SoC02 Utawala Bora

Stories of Change - 2022 Competition

alpine65

New Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Utawala bora ni matumizi ya mamlaka ambayo yanakuwa na uwazi, uwajibikaji, ushirikishaji wa watu, ufanisi, tija, uadilifu, usawa na unafuata utawala wa sheria. Tanzania ikiwa moja kati ya miongoni mwanchi zenye kuzingatia demokrasia na utawala bora, ilifanikiwa kuanzisha tume ya haki za binadamu na utawala bora mnamo Julai 1, 2001.

Vilevile serikali ya Tanzania kwa kutambua umuhimu wa utawala bora nchini, imeweza kuanzisha wizara ya utumishi na utawala bora) ambayo kwa sasa inaongozwa na Mhe. Jenista Joackim Mhagama. Ili kutekeleza dhana ya utawala bora, kuna mambo kadha wa kadha ambayo ni lazima yazingatiwe na taifa lolote lile, mambo hayo ni pamoja na:
  • Moja, matumizi sahihi ya dola
  • Pili, matumizi mazuri ya rasilimali za taifa kwa faida ya wananchi
  • Tatu, matumizi mazuri ya madaraka yao
  • Nne, kuyajua na kutambua madaraka waliyonayo viongozi na matumizi yake yenye tija kwa taifa na wananchi wote na mwisho ni vipi madaraka hayo yanatumika kulingana na mipaka iliyowekwa na katiba na sheria.

Utawala bora ni dhana yenye misingi mbalimbali kama ifuatavyo

Uwazi,
hii ni hali ya kuendesha shughuli za umma bila uwepo wa usiri na kificho, hii husaidia wananchi wawe na uwezo wa kupima utendaji na uzingatiaji wa kanuni, taratibu na sheria katika mambo mbalimbali yanayotokea ndani ya nchi kama vile wananchi kupewa taarifa za mapato na matumizi,kujulishwa mahali na wakati muafaka wa kupata taarifa wanazohitaji na wazipate bila usumbufu wowote

Uwajibikaji, i hali ya kiongozi na mtendaji kuwa tayari kujibu, kubeba dhamana na kutoa maelezo kwa wananchi juu ya maamuzi au matendo aliyoyafanya katika kutekeleza dhamana aliyopewa na wananchi ili awatumikie na kuleta maendeleo

Usawa, hali ya kuwapatia wananchi wote fursa sawa katika kushiriki kwenye mambo yanayohusu jamii yao
Hiyo ni baadhi tu ya misingi ya utawala bora. Zipo pia nguzo mbalimbali za utawala bora ambazo serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora hutumia nguzo husimamia utawala bora kwa maslahi ya watanzania na taifa kwa ujumla, nguzo hizo ni kama ifuatavyo

Uhuru wa habari na uhuru wa vyombo vya habari
Uhuru wa habari una maana ya watu kuweza kuzungumza na kupashana habari na kuwa na haki ya kupata habari kutoka katika vyombo vya umma na hata binafsi ambavyo vinatekeleza wajibu wa umma.

Hili lazima liende sawia na kuwa na vyombo vya habari vilivyo huru, kwa maana ya kuwa na uwezo wa kutafuta na kuandika habari na kuzisambaza kwa watu ndani na nje ya mipaka ya nchi bila ya kuingiliwa na bila ya sababu maalum na Serikali. Lengo ni kuwawezesha wananchi kufahamu namna viongozi wanavyoendesha nchi na hatimaye kujadili na kutoa maamuzi juu ya rasilimali za nchi yao. Nchini Tanzania idadi ya vyombo vya habari vya mitandaoni ni Idadi ya Vyombo vya Habari vya Mtandaoni ni kama ifuatavyo:

1. Simulcasting Redio- 26
2. Online Radio- 6
3. Simulcasting Television- 6
4. Online Television- 91
5. Online Blog- 63
6. WeBlogs- 30
7. Online forums- 2
Hii huonesha kwa uwazi juu ya uwepo wa uhuru wa habari pamoja na vyombo vya habari nchini

Uhuru wa Mahakama
Uhuru wa Mahakama unamaanisha kuwa kila jaji au hakimu yuko huru kuamua kesi iliyopo mbele yake kwa mujibu wa sheria na ushahidi ulioletwa mbele yake, na katika kutekeleza majukumu hayo, hapaswi kuingiliwa, kushawishiwa, au kushinikizwa na mtu au chombo chochote, ikiwemo Bunge na Serikali kama inavyoelezwa katika Ibara ya 107B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Hivyo, dhana ya uhuru wa mahakama inaitaka mahakama kutekeleza majukumu yake bila woga wala upendeleo.

Ulinzi, Ukuzaji na Uzingatiaji wa Haki za Binadamu
Utawala bora ni ule unaolenga kuboresha na kujali maisha ya watu. Njia ya msingi ya kujali maisha ya watu ni kulinda, kukuza na kuzingatia haki za binadamu. Utawala bora unataka kuwe na mfumo wa kisheria, kiutawala na utashi wa kisiasa unaolinda, kukuza na kuzingatia haki za binadamu.

Mgawanyo wa Madaraka
Nchini Tanzania dhana ya mgawanyo wa madaraka inaeleza kuwa utawala wa dola unapaswa kugawanywa katika vyombo vitatu ambavyo ni Serikali, Bunge na Mahakama. Kila chombo kina majukumu tofauti na chombo kingine, vilevile vyombo hivyo vitatu hushirikiana kwa lengo kuu la kuhakikisha viongozi na wananchi wanafata sheria na kanuni mbalimbali katika Nyanja za kiuchumi na kijamii.

Katiba ya Kidemokrasia
huu ni waraka wa kisiasa na kisheria wenye muafaka wa kitaifa juu ya namna ya kuendesha masuala ya nchi. Demokrasia ni mfumo wa kisiasa wa kuchagua na kubadilisha serikali kwa njia ya uchaguzi ulio huru na wa haki. Ni Ushirikishwaji wa kweli wa wananchi katika maisha ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hivyo, Katiba ya Kidemokrasia ni ile ambayo kuandikwa kwake kumetokana na ridhaa na mwafaka wa wananchi.

Zifuatazo ni faida za utawala bora nchini
  1. Kuheshimiwa kwa haki za binadamu
  2. Utatuzi wa migogoro kwa mujibu wa sheria na taratibu
  3. Kuleta ustawi wa wananchi
  4. Matumizi mazuri ya rasilimali za nchi
  5. Maendeleo endelevu
  6. Kupungua kwa umasikini, ujinga na maradhi
  7. Kutokomea kwa rushwa
  8. Huduma bora za jamii

References
SHERIA, W. Y. K. N. (2009). JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Assey, P., Bass, S., Cheche, B., Howlett, D., Jambiya, G., Kikula, I., ... & Rutasitara, L. Mazingira ni Kitovu Cha Maendeleo Tanzania. IIED.
Tungu, M., Sirili, N., Frumence, G., Kagaigai, A., Anaeli, A., Mwangu, M. A., & Kiwara, A. D. (2022). Health care prioritization process for the elderly in rural Tanzania under decentralized system: prospects and challenges.
 
Upvote 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…