DOKEZO Utendaji kazi wa TASAC unahatarisha maisha ya watu na mali zao kwenye Ziwa Viktoria

DOKEZO Utendaji kazi wa TASAC unahatarisha maisha ya watu na mali zao kwenye Ziwa Viktoria

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Posts
841
Reaction score
909
Mamlaka ya usimamizi wa usajili wa majini TASAC katika mkoa wa Mwanza, wameendelea kwa muda sasa kufanya jambo la hatari kwa maisha ya watu na mali zao kwa kushindwa kusimamia usafiri wa Majini katika ziwa Victoria.

Hivi karibuni zilitokea ajali mbli karibu na maeneo ya Kirumba jijini Mwanza ambapo watu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya vyombo vya majini walivyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Ziwa Victoria.

Kana kwamba hiyo haitoshi, mamlaka hiyo imeendelea kusuasua kuchukua hatua dhidi ya vyombo vinavyofanya safari kati ya Mwanza na Kamanga wilayani Sengerema ambapo maisha ya abiria na mali zao yamekuwa hatarni hata baada ya kufikishiwa tarifa za kuwepo kwa hali hiyo.

Imekuwa jambo la kawaida kwa siku za hivi karibuni ( jana ni mfano mwingine) kivuko cha Mkombozi kutoka Upande wa Kamanga kwenda Kirumba kilibeba abiria na mizigo ambapo magari yaliyokuwa katika kivuko hichp yalikuwa yakining'inia.

Hali ni hiyo pia katika kivuko "Geji" kinachofanya safari pia kati ya Mwanza na Kamanga ambako utaratibu wa kubeba abiria na mizigo hauzingatiwi.

IMG-20241010-WA0002.jpg
IMG-20241010-WA0004.jpg
IMG-20241010-WA0002.jpg
 
Back
Top Bottom