Kwa Mimi binafsi utawala wa kimajimbo ni mzuri ila usiwe na full mandatory kama nchi za wenzetu (yaani usiwe na Uhuru wa kila kitu kwenye maamuzi na kila kitu )
FAIDA ZA MAJIMBO (ninazozijua kwa mtazamo binafsi)
1) kiongozi katika jimbo huchaguliwa na wananchi wa jimbo husika hivo kama jimbo likipata kiongozi sahii nirahisi kupata maendeleo kwakua atapatikana MTU wa eneo husika anaejua changamoto na jografia ya eneo
2) kurahisisha maendeleo na ukuwaji wa jimbo haraka kwakuwa nirahisi kuanzisha miradi na kuitekeleza bila kupangiwa na uongozi moja kwa moja
3) kutoa fursa nying za ajira katika jimbo husika kwa wananchi wake kwakuwa kila idara inakuwa chini ya jimbo hivo kutoa urasimu kwenye mchakato waajira kujazana watu wa waeneo tofauti na jimbo husika
3) ukuwaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi na jimbo kwa pamoja kama kutakuwa na uongozi sahihi wakutekeleza majukumu yake kwakua maamuzi yenu yote hufanyika bila kupangiwa na uongozi tofauti na jimbo