SoC02 Utawala Bora ni uwajibikaji sio Ubepari

SoC02 Utawala Bora ni uwajibikaji sio Ubepari

Stories of Change - 2022 Competition

Chinga94

New Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
2
Reaction score
1
Utawala bora ni utendaji au uongozi wenye kuleta tija na manufaa kwa maendeleo ya nchi na wananchi wake, na kwa uharisia utawala bora hudumisha upendo na uhusiano baina ya serikali na wananchi, pia kwa upande huu viongozi wanapaswa kua shupavu, imara, wa kweri na wawe wenye uwazi.

MISINGI YA UTAWALA BORA
Kama ilivyo kawaida kwa maisha ya wanadamu ili uweze kufikia mafanikio ni lazima ujiwekee malengo na misingi yenye kukufanya utimize ndoto zako vivyo hivyo kuna mambo mhimu ambayo watawala wanapasawa kuzingatia ili waweze kutimiza dhima ya utawala bora wenye haki ukweri na uwazi kwa jamii na kuifanya jamii kuishi ndani ya utawala bora.

1. TASWIRA
Watawala wanapaswa kua na maono, kutizama mbele kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo, na hii dhima itasaidia nchi husika na jamii kwa ujumla kupata maendeleo kwa kiwango kikubwa sana.

Tunahitaji watawala wenye fikra imara ili kuilinda jamii na maono hayo yaanzie kwao binafsi na hapo itatusaidia kua na utawala ulio bora kabisa(ukiona vya elea vimeundwa).

2. UADILIFU
Utawala bora unahitaji utendaji imara wenye nidhamu na kujituma kutunza na kujali amali za taifa au jamii husika, hivyo basi tusiwekee viongozi wasio jitambua ambao badae watakua wezi, wadanganyifu na wabadhirifu wenye kuhujumu mali za umma na badae kugeuka kuwa mizigo kwa taifa.

3. HAMASA
Ili utawala uwe bora ni lazima viongozi wake wawe na ushawishi,mvuto na kauli njema kwa wananchi, huu ni msingi mkubwa saana ambao utamfanya hata kiongozi mwenyewe aone uongozi ni kazi rahisi sana kwa sababu jamii ita mpenda na kumsikiliza kwa kila jambo, utawala utakua na nguvu kubwa ya kuishawishi jamii ili iwe na umoja pia ushirikiano kwa ajili ya kuleta maendeleo ya taifa na mwana nchi mmoja mmoja. Hivyo basi viongozi mjitahidi sana kuwa wenye hamasa na ushawishi kwa wananchi wenu.

4. UTHUBUTU
Utawala bora unahitaji viongozi wenye maamuzi sahihi wasio waoga wenye uthubutu wa kuamua jambo lenye manufa kwa jamii, wenye kujiamini watawala wasio na mawazo hasi na kufikiri kua kuanzia jambo dogo ili kuendea kubwa ni uharifu, utawala unapaswa kusimamia mambo yote iwe kubwa ama dogo kwa haki ukweli na uwazi pasina kupepesa macho hili litaifanya jamii ione kua utawala ni bora hauna ubaguzi wala ubabaishaji.

5.TAARIFA
Ni jambo la aibu na la kushangaza tunapokua na utawala ambao wakati wote ni kuzuia na kuwawekea vikwazo waandishi wa habari na vyombo vingine vinavyo toa taarifa kwa jamii kwa manufaa yao binafsi, utawala ambao unatoa taarifa za kusifu tu pasipo kukosoa. Katika utawala bora hili jambo sio rafiki hata kidogo, utawala bora unahitaji viongozi wepesi wenye uwezo mkubwa pia wa kutafta taarifa na kuziwasilisha kwa umma kwa manufaa chanya.Uwepo uhuru wa vyombo vya habari ili kuleta mambo chanya kwenye jamii na kukemea mambo hasi na tukifanikisha hilo utawala utakua tunu katika jamii.

6.UBUNIFU
Hili ni jambo la mhimu hasa endapo utawala utahitaji kua bora kwa jamii, wawepo viongozi walio na ujuzi wenye kufikilia namna gani wanaweza inusuru nchi na tatizo ama la ajira au kwa maendeleo ya nchi na wananchi wenyewe kqa kutoa ushauri namna gani ya kutatua ama kujenga chanya ya sasa ama ijayo, na baada ya jamii kunufaika na ubunifu au maarifa yake pasina shaka jamii itaishi kwa furaha na amani isiyo kifani.

ZINGATIA: utawala bora hauletwi kwa siasa za uongo na kweli bali kwa ubunifu imara wenye kuijenga nchi.

7. RIDHAA
Utawala bora ni tunu na kila mmoja angependa kuishi kwenye nchi iliyo na utawala ulio bora, lakini ni nani hasa wa kutupatia huo utawala bora pasipo sisi wenyewe wana nchi kuhakikisha tunaweka viongozi madarakani ambao wapo tiari kuitumikia nchi kwa moyo wao na kwa hisia pasipo kulazimishwa na mtu yeyote. Pamoja na viapo wanayo toa bado tunakua na viongozi hawako tiari kujitoa kwa ajili ya nchi yao, viongozi wenye kisusia mambo,viongozi wenye hasira wasio penda kuulizwa, viongozi wanaopenda nchi iwafanyie jambo na sio wao waifanyie jambo.

Tafadhari serikali na jamii tunaiomba kuwepo na mchujo maalumu wenye tija ikiwemo kufuatilia historia ya nyuma kwa anaetaka kua kiingozi na sio siasa siasa tu, na tukifanikiwa hapo tutaishi kwenye utawala bora.

NINI CHA KUFANYA?
Kwa asilimia kubwa zaidi jamii inaitegemea serikali ili kuwepo na maisha bora kutokana na utawala bora, lakini jicho langu linaitizama kwa ukubwa jamii au wanachi kwa sababu serikali ni mimi na wewe, serikali inaundwa na wananchi wenyewe, kutokana na jamii kurubunika na vitu vidogo vidogo yaani rushwa na kuamua kuweka watawala wasio na sifa matokeo yake ni kuishi kwenye utawala usio rafiki wenye manyanyaso na wenye ubaguzi mkubwa usio jali haki za raia.

Na lawama itabaki kupewa serikali wakati makosa yamefanywa na jamii,
Hivyi basi cha kufanya naiomba jamii au wana nchi wawe msitari wa mbele kupinga hili jambo kwa kukemea rushwa na kuchagua viongozi wenye uthubutu, taswira, ubunifu na wenye uwezo wa kuipatia jamii utawala bora kwa kuzingatia haki na wajibu.

ZINGATIO: Utawala bora ni UAJIBIKAJI na sio UBEPARI.

IPENDE NCHI YAKO, IJALI NCHI YAKO, NA UILINDE NCHI YAKO
by chinga mnyonge...
 
Upvote 1
Back
Top Bottom