SoC03 Utawala imara na utendaji

SoC03 Utawala imara na utendaji

Stories of Change - 2023 Competition

ANSIKARO JOHN

New Member
Joined
May 31, 2023
Posts
1
Reaction score
2
Utawala bora na uwajibikaji, ni usimamizi sahihi unaozingatia sheria na haki kwa usawa kati ya viongozi na raia, ili kuondoa uvunjifu wa haki za watu na matumizi mabaya ya mali za uma, mfano rushwa.

Utawala bora na uwajibikaji huchochea maendeleo katika taifa lolote, uwajibikaji hutokana na viongozi walio bora, siasa huru na sheria imara. Sheria imara hulinda rasilimali na hulinda haki za watu kwa usawa, hii huchochea haki na utawala bora.

Uwajibikaji huleta uimara kwenye usimamizi wa rasilimali, usimamizi sahihi wa rasilimali huchochea ukuaji wa uchumi kati ya watu na taifa kwa ujumla, hivyo ikiwa uwajibikaji ni dhaifu pia maendeleo huwa ni finyu katika taifa lolote.

Utawala bora huzingatia uwazi, uwajibikaji, mgawanyo wa madaraka, usawa, uhuru wa kujieleza na maridhiano, mfano maridhiano kati ya rais Samia suluh hassan na vyama vya upinzani nchini Tanzania.

Nchini Tanzania madaraka yamegawanyika katika mihimili Mitatu, bunge, mahakama na serikali. Ni kithibitisho cha utawala bora katika taifa, mahakama hulinda haki za watu, bunge hutunga sheria na serikali husimamia watu pamoja na rasilimali kwa usawa.

Utawala bora na uwajibikaji huchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo katika taifa, mfano Marekani. Rushwa huondoa maendeleo na haki msingi za watu, hivyo uwajibikaji huondoa rushwa na kuleta maendeleo katika taifa lolote.

Faida za utawala bora na uwajibikaji, hupunguza umasikini katika taifa, huchochea maendeleo endelevu,huleta amani na upendo kati ya watu katika taifa,huondoa uvunjifu wa haki za binadamu na matumizi sahihi ya dola au mmlaka.

Kwa mujibu wa ibara ya 8(1) (c) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,1977 Serikali (viongozi na watendaji) itawajibika kwa wananchi. Misingi ya utawala bora niuwazi,ushirikishwaji,usawa,utawala wa sheria na maridhiano.

Uwajibikaji hukidhi matarajio na uhitaji wa raia katika kutatua kero na matatizo yanayo wakabili , kutoa huduma kwa haraka na kwa kiwango bora kwa mujibu wa sheria na haki za watu.

Uwajibikaji hujenga uaminifu kati ya raia na viongozi wao, utawala bora hulindwa kwa sheria, hivyo hairuhusiwi kwa mhimili mmoja kuingilia mhimili mwingine katika kufanya kazi zake kama ilivyoelekezwa kikatiba, kwakua kila mhimili hufuata katiba katika kutimiza majukumu yake kikamifu bila dosari yeyote.

Nchi nyingi za afrika huvunja utawala bora na kuanzisha utawala wa mabavu kwa maslahi binafsi ya viongozi, mfano somalia, congo, burundi, nigeria, uganda and sudan. Hali hii huleta machafuko, umasikini, njaa, uvunjifu wa haki za raia, ukosefu wa huduma muhimu za kibinadamu,mauaji na uharibifu wa mali na mazingira.

Demokrasia na utawala wa sheria huletwa kwa katiba bora bila kulinda dola au mamlaka husika kwa ujumla, pia wananchi lazima washirikishwe katika maamuzi ya ujenzi wa taifa lao.

Serikali kuu inatakiwa kuimarisha serikali za mitaa na taasisi zote zinazolinda na kutetea haki za watu na kuchochea uwajibikaji katika mitaa kwa ujumla, ushirikishwaji wa wananchi wa ngazi za chini ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha kunakuwa na maendeleo katika jamii na kuhamasisha utawala bora na uwajibikaji katika jamiii.

Viongozi lazima wazingatie mambo yafuatayo ili hahakikisha kunakuwa na utawala bora na uwajibikaji,viongozi lazima wajue mipaka yao ya madaraka, matumizi sahihi ya madaraka na matumizi sahihi ya dola.

Changamoto za utawala bora na kutokuwa na uwajibikaji, rushwa,wizi na uvunjifu wa haki za watu hutokea kwa gafla katika taifa.

Utawala bora hubeba nyenzo bili muhimu, utawala na mtawala. Mtawala ni mtu na utawala ni mamlaka anayakuwa nayo mtu katika kufanya maaamuzi ya kidola, hivyo uwajibikaji hutokana na mamlaka ya mtawala kutumika vizuri katika kutoa mamlaka kwa watu anaiwasimamia.

Katika nchi nyinyi za dunia ya tatu hakuna utawala bora na uwajibikaji, rushwa na matatizo mengi ya raia hayatatuliki kwa muda sahihi, hivyo maendeleo yamekuwa magumu kupatikana kwakua hakuna uwajibikaji unaihitajika katika kulijenga taifa, mfano Kenya na Tanzania rushwa imeshamiri kwa ukubwa wa hali ya juu, jambo hili limepelekea kukwamisha maendeleo ya watu na taifa kwa ujumla.

Maisha ya kila siku hutegemea utawala bora na uwajibikaji ili kuwa imara, hivyo kama hakuna uwajibikati hata maisha hugeuka kuwa magumu, ikiwa utawala ni sio bora pia huchochea maisha kuwa magumu na hatarishi kwa kila namna, hivyo ni bora zaidi kuheshimu haki na misingi bora kwa kila mtu na kila mtu anapaswa kuheshimu mamlaka na sheria zote ili kulinda heshima ya mamla husika.

Kwa kumalizia, utawala bora na uwajibikaji hubomolewa na siasa mbovu, siasa za matusi na ukosekanaji wa sheria imara za kudhibiti wala rushwa, viongozi wazembe na taasisi kivuli, hivyo serikali inatakiwa kuweka sheria imara na kuongeza ufanisi katika ufuatiliaji wa mipango yake na hakikisha inasimamia imara katika mipango yako na haki za raia na mali zao.
 

Attachments

  • D2B4071C-0BC6-4951-9C9F-C01A95539D6E.jpeg
    D2B4071C-0BC6-4951-9C9F-C01A95539D6E.jpeg
    107.7 KB · Views: 4
  • 8EFBA2EA-D590-4611-868D-FAAB1AAA6080.jpeg
    8EFBA2EA-D590-4611-868D-FAAB1AAA6080.jpeg
    51.7 KB · Views: 3
  • F48BCF82-278D-4A44-9A2D-BFA964C8C85D.jpeg
    F48BCF82-278D-4A44-9A2D-BFA964C8C85D.jpeg
    30.1 KB · Views: 3
  • 466C5B11-F7AC-4779-A2C7-3B2D2C98D815.jpeg
    466C5B11-F7AC-4779-A2C7-3B2D2C98D815.jpeg
    48.4 KB · Views: 4
  • 51E9AD8E-9EE9-4164-8141-B8DF6484488B.jpeg
    51E9AD8E-9EE9-4164-8141-B8DF6484488B.jpeg
    40.5 KB · Views: 3
Upvote 3
Back
Top Bottom