Utawala wa ccm umetutenda vya kutosha, sasa tuseme basi

Utawala wa ccm umetutenda vya kutosha, sasa tuseme basi

babatovu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
2,739
Reaction score
1,602
Wamejivika ufalme mabegani mwao, wameifanya hii nchi kuwa ni pango la wanyang'anyi toka nje na ndani ya nchi.
Wamekua wakiingia mikataba mibovu na yenye kudhalilisha walio wengi kwa manufaa yao na vizazi vyao.
Umasikini na ujinga wetu uliosababishwa na watala hawa dhalimu, ndio imekua silaha yao kubwa ya kutuangamiza sisi na vizazi vyetu na kuwastawisha wao na vizazi vyao. It's a time now, let's stand up for our own rights until there will be no longer first class and second class citizen in our nation.
Wanaringia vyombo vya ulinzi kwa sababu vinapokea amri na maagizo toka kwao. Wamesahahu sisi ndio tuliowaweka hapo walipo sasa, lakini wametumia umasikini wetu na ujinga wetu kutudhalilisha.
Shime watanzania, tuamkeni sasa kwa umoja wetu na kwa nguvu zetu tuseme sasa basi. Mustakabali wa maisha yetu ya sasa na yabaadae opo mikononi mwetu.
 
Back
Top Bottom