SoC03 Utawala Bora na Uwajibikaji ni chachu ya Maendeleo

SoC03 Utawala Bora na Uwajibikaji ni chachu ya Maendeleo

Stories of Change - 2023 Competition

taj mashair

New Member
Joined
Jun 8, 2023
Posts
3
Reaction score
2
Hii ni kampuni ambayo ilikufa kutokana na utawala wao mbovu hasa kwa walio juu yaani mkurugenzi na mameneja kwani walikuwa wakiwaendesha sana wenzao wa chini waliokuwa wafanyakazi wenzao ambapo wengi wao waliomba kuacha kazi na kuhama na wengine walikuwa hawafanyi kazi kwa ufanisi na weledi hali ambayo hata huduma walizozitoa hazikuwa na ubora na wateja hawakuridhika nazo, hali hii ilipelekea kampuni kuzorota kimaendeleo na kufa kabisa.

Lakini kampuni hii ilikuwa ikishindana katika soko na wateja na kampuni nyingine ambapo hii kampuni nyingine baada ya kampuni ya kwanza kufa, hii ilikuwa na kuongeza uzalishaji na kupanda kimaendeleo kwani ilikuwa maarufu na wateja kufurika kutokana na utendaji kazi wake , uimara na uchapakazi kwa wafanyakazi wake iliyotokana na kiongozi wa juu Mkurugenzi wa kampuni kuwa imara, mwenye busara na hekima,upendo na mwenye kauli nzuri kwa wafanyakazi wake na mameneja na kufanya kuwa na utawala bora na kuwajibika kwa wafanyakazi wote hali iliyopelekea kufanya kazi kwa weledi na kutoa huduma bora kwa wateja hali iliyofanya kampuni hii kukua na kupata maendeleo na kupata soko kubwa.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom