Utawala wa Zanzibar uliopita ulikithiri ufisadi hadi hauonekani

Utawala wa Zanzibar uliopita ulikithiri ufisadi hadi hauonekani

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Kwa jinsi Husein Mwinyi anavyoshindwa kuvumilia juu ya vitendo vilivyofanywa na watawala, sikusudii watawala wa kiarabu, nawakusudia hawa tuliopigania uhuru pamoja na kuahidi kuleta maendeleo.

Rais Hussein kila anapopagusa patupu, watawala wa waliopita wakiongozwa na CCM wameshakwapua. Yaani wameishachukua chao mapema, ugumu ni kauli aliyopenda kuitumia kuwa hatafukuwa makaburi, ila kwa hali ilivyoachwa uzalendo utamshinda na inaonesha ataenda kuyafukua makaburi ili apate angalau cha kuanzia mradi wa Zanzibar mpya. Yajayo yanafurahisha,

Utawala wa Zanzibar wa CCM umekomba kila kitu sijui walifikiria ndio mwisho wa dunia au ndio mwisho wa Muungano. Huseini anaenda kufungua makasha anakuta kweupe.

CCM ni kama nzige lile kundi la Zanzibar limefisidi kila kitu. Tunasubiri chunguzi kedekede zinazokuja ili kuitafuta hazina ya Zanzibar wapi imezikwa.

Je, Mwinyi ataweza kumfunga Nzige wakubwa kengele na sheria na haki ichukue mkondo wake?
 
Dk shein alikuwa mpole sana wacha Mwinyi awanyooshe
 
Dk shein alikuwa mpole sana wacha mwinyi awanyooshe

Wanafanana wote, na atakapotaka kuchukua hatua hao atakaotaka kuwachukulia hatua atakuta wote ndio waliomsaidia kwenye wizi wa kura ili awe rais. Kama yeye yuko madarakani kwa wizi wa kura, atamuwajibisha mwizi gani wakati yeye mwenyewe ni zao la wizi? Tusubiri siku jiwe naye anatoka madarakani jinsi wizi wa yeye na genge lake utakavyowekwa hadharani.
 
Mkuu tindo unadhani jiwe ataondoka hapo leo ama kesho? Maweeee!
 
Ccm ni ile ile, hapo Husseni Mwinyi anabadilisha tu chupa (watendaji) ila mvinyo (CCM) ni ule ule.

Rais ajae pia atafanya hivyo hivyo yaani kubadilisha chupa huku mvinyo ni ule ule.
 
Mbowe alikuwa mkali alishinda nini hapo ufipa na jengo la kupanga na mbunge mmoja.poor you
Wanafanana wote, na atakapotaka kuchukua hatua hao atakaotaka kuwachukulia hatua atakuta wote ndio waliomsaidia kwenye wizi wa kura ili awe rais. Kama yeye yuko madarakani kwa wizi wa kura, atamuwajibisha mwizi gani wakati yeye mwenyewe ni zao la wizi? Tusubiri siku jiwe naye anatoka madarakani jinsi wizi wa yeye na genge lake utakavyowekwa hadharani.
 
Wananchi wenyewe wazanzibar idadi yao wapo 1.6milioni ,yaani ni sawa na kijiji,
Lakini kila siku shida na matatizo hayaishi.
 
Siasa za ccm kila anayekuja anakuwa na mkwara wake wa kutofukua mizoga na mifupa, hii ni njia ya kuaminishq umma kuwa hiki kilichoingia ni chuma cha pua ila subiri kidogo.

Mfano ni hapo hapo kwako angalia yanayoendelea nyuma ya pazia.
 
Kila awamu kuna WANACCM wanaokula na wanaowatazama wengine wakila.

Alipoingia Benja, mikwara ilikuwa kama yote kwa utawala wa Alhaji.

Hali kadhalika huko visiwani, kwa sasa mtoto wa alhaji anaonyesha kama kuna uovu hivi ila naye Akimaliza atakayekuja naye atafanya hivyo hivyo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Yaani kuongoza nchi ya watu takriban 2M afu ukakuta watu maskini wewe mtawala lazima ujitathmini - hata ukiamua kuwaweka kwenye clusters (wavuvi, kilimo, ufugaji, michezo, utalii nk) inawezekana sababu ya uchache wao

Hope Dkt Hussein Mwinyi atakuwa na jambo muhimu kwa awamu yake
 
Back
Top Bottom