SoC02 Utawala Bora katika kujenga taifa lenye maendeleo na uchache wa migogoro

SoC02 Utawala Bora katika kujenga taifa lenye maendeleo na uchache wa migogoro

Stories of Change - 2022 Competition

Mzaliwaa

New Member
Joined
Sep 13, 2022
Posts
2
Reaction score
1
Utawala ulio bora hujengwa kwa vitu viwili muhimu ambavyo ni MFUMO na WATU ambao ndio viongozi walio katika utawala. Mfumo ni mpangilio wa jinsi jambo au mambo yatakavyofanyika na Watu ndo husimamia, huendesha na kutekeleza mambo yaliyo ndani ya mfumo. Pia watu ndio watekelezaji wakuu wa majukumu na vitu vyote vilivyoundwa na mfumo ili kuhakikisha kila kitu kiko katika mstari ulinyooka na vinakwenda sawia.

Wananchi huwa na dukuduku huponda utawala uliopo kutokana na mambo makuu mawili ambayo ni;
A: Yale wanayoyaona; wananchi huwa na maswali mengi kutokana kile wanachokiona kwa kutazama utekelezaji ambao huenda ukaleta utofauti na uzuri au ubaya wa jambo fulani au kile kinachofanyiwa kazi.
B: Yale yanayofanywa; wananchi huuliza hiki na kile kutokana na matendo ambayo hufanywa na viongozi walio katika mfumo ambao huleta picha na mtazamo tofauti na vile waonavyo wao. Je hiki kilichofanyika ni sawa na kina tija katika taifa?. Je kinachochea mafanikio au ni kwa sababu kinatakiwa kufanyika?.

Mfumo bora huundwa na watu walio bora wenye mapungufu kiasi na sio watu walio kamili, maana hakuna aliye kamili. Kwa kama mfumo ni hafifu basi watu wanaouendesha na kuusimamia huo mfumo (viongozi) hawana tatazo, na kama watu ndio changamoto maana mfumo hauna tatizo bali wanaousimamia na kuundesha basi wanafanya vitu kwa maslai yao au kwa sababu ndivyo ilivyozoeleka. Utawala hauwezi kuwa bora siku zote maana mapungufu yapo lakini kuwepo kwa watu makini wanaopunguza mapungufu katika sehemu zao za kazi basi ndio huchochea utawala bora.

Pia utawala ulio bora huendana na siasa zilizo na tija zenye mashiko zinazochechea maendeleo hata kama ni kutoka katika chama cha upinzani na chama tawala ili hali wote mko katika mfumo mmoja wa uendeshwaji na mnasimamia misingi iliyo sahihi na kutekeleza yaliyo sahihi. Kampeni ndio hututofautisha kwamba mimi ni chama cha upinzani na wewe lakini maendeleo ni kwa sisi wote, kwa maana likijengwa daraja mtu wa CCM atapita, wa CHADEMA atalitumia, wa CHAUMA na vyama vingine vyote na hata wale wasio na vyama watalitumia katika shughuli zao za kila siku.

Kuthamini mawazo na hoja mbalimbali zenye tija baina ya viongozi wote wa vyama vyote ni jambo la muhimu maana ndio huchochea maendeleo kwa kutazamia ni nini hasa hasara na faida za mapendekezo yaliyotolewa na fulani na je yatatufikisha katika yale tunayoafikia baada ya muda kufikia au lahasha.

NA HAYO NDIYO HULETA NA KUCHOCHEA UTAWALA ULIO BORA WENYE MAENDELEO NA MAFANIKIO YA MUDA MREFU....
 
Upvote 1
Back
Top Bottom