Utangulizi
Katika miaka ya hivi karibuni uhalifu wa kimtandao umekuwa tishio kubwa sana kwa wafanyabiashara, makampuni na mataifa mengi duniani.Tanzania kama nchi zingine imekumbwa na tishio hili la kidunia. Mamlaka ya kudhibiti mawasiliano TCRA inafanya kazi kubwa kupambana na janga hili na kuhakikisha usalama wa kimtandao ni wa kuaminika kwa kiasi fulani ingawa sio kwa ufanisi mkubwa kwani bado uhalifu wa kimtandao unaendelea nchini. Hivyo basi, TCRA kama kama chombo mahususi kwa ajili ya kulinda watumiaji wa mtandao inawajibu wa kutumia njia madhubuti itakayosaidia kuondoa tishio hili la uhalifu wa mtandao.
Moja ya mikakati hiyo ni kutumia mfumo wa intelijensia bandia kwa usalama wa kuaminika zaidi mtandaoni.Andiko hili linalenga kuishauri TCRA namna ya kudhibiti uhalifu wa kimtandao kwa kutumia Intelijensia bandia. Andiko hili linajumuisha mkakati na uchambuzi wa kina kuhusu uhalifu mtandaoni ambapo mkakati huo utaweza kuileta Tanzania tuitakayo ndani ya miaka 5 hadi 25.
Umuhimu wa Usalama mtandaoni
Tanzania imeshuhudia ongezeko kubwa la watumiaji wa intaneti kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na mapinduzi makubwa ya sayansi na tekinolojia. Wakati ambapo mageuzi haya yameleta faida nyingi kama kurahisisha ufanisi wa kazi viwandani, serikalini na maeneo mengine,hata hivyo, mageuzi haya yamekuja na matokeo hasi yanayohatarisha usalama wa raia na mali zao.
Uhalifu wa kimtandao kama udukuzi wa taarifa binafsi za mtu,mfano akaunti za pesa bila ruhusa ya mhusika, programu hasidi, programu za kudai fidia na wizi wa utambulisho unaongezeka kwa kasi kufikia kuwa tishio kwa makampuni, jamii na serikali yote.
Katika kizazi hiki cha kidijitali, ulinzi wa taarifa muhimu za mtu si wa kupuuzwa hata kidogo. Taarifa muhimu kama za kifedha na siri za srikali ni muhimu zikawa na ulinzi na usalama wa uhakika. Hivyo basi, TCRA inawajibu wa kuchukua tahadhari mapema ili kulinda miundombinu ya kidijitali nchini na kuwalinda wananchi dhidi ya uhalifu wa kimtandao.
Wajibu wa Intelijensia bandia katika kuzuia uhalifu wa kimtandao
Tangu kugunduliwa kwa mfumo huu wa Intelijensia bandia, imekuwa ni moja ya njia bora kabisa za kuhakikisha ulinzi wa kimtandao.Mfumo huu unauwezo wa kuchambua taarifa nyingi kwa haraka zaidi na kwa ufanisi mkubwa, ambapo inasaidia kutabiri na kuzuia uwezekano wa uhalifu wa kimtandao hata kabla haujatokea na kuleta madhara. Kwa kutumia algorithm za mashine za kujifunzia na uchambuzi wa hali ya juu, mfumo huu unaweza kuimarisha usalama zaidi wa kimtandao.
Pia mfumo wa intelijensia bandia unauwezo wa kufuatilia trafiki za kimtandao, kutambua shughuli zenye shaka ndani yake, na kutoa mwongozo sahihi wa kiusalama mtandaoni. Aidha,mfumo huu unaweza kutumika katika kazi za kila siku kama vile usimamizi wa kazi na kutathimini udhaifu uliopo katika kazi, hivyo, itaisaidia TCRA kutatua vikwazo na matatizo ya kiusalama ambayo kibinadamu ni magumu sana.
Namna ya kutekeleza mfumo wa intelijensia bandia kwa usalama wa kimtandao
Ili kupambana na kuzuia kabisa tishio la usalama wa kimtandao TCRA haina budi kutumia Intelijensia bandia kuwalinda watumiaji wa mtandao. Zifuatazo ni hatua muhimu za kufuatwa na TCRA ili kutekeleza utumiaji wa Intelijensia bandia.
Ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa
TCRA ni lazima ikusanye na ichambue taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kama vile logi za intaneti na tahadhari za kiulinzi. Kwa kuweka taarifa hizo katika algorithm za intelijensia bandia, TCRA itaweza kutambua viashiria vya hatari za kimtandao, na pia kutambua mwenendo wa hali ya kiusalama mtandaoni. Hii itasaidia hata vyombo vya usalama kama polisi kufuatilia hatari zinazoweza kujitokeza mtandaoni.
Ugunduzi na majibu ya tishio
Mfumo huu wa intelijensia bandia unaweza kutumika kugundua na kutoa majibu sahihi ya tushio la uhalifu wa kimtandao kwa ufanisi mkubwa na ndani ya muda mchache. Kwa kuendelea kufuatilia trafiki za mtandao na tabia za watumiaji,mfumo huu wa intelijensia bandia unaweza kutabiri uwezekano wa uhalifu wa kimtandao, hivyo tahadhari kuchukuliwa mapema hata kabla ya hatari kutokea. Aidha, ikiwa tishio la kihalifu la kimtandao limegundulika, intelijensia hii bandia inauwezo wa kumzuia mhalifu asiendelee kuleta madhara zaidi wa watumiaji wengine wasio na hatia, hivyo, kumlinda mtumiaji asiyemhalifu.
Hitimisho
Yote kwa yote ni kwamba, matumizi ya kimtandao yana manufaa makubwa sana endapo mitandao itatumika vizuri. Kwa mfano, matumizi ya intelijensia bandia yamekuwa msaada mkubwa sana siku za hivi karibuni kwa wanafunzi ambapo inawasaidia kupata maarifa ya kielimu na kimaisha kwa kuuliza maswali mbalimbali yanayowahusu. Hivyo basi, endapo TCRA itaanza matumizi ya mfumo huu itakuwa imeleta msaada mkubwa sana katika kuhakikisha watumiaji wa mitandao wanakuwa salama zaidi. Lakini pia, jamii nayo inao wajibu wa kuhakikisha mitandao inakuwa salama kwa kutoa taarifa za tishio la uhalifu mtandaoni katika vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo polisi, na TCRA yenyewe.
By Boaz.

Upvote
1