Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Nadhani wengi tumekutana na tulio lililotrend jana, video ya inayomuonesha 'Bonge' akipambana na watu waliokuja kumteka na kufanikiwa kuwazidi nguvu, wakimuachia zawadi ya pingu. Kama mpaka sasa hujakutana na tukio hilo basi pitia hapa.
Kutokana na taarifa ya polisi, Bonge ni mfanyabiashara na alikuwa kwenye hoteli hiyo Kilivya kwaajili ya mambo ya kibiashara, kama hujakutana na tamko la polisi pia fanya kuzama hapa.
Kama tunakumbuka vizuri tukio kutekwa kwa Mkurugenzi wa Dar24, naye taarifa yake haikuwa mbali sana kwenye kuhusisha wafanyabiashara. Na yeye alienda mbali kabisa kusema kuwa watu hao anawafahamu wamekuwa wakiwasiliana kwaajili ya mambo ya biashara, na huenda labda walitaka password na siri nyingine za kibiashara. Ingia hapa kujikumbusha kilichosemwa kwa undani.
Je, hii yote ni mpango wa kuhalalisha kuwa watu wanajiteka, kifo cha Kibao huenda ni mambo ya kibiashara, akina Soka, Shedrack na wengine ambao hawajulikani walipo mpaka sasa, kwamba hakuna mkono wa polisi wanaotuhumiwa kila leo kuhusika na matukio haya?
Waliyomteka Mkurugenzi wa Dar24 wanajulikana, mhanga aliwatambua kwakuwa wamekuwa wakiwasiliana, kwanini hatujasikia kukwamatwa kwao mpaka sasa? Polisi wanasubiri nini? Kwa mwenezi wa BAWACHA uchunguzi wake nae umefikia wapi?
Sativa alihojiwa na kusema kila kilichotokea na alienda mbali zaidi mpaka kumtambua moja ya watu waliomteka, lakini mpaka sasa hakuna yoyote aliyeshikwa au kuhojiwa kutokana na tuhuma hizo za kuhusishwa na utekaji wake, zikaanza danadana za kumhusisha na masuala ya wivu wa mapenzi ila haikufika mbali toka muda huo ni jiii, uchunguzi wa Kibao nao kimya!
Ni mwendo wa kuzuga mpaka tusahau mwisho wa siku matukio yote yawe kawaida na kuhusishwa ama na uhasama wa biashara au ukatili wa mapenzi tuushi hivi hivi kama nyumbu, watu wawe wanapotea na uchunguzi kufa jujuu bila watu kuchukuliwa hatua sababu watekaji halisi actually wanajulikana?
Narudisha mpira kwenu Wakuu, chawa nawasubiri mkija mkiwa mnabubujikwa machozi ya huzuni mkiongozwa na Lucas Mwashambwa Tlaatlaah johnthebaptist

, kujipambania muhimu, usichukuliwe kizembe