SoC02 Utawala Bora kwa amani na maendeleo endelevu

SoC02 Utawala Bora kwa amani na maendeleo endelevu

Stories of Change - 2022 Competition

Viola Costantine

New Member
Joined
Jul 25, 2022
Posts
1
Reaction score
6
UTANGULIZI.

Utawala Bora ni nini?

Ni utaratibu wa kutumia madaraka ya Umma,kusimamia haki za binadamu, rasilimali na kuzitumia kuboresha Maisha ya wananchi. Utawala Bora huzingatia sheria na taratibu zilizopo nchini na kuleta amani na maendeleo ya nchi. Utawala Bora tunaupata endapo tutakua na Viongozi Bora hivyo wananchi tunapaswa kuchagua viongozi Bora kuanzia viongozi wa juu adi wa chini ili kuleta maendeleo kwa jamii. Katika Utawala Bora Viongozi hutumia vizuri madaraka na rasilimali za taifa kwa manufaa ya wananchi.

Utawala Bora ushirikisha Taasisi na Asasi mbalimbali ili kuhakikisha ushirikiano na kutekeleza majukumu mbalimbali kiufanisi kuleta amani na maendeleo nchini. Taasisi na Asasi hizo ni kama;
❖Sekta binafsi, hizi zina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo nchini na maendeleo hayo ni kama vile, Afya, Elimu, Uchumi, Maendeleo ya miji na Ajira, hivyo basi Utawala Bora huzipa sekta binafsi nafasi ya kuwekeza maeneo mbalimbali ili kuchangia uchumi wa Taifa.​
❖ Asasi za kiraia, ni asasi zisizo za kiserikali na hufanya kazi nje ya serikali na hulenga kunufaisha Umma. Asasi hizi hujumuisha mashirika na taasisi za kijamii, pia huzingatia haki za binadamu, usawa, uwazi na ushirikishwaji, Mfano wa Asasi za kiraia ni Tanzania Media Women Association (TAMWA) ambayo hupambania haki za binadamu hasa wanawake na Watoto, pia Haki Elimu ambayo husimamia maswala ya elimu kwa kusimamia misingi ya uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji.​


UTAWALA BORA HUZINGATIA MAMBO YAFUAYAYO.
❖ Ushirikishwaji, tunapokua na Utawala Bora wananchi hushirikishwa katika maswala mbalimbali ya maendeleo na maendeleo huletwa na wananchi husika. Wananchi wanashirikishwa kwa kuhudhuria mikutano katika maeneo yao kama vijiji, vitongoji na mitaa na kupewa nafasi ya kusikilizwa na kueleza mawazo yao na kuwaeleza viongozi juu ya ufanisi katika utendaji wao.​
❖ Uwajibikaji na Uwazi, Utawala Bora hutekeleza majukumu mbalimbali mfano kutatua migogoro na kutekeleza majukumu mengine ipasavyo ili kuleta amani na maendeleo.Utawala huo unakuwa wazi na kuwafahamisha wananchi mara kwa mara juu ya mambo mbali mbali yanayoendelea na wananchi kutoa tathimini juu ya utendaji wa utawala huo.​
❖ Demokrasia, ni mfumo unaowapa wananchi uwezo wa kushiriki na kufanya uamuzi katika maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi pia watu wote huwa sawa mbele ya sheria. Wananchi hushiriki katika maswala haya moja kwa moja, mfano kipindi cha uchaguzi kupiga Kura. Demokrasia husaidia kuleta Amani na Maendeleo.​
❖ Kutawala kwa Sheria, katika Utawala Bora kila mtu natakiwa kuongozwa na kuzingatia sheria na katiba ya nchi pia utaratibu uliopo nchini. Viongozi wanatakiwa kuongoza na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba na sheria na hawatakiwi kuwa juu ya sheria wala kukiuka sheria na katiba.​
❖ Haki na Usawa, Utawala Bora husimamia haki na usawa kwa wananchi hasa viongozi wanapotekeleza majukumu yao bila ubaguzi, upendeleo na uovu wa aina yoyote ili kuwapa wananchi tumaini la kushirikiana na viongozi kuleta maendeleo nchini.​


YAFUAYAYO NI MAMBO YANAYOPATIKANA KATIKA UTAWALA BORA.
❖ Haki za binadamu na usawa, taifa lolote lenye Utawala Bora huzingatia upatikanaji wahaki za binadamu na usawa kwa watu wote bila uonevu na ubaguzi wa aina yoyote.​
❖ Huduma Bora za jamii, upatikanaji wa huduma bora za kijamii katika taifa lenye Utawala Bora huwezekana kwa sababu rasilimali za taifa hutumika kwa manufaa ya wananchimfano, afya, maji, elimu na miundo mbinu kama barabara.​
❖ Matumizi mazuri ya rasilimali, taifa lenye Utawala Bora viongozi wake hutumia vizuri rasilimali za taifa ili kuleta maendeleo ya wananchi na siyo maendeleo binafsi.​
❖ Amani na utulivu, amani na utulivu hupatikana ndani ya taifa lenye Utawala Bora kwani uongozi uliopo hutekeleza majukumu yake ipasavyo,hutumia rasilimali za nchi vizuri kwa manufaa ya wananchi, huduma za kijamii hupatikana, haki za binadamu na usawa kwa usitawi wa taifa.​
❖ Maendeleo endelevu, ni utaratibu wa kupanga na kuandaa malengo ya maendeleo ya badae na kutoa huduma za kijamii na utumiaji wa rasilimali vizuri. Maendeleo endelevu huondoa umasikini, njaa, na kuleta usawa wa kijinsia na haki za binadamu, hivyo Utawa Bora hupigania hayo yote.​
❖ Kutokomeza rushwa, rushwa ni kitu chochote cha thamani anachopewa mtu mwenye mamlaka juu ya jambo flani ili mtu binafsi apate kunufaika. Hivyo basi rushwa ni adui wa haki na nchi yenye Utawala Bora hupambana dhidi ya rushwa na kuleta maendeleo nchini.​
❖ Kupunguza umasikini, umasikini ni hali ya mtu au jamii kutokuwa na uwezo wa kupata mahitaji mhimu mfano, chakula, huduma za afya na maladhi. Utawala Bora husaidia kupunguza umasikini kwa kushirikiana na taasisi na asasi mbalimbali ili kuleta maendeleo hasa kwa watu wenye maisha ya hali ya chini.​
TAIFA LISILO NA UTAWALA BORA HUKUMBWA NA CHANGAMOTO ZIFUATAZO.
❖ Rushwa, nchi yoyote isiyokua na Utawala Bora rushwa inatawala na kupelekea kutokuwepo kwa haki za binadamu, uoneaji na maendeleo ya nchi.​
❖ Migogoro, ni mvutano baina ya pande mbili au Zaidi na hupelekea kutokuwepo kwaamani. Nchi zenye migogoro husabababishwa na kukosa Utawala Bora na kupelekea kukosekana kwa haki za binadamu, huduma za kijamii, matumizi mabaya ya rasilimali na kukosekana maendeleo.​
❖ Kukiukwa kwa haki za binadamu, kama nchi haina Utawala Bora haki za binadamu haziwezi kuzingatiwa, mfano ushirikishwaji katika maswala ya maendeleo na wananchi kukosa nafasi ya kueleza mawazo yao.​
❖ Utakatishwaji wa rasilimali za umma, nchi ikikosa Utawala Bora rasilimali hutumiwa na watu wachache kwa manufaa binafsi na si kwa manufaa ya wananchi.​
❖ Kutokuwepo maendeleo endelevu, Taifa lisilo na Utawala Bora halina maendeleo endelevu kwa sababu rasilimali hutumiwa vibaya pia viongozi hushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kupelekea kutokuwepo kwa huduma bora za jamii namaendeleo.​

Tuna mifano ya mataifa Afrika yenye Utawala Bora na wana maendeleo mazuri, amani na utulivu vilevile mataifa yasiyokua na utawala Bora na wanakumbwa na changamoto mbalimbali kama kukosa haki za binadamu, utumiaji mbaya wa rasilimali na kupelekea kukosekana kwa amani na maendeleo mfano ni Libya, Somalia.


HITIMISHO.
Utawala Bora huimarika zaidi kama mambo mhimu yanayopatikana katika Utawala Borayatazingatiwa na kutatua changamoto zinazotokana na kutokuwepo Utawala Bora. Tunaonamadiwani wanatakiwa kutimiza wajibu wao na kutatua changamoto za wananchi pia kuwa wazi na kuwaeleza wananchi mambo yanayoendelea ili wananchi washirikiane na viongozi kuleta Amani na Maendeleo.

Imeandikwa nami Viola Costantine.
Karibuni msome na kunipigia Kura.
 
Upvote 6
Back
Top Bottom