joshydama
JF-Expert Member
- May 10, 2016
- 4,623
- 5,039
Habari zenu wanafamilia na waheshimiwa wa mtandao wa Jamii forums? Ni matumaini yangu kwamba mu wazima wa afya njema kabisa na mnaendelea vyema katika ujenzi wa taifa letu.
Napenda kuchukua wasaa huu kuzungumzia suala la umuhimu wa utawala bora na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Mabibi na mabwana, dhana ya utawala bora na maendeleo ya jamii ni vitu viwili ambavyo huwezi kuvitenganisha yaani ni pande mbili za shilingi.
Nini maana ya dhana ya utawala bora? Dhana ya utawala bora inaweza kuelezewa katika mitazamo mbalimbali kulingana na uelewa wa mtu na mtu. Ingawa utawala bora ni dhana ambayo msingi wake umejikita katika uwajibikaji, ushirikishwaji na uwazi kwa wanajamii katika nyanja mbalimbali ya maendeleo ya jamii. Nyanja hizo ni:-
a) Kiuchumi
b) Kijamii
c) Kisiasa.
Kadhalika, kuna hii dhana ya utawala bora ina viashiria vyake ambavyo vikipatikana katika jamii basi hutushawishi kwamba katika jamii fulani au Nchi fulani kuna utawala bora. Ndugu wana JF, yafuatayo hapa chini ndiyo mambo ambayo huashiria utawala bora katika Nchi au jamii fulani. Mambo hayo ni kama ifuatavyo:-
i) Utawala wa sheria
ii) Haki na usawa.
iii) Demokrasia
Utawala bora huzingatia utawala wa sheria. Utawala wa sheria ni moja ya nguzo muhimu sana katika utawala bora kwa sababu husaidia mambo yafuatayo:-
i) Huleta usawa na kuheshimu haki za raia mfano haki ya kuishi kama inavyotajwa katika ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, haki ya uhuru wa maoni katika ibara ya 18 ya JMT, haki ya kufanya kazi katika Ibara ya 22, Haki ya kupata ujira wa haki katika Ibara ya 23 na haki ya kumiliki mali, pia panakuwepo na haki sawa mbele ya sheria yaani hakuna aliyejuu ya sheria. Ingawa hili jambo la kusema kwamba watu wote ni sawa mbele ya sheria limeshindwa kutekelezeka ambapo kuna baadhi ya viongozi wana kinga ya kutokushitakiwa mfano Rais wa Nchi yetu ana kinga hivuo hawezi kushitakiwa kwa makosa aliyoyafanya wakati akiwa katika uongozi.
ii) Utawala bora huzingatia demokrasia iliyo bora
.Hapa ndipo tunaona wananchi wanapata haki yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka. Pia kuna uhuru wa kujikosoa na kukosoana. Uhuru wa kupinga jambo kwa hoja, uhuru wa kutoa maoni. Katika uchaguzi wa mwaka 2020 tuliona ni kwa namna gani suala la demokrasia nchini Kwetu bado ni tatizo kubwa sana ambapo wananchi walinyimwa haki zao za kuwakilishwa na viongozi waliowachugua, tunaona serikali inavyozuia mikutano na shughuli za kisiasa nchini.
iii) Ushirikishwaji wa jamii katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo mfano katika suala la kutunga sheria ambazo huathiri moja kwa moja wananchi. Hivyo ni lazima wananchi washirikishwe katika hatua zote za utungaji sheria kwa ajili ya kutoa maoni yao juu ya hiyo sheria faida na madhara ya sheria husika.
.Mfano hivi karibuni kumezuka malalamiko makubwa sana ya wananchi na wawekezaji kutokana kodi ya mshikamamo(solidarity tax) ambapo sheria hiyo ya kodi ya kutoza miamala kwa njia ya simu ilitungwa bila kuwashirikisha wananchi kitu ambacho kimeleta vilio vikubwa sana kwa wananchi na wawekezaji nchini.
iv) Uwazi
. Dhana hii ya uwazi inahitaji kwamba kila kinachofanywa na serikali na ambacho kitawagusa wananchi kwa namna moja au nyingine lazima pawepo uwazi. Ni lazima Wananchi wajulishwe juu hilo jambo pasipokuwa na siri zozote. Mfano tumekuwa tukishuhudia serikali ikiingia mikataba ya aina mbalimbali bila kuweka wazi, ununuzi wa wa ndege, ujenzi wa miradi mikubwa nchini. Hivyo basi kutokuwepo kwa uwazi husababisha kuwepo kwa ubadhirifu wa mali, rushwa na matumizi mabaya ya mali za Umma.
#MADHARA YA KUTOKUWEPO KWA UTAWALA BORA.
i) Husababisha uvunjifu wa haki za binadamu mfano ya haki ya kuishi, haki ya kutoa maoni, haki ya kukusanyika, haki ya kufanya kazi n.k.
ii) Husababisha Rushwa na ubadhirifu wa mali za Umma mfano EPA, ESCROW n.k
iii) Husababisha kuwepo kwa sheria kandamizi mfano Sheria mpya ya mashikamano, Sheria mpya ya uvuvi, sheria mpya ya ubashiri.
iv) Kutokuwepo kwa uwajibikaji mfano kipindi cha EPA, ESCROW hakuna kiongozi yeyote aliyewajibishwa kufuatia huo uhujumu uchumi uliofanyika.
#MAPENDEKEZO
. Ili pawepo na utawala bora na maendeleo yaliyo bora nchini Tanzania suala la katiba mpya ni suala ambalo ni la msingi sana na kitu ambacho hakiwezi kukwepeka. Napendekeza katiba mpya iwe na mambo yafuatayo:-
a) Katiba ieleze mfumo bora wa elimu nchini Tanzania. Mfumo bora ni pamoja na kuthamini na kuyapa kipaumbele masomo ya ufundi na vipaji nchini Tanzania. Mwanafunzi apewe haki ya kufanya uchaguzi katika masomo anayopenda.
b) Suala la ajira liwe ni haki ya msingi kama ilivyo haki ya kuishi. Kama mjuavyo suala ajira limekuwa ni Tatizo sana nchini Tanzania. Hivyo basi inabidi katika katiba mpya inabidi ieleze haki hiyo kama ni ya msingi na inabidi serikali iweke mazingira mazuri na yaliyosafi katika utoaji wa ajira na na kuhakikisha inawasaidia vijana au watu wa rika yoyote wanajiajiri. Mambo ya kufanya ili kuboresha ajira ni pmoja na kupunguza kodi kwa wanaoanza maisha ya kujiajiri katika nyanja mbalimbaku mfano katika TEHAMA n.k, kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vijana au wananchi wote.
c) Uwajibikaji wa viongozi
. Serikali inabidi iruhusu mchakato wa katia mpya ili hiyo katiba mpya itakayotungwa iondoe kinga na kuruhusu viongozi wasio waaminifu na watakaovunja katiba kushitakiwa kwa makosa ya jinai. Hii dhana ya uwajibikaji itasaidia kupunguza na kuondoa kabisa ubadhirifu, rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na matumizi mabaya ya mali ya Umma. Kadhalika wananchi wapewe mamlaka ya moja kwa moja ya kuwawajibisha wawakilishi wao kule bungeni pindi wanapotenda kinyume na matakwa ya wananchi.
d) Katiba mpya ibainishe wazi sifa na mchakato mzuri wa kuwapata viongozi wa Umma mfano RC, DC. Hili litasaidia kupata viongozi wenye sifa na wanaostahili.
e) Ushirikishwaji wa moja kwa moja kwa wananchi juu ya utungaji wa sheria.
. Katiba mpya itoe mwanya wa moja kwa moja kwa wananchi wa tabaka zote katika kushiriki juu ya utungwaji wa sheria hizo ili kuondoa sheria kandamizi na ambazo hazigusi maslahi yao bali hugusa maslahi ya watu wachache.
f) Pawepo na tume huru ya uchaguzi.
.Tume huru ta uchaguzi isiyofungamana na chama chochote cha siasa itasaidia kuboresha suala la demokrasia nchini hasa katika mchakato wa kuwachagua viongozi wa nchi.
g) Mgombea binafsi. Ili pia kuboresha demokrasia nchini Tanzania itabidi katiba mpya iruhusu suala la mgombea binafsi kwani itaongeza utendaji kazi nchini Tanzania.
h) Serikali iwe na jukumu la kutunza wazee. Kama ilivyo nchi nyingi zilizoendelea itakuwa vyema sana kama Serikali itachukua jukumu la kuwayinza wazee.
i) Katiba mpya ieleze kuhusu uhuru wa kujitoa, kuchagua, kuhama na kujinga katika mifuko ya jamii. Na hii haki iwe ni haki ya kikatiba na si vingenevyo. Mfano kwa sasa tunashuhudia kuwepo kwa sheria kandamizi ya NSSF inayozuia fao la kujitoa. Hii sheria ni kikwazi kijubwa sana kwa vijana hasa wale wanaohitaji haki yao ili wakajiajiri.
h) Pawepo na haki sawa ya maendeleo kwa wananchi au kufaidi keki ya taifa. Hapa inabidi katiba mpya ieleze bayana kwamba suala la maendeleo ni kwa wote bila kujali sehemu, hali, kabila n.k mfano suala la maji, umeme, barabara, huduma za afya liwe ni jambo la kikatiba na liweke katika haki za msingi. Hii itasaidia kupeleka maendeleo sehemu zote za vijijini kwa kuhakikisha mapato yanayopatikana yanajenga miundombinu sehemu za vijijini, kujenga hospitali na vituo vya afya, kupeleka umeme, kujenga masoko makubwa sehemu za vijijini n.k.
Mwisho, utawala bora, siasa bora itasaidia kuleta maendeleo katika jamii, itapunguza tatizo la ajira kwa sababu tutapata wawekezaji wa kigeni na wenyeji ambapo wananchi watapata ajira, serikali itaongezeka wigo wa mpana wa mapato, pia walipa kodi wakiongezeka itasaidia kupunguza mzigo mkubwa wa kodi kwa mwananchi wa kawaida.
Ahsanteni na karibuni kwa michango.

Upvote
1