Utayari kisaikolojia na kimwili kabla ya kujihusisha na ngono ni muhimu

WLF Tanzania

Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
38
Reaction score
22
Habari wakuu,

Kama tunavyofahamu, kila jambo na wakati wake.

Tupo katika karne ya 21 ambapo vijana hujiingiza katika ngono wakiwa wadogo, wengi wao kabla ya miaka 18. kufanya hivi kuna hatari zake. Pamoja na kupata madhara kisaikolojia, hasa mahusiano yakivunjika na kutengwa na jamii (hasa kwa wasichana), kuna athari za kimwili kama kupata matatizo ya uzazi.

Ni vizuri kuepuka yanayoepukika. Kaa salama. Kama uko tayari kuanza mambo haya, jilinde kwa vyote uwezavyo.

Utashangazwa na jinsi utakavyoweza kufurahia maisha ukifanya mambo katika wakati muafaka.


Mna maoni gani wadau?

Karibuni
 
umemaliza au bado kuna vitu unavitafakari utakuja kujazia?nilitegemea hasa kukuta hayo maandalizi ya kisaikolojia
 
umemaliza au bado kuna vitu unavitafakari utakuja kujazia?nilitegemea hasa kukuta hayo maandalizi ya kisaikolojia

Maandalizi kisaikolojia yanawahusu wale wanaokwenda kufanya tendo la ndoa. Iwe ni mipango ya muda mrefu au mfupi. Kabla ya kufanya ngono na mtu yeyote kuna maswali ya kujiuliza na vitu vya kuweka akilini. Mfano, nini kitatokea baada ya tendo hili? Nikipata mimba (au mwanaume ajiulize msichana akipata mimba) itakuaje? Niko tayari kuwa baba/ mama? Nikipata magojwa ya zinaa ntayatibu vipi? Kama mtu ninayefanya naye tendo hili hana hisia za kudumu kwangu itakuwaje? Nikipata mimba familia/ jamii itakuwa upande wangu?

Majibu ya maswali haya yanapatikana katika hali ya utulivu na ukimya, yanahitaji muda mrefu kufikiri na mwishowe majibu yakipatikana, ndipo mtu anaweza kujipima na kuona kama yupo tayari kujiingiza katika ngono. Mara nyingi ni vizuri kushauriana na wazazi au wataalamu wa afya kabla ya kuamua mwenyewe.

Pale unapoona kuwa upo tayari na utaweza kukabiliana na mambo yatakayojitokeza baada ya tendo hilo kwa ushupavu, hapo tu ndipo unapoweza kuendelea na kufurahia tendo hilo.

Cha kuikitisha ni kwamba vijana wengi, hasa wadogo (wenye umri wa miaka 16- 21) hufanya ngono bila kuwa na muda wa kutosha kujipima na kuangalia kama wapo tayari. Matokeo yake ni hasi kama vile mimba, magonjwa ya zinaa, kutibuliwa akili kwa sababu ya kuachwa na wenzao n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…