UTAWALA BORA: Mambo yanayohifadhi Uhuru wa Mahakama

UTAWALA BORA: Mambo yanayohifadhi Uhuru wa Mahakama

Status
Not open for further replies.

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
20210329_065838_0000.png


Uhuru wa Mahakama unamaanisha kuwa kila Jaji au Hakimu yuko huru kuamua kesi iliyopo mbele yake kwa mujibu wa Sheria na ushahidi ulioletwa mbele yake, na katika kutekeleza majukumu hayo, hapaswi kuingiliwa, kushawishiwa au kushinikizwa na mtu au chombo chochote, ikiwemo Bunge na Serikali kama inavyoelezwa katika Ibara ya 107B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Hivyo, dhana ya Uhuru wa Mahakama inaitaka Mahakama kutekeleza majukumu yake bila woga wala upendeleo.

Uhuru wa Mahakama unahifadhiwa na kulindwa katika maeneo manne ambayo ni:

i) Kuzuia kuondolewa kwa Jaji au Hakimu katika ofisi bila ya sababu za msingi na bila ya kufuata taratibu zilizowekwa hata kama kuna sababu za kumuondoa,

ii) Kuweka kinga ya kutoshtakiwa kwa Jaji au Hakimu kwa makosa yoyote, yawe ya jinai au madai kutokana na maamuzi yake ya kimahakama aliyoyafanya

iii) Kutopunguza au kuondoa mishahara na maslahi ya Jaji au Hakimu

iv) Kutokuwa na vyeo kwenye vyombo vingine vya dola au kushiriki katika shughuli za vyama vya siasa.

Hata hivyo, ni vema ikafahamika kwamba Uhuru wa Mahakama sio kibali kwa Jaji au Hakimu kuamua kesi kwa namna anavyojisikia yeye au kwa matakwa yake.
 
Upvote 0
Hiyo ni sawa kabisa na katiba yetu imeelezea vizuri, lakini changamoto iliyopo ni kwamba upatikanaji wa jaji mkuu na mwanasheria wa serikali, wote wanatokana na uteuzi toka kwenye muhimili mwingine wa serikali,


Hivyo kwa namna moja ama nyingine lazima mteuzi aweke mtu ambae atakuwa na maslahi kwake, ndo mana kwa mienendo ya nchi yetu tunaona wazi hakuna SEPARATION OF POWER, Mh president anaingia popote k2a muda na saa yoyote,
 
Ingependeza sana katika hyo katba mpya hiki kipengere kizingatiwe sanaa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom