Utawala wa sheria wa kimataifa

Utawala wa sheria wa kimataifa

africa6666

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2008
Posts
281
Reaction score
53
Wana JF,
Binafsi kuna hili suala linanitatiza sana,

Utawala wa kisheria wa kimataifa (International Law of Governance), nini lange lake kuu?

je,

  • inalenga kuwadhalilisha vingozi wa afrika tuu?
    inalenga kuweka misingi imara kwa utawala na watawala?
    inalenga kulinda na kusimamia haki za binadamu?
    inalenga kuzuia ufisadi katika nchi zinazo endelea?
    inasimamia njia kuu na bora za kufikia malengo ya milenia (international globalization)?
  • so on so forth....

naomba tujadili wakuu.
 
Utawala wa sheria unaanza kwanza nyumbani


HAPA Tanzania wa ndani tumeushindwa akija wa nje na lwake tutamfuata vivyo hivyo.

Lakini bwana mmoja ambaye ninamuita mwanafalsafa alishwahi kuniambia kwamba 'as long as the Tanzania government cannot manage road traffic and daladala it will never be able to manage the country properly!#

Alikuwa na maana kwamba kwa kuwa:
. magari mabovu ya abiria au daladala ni tele barabarani
. kwa kuwa madereva na makonda wanavaa matambara badala ya unifomu.
. kwa kuwa dereva wa daladala anaweza akapita popote.
. kwa kuwa askari wa usalama barabarani ni magwiji wa rushwa ndogo ndogo na wanaharibu ratiba za wananchi wengine kwa kamatakamata yao isyo na mpango wala nidhamu
. kwa kuwa lugha ya makonda ni chafu na wanachokijua ni pesa tu na sio uungwana,
. kwa kuwa wenzetu Kenya na Uganda wanakaa 'levo siti' na kujifunga mkanda na sisi huko magari yanajaza hadi pomoni,
. kwa kuwa hakuna anayejali mtembea kwa miguu au mwendesha baiskeli na jamaa hawa wanauawa ovyo,
. kwa kuwa hakuna anayejali watoto, wazee au walemavu wanaokuwepo mabarabarani nyakati mbalimbali na hivyo salama yao sio kuachia usalama barabarani bali Muumba,
. kwa kuwa usalama wa barabarani ni 'ufidiaji pengo la mishahara duni na tamaa za utajiri wa haraka na sio usalama wa wananchi,
. kwa kuwa wenye magari ndio mabwana na watembea kwa miguu watwana,
. kwa kuwa magari yote hayaheshimu 'zebra crossing' na waendao kwa miguu, ikiwa ni pamoja na yale yalinonunuliwa kwa pesa ya walipa kodi
. kwa kuwa serikali yetu inaabudu magari ya kifahari ambayo mengine yanafanya kazi za 'uboi' za wakubwa wakati wachangiaji muhimu wa maendeleo ya nchi hawana usafiri wa kuaminika,
. kwa kuwa viongozi watawala hawana shida ya usafiri ila ni walalahoi na wapiga kura wao ambao wamezoea hili,
. na kwa kuwa wabunge wanaona ni muhimu kuzungumzia maslahi yao lakini sio suala la wananchi kuwa na usafiri wa salama, wenye heshima, staha na utu

........hatuwezi kuwa na utawala wa sheria hapa nchini na kwa hiyo tusishangae tukiburutwa na watu wa nje kwa kuwa sisi wenyewe tumeshindwa kujenga ustaarabu na umakini katika maongozi ya nchi zetu.

Mdharau kwao mtumwa, na mdharau wa kwao akaabudu wazungu tutamwitaje???
 
Back
Top Bottom