Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
Chadema inahubiri kuwa endapo watashika dola (ndoto ya kawaida) basi wataanzisha utawala wa kimajimbo Ili kurahisisha huduma za kijamii na kuharakisha maendeleo. Ukiitazama mfumo huu na jinsi wanavyouelezea kwa haraka unaweza kudhani ni kweli.
Kama kuna jambo ambalo ukitaka ugomvi na Watanzania na uachwe kwenye mataa na uchukiwe kama ukoma au saratani basi njoo na sera yoyote ya kibaguzi iwe ni udini, rangi, ukabila, ukanda, jinsia nakadhalika.
Moja ya tunu adhimu wanayoienzi Watanzania ni Umoja wao, udugu wao, ushirikiano wao, ushirika wao. Hakuna zuri ndani utawala wa Majimbo zaidi ya kutugawa watu wa nchi moja. Utawala wa majimbo utafanya kuwepo na tofauti kubwa sana ya ulaji wa keki Taifa ndani ya kapu moja.
Sera hii inataka kila Jimbo lijikusanyie mapato yake binafsi na kutumia itakavyo na Salio (kiduchu) kupelekwa Serikali Kuu. Hii maana yake ni kwamba baadhi ya maeneo watakufa masikini na ushahidi tunaona katika ukusanyaji mapato Katiba baadhi ya H/Mashauri. Bila fedha kushushwa Toka kapu la Taifa hawawezi kujiendesha.
Vita na migogoro isiyoisha DRC ni matokeo ya mfumo huu. Ndani ya nchi moja lakini kutoka Jimbo moja kwenda linguine unakutana na "Beria" na unalipia Dola mia mfano utoke Arusha kwenda Tanga. Hii ndio sababu Tshekedi hawezi kuitawala Kongo maana hakuna Jeshi la nchi Bali majeshi ya majimbo. Huo ni mfano mmoja.
Watetezi wa hoja hii utolea mfano Marekani na Ujerumani lakini wanasahau umri wa nchi hizi katika utawala na demokrasia. Nchi changa kama hizi za Afrika zenye kujitawala chini ya miaka 60 bado zinatakiwa kukaa pamoja si kutengana.
Jambo la maana ni kuweka mfumo mzuri wa kuwafikia kila raia katika kupata huduma za lazima: kula, kuvaa na kulala.
Ni kutokomeza rushwa, ufisadi, upigaji, uhuni wa kimkakati nakadhalika. Raia kutendewa haki sawa kwa kila jambo. Lakini hakuna ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kuwa utawala wa Majimbo ndio suluhisho la matatizo yetu. Tuwapinge, tuwakatae wanaotaka kututumbukiza kwenye vita ya kugombania rasilimali zetu. Tuwanunie.
#BringBackOurMoneyCAG