pia, viongozi hao hushiriki taarifa muhimu na kuwajibika kwa uwajibikaji wao.

Mfano wa vitendo: Kutoa taarifa na maelezo yanayoeleweka kwa umma kuhusu sera, mipango, na maamuzi ya kiutawala. Kuweka mifumo ya kushughulikia malalamiko na kufanya uchunguzi wa uwajibikaji kwa uwazi na haki.

Uongozi wa Kusikiliza: Viongozi bora hufahamu umuhimu wa kusikiliza na kuelewa mahitaji, wasiwasi, na maoni ya watu wanaowaongoza. Wanawasiliana vizuri na kuwapa fursa watu kutoa maoni yao na kushiriki katika mchakato wa maamuzi.

Mfano wa vitendo: Kufanya mikutano na vikao vya mashauriano na wadau mbalimbali na kusikiliza maoni yao. Kujenga mifumo ya kushirikisha umma katika mchakato wa maamuzi na kufanya maamuzi kwa msingi wa ushauri na tafiti.

Uongozi wa Ushirikiano: Viongozi bora wanatambua umuhimu wa ushirikiano na kushirikiana na wadau wengine ili kufikia mafanikio. Wanajenga timu imara na kuwawezesha watu kufanya kazi pamoja kwa mshikamano na kushirikiana kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya.

Mfano wa vitendo: Kukuza ushirikiano na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali, kama serikali, mashirika ya kiraia, na sekta binafsi, katika kubuni na kutekeleza sera na mipango. Kufanya majadiliano na mashauriano ya mara kwa mara na wadau na kuwashirikisha katika maamuzi muhimu.

Uongozi wa Ubunifu: Viongozi bora wanakuwa na uwezo wa kufikiri ubunifu na kuleta mabadiliko. Wanatambua umuhimu wa kubadilika na kuzoea mazingira ya haraka na kufanya mabadiliko yanayohitajika ili kukabiliana na changamoto za kisasa na kuleta maendeleo endelevu.

Mfano wa vitendo: Kuhamasisha ubunifu na kusaidia mawazo mapya na ufumbuzi katika kutatua matatizo ya jamii. Kuendeleza mazingira ya kuunga mkono uvumbuzi na kusaidia utekelezaji wa miradi na mipango inayohamasisha ubunifu.

4. Hitimisho
Ni muhimu sana jamii yetu ya kitanzania kutambua misingi wa utawala bora ili kuleta mabadiriko ndani ya jamii zetu. Viongozi wanatakiwa kufuata misingi, kanuni na taratibu na kutumia taranta zao za kiuongozi ili kujenga utawala bora na kuleta mtazamo mpya katika jamii. Kwankufuata haya serikali itakuwa bora na mifumo yake itakuwa imara katika kupigania masilahi ya watu katika jamii. Hivyo ni muda wa viongozi kuamka na kuandaa kesho yetu na taifa letu.
 
Upvote 0
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…