Utendaji wa ICDs-TALL

Bobby

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2008
Posts
2,182
Reaction score
1,896
Heshima kwenu wana JF!

Mimi ni miongoni mwa wale wanaosupport kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa Inland Container Depots (ICDs) kwani kwa kiasi kikubwa zimepunguza usumbufu tuliokuwa tukiupata kwenye kuprocess mizigo TPA peke yake. Lakini pamoja na mazuri ya hizi ICDs bado kuna mambo ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi. Mojawapo ni hili la muda wa kazi kwa hizi ICDs, naeleza kidogo hapa chini.


Jumamosi hii nilikuwa naclear gari kwenye ICD ya mheshimiwa katibu mkuu wa ccm hapo Shaurimoyo inayoitwa kwa kifupi TALL. Kule ndani of course kama zilivyo ICDs zote kuna madirisha mawili ya malipo moja la TPA na moja la ICD husika. Agent wangu alilipa dirisha la ICD saa 6 kasoro akaelekea kwenye dirisha la ICD ambako alipigwa stop na Director wa kizungu mwajiriwa wa Kinana kwamba muda wa kazi umeisha asubiri j3. Hili liliniboa sana kwani niliona kama ni uonevu na kama vile ana force biashara kwa kuattract storage charges zisizo na sababu. Lakini kingine kikubwa niliona upuuzi kama huu unaweza kuhatarisha kushuka kwa mapato ya TPA. Miongoni mwa wateja tuli0athiriwa na maamuzi ya mzungu yule mwajiriwa wa kinana ni wageni wakiwemo wazimbabwe. Najaribu kuimagine Mzimbabwe amekaa wiki nzima kufuatilia gari yake then jmosi saa 6 wakati anamalizia process yake anaambiwa asubiri J3.

Hilo liliishia hapo lakini machungu yangu yaliongezeka baada ya kupita maeneo ya Kibasila Secondary na kukuta kwamba ile ICD ilikuwa bado inafanya kazi saa 12 jioni. Sasa nikajiuliza hivi kumbe kila ICD ina moda wake wa kufanya kazi? Kwa hiyo mteja ambaye gari lake limefikia TALL analipa storage charges na mteja wa ICD nyingine hawezi kulipa storage charges hata kama mizigo yao imefika siku moja? I thought hawa ni kama agents wa TPA so wanapaswa kuoperate kwa same standards? Au hawa wenzetu wa TALL hii nyodo waliyonayo ni kwa sababu nchi wameibinafsisha? Kuna uzi ulitoka last week humu kwamba TPA walipata mapato ya 50 billion kwa mwezi Dec hii ni kama 16% ya pato la Taifa. Hii inaonesha ni jinsi gani TPA ilivyo na mchango kwa TAIFA lakini hatujawa serious namna ya kuioperate ili mchango wake uongezeke kwani fursa bado ipo kabisa tena ni kubwa.
 
Ndio tatizo la mwanasiasa kuwa mfanya biashara! Kubali au La kila mmoja wetu anawaza apate zaidi, sasa mwanasiasa hawezi kuwajibishwa kwa sababu yeye au jamaa zake ndio wenye uwezo huo!

Nchi hii sijui nani ataikomboa!!!!
 
hapo kwenye reds, kwa nini usingemwambia huyo bosi akamtumia hata sms ya kumwamrisha alitoe?
Hivi ni huyu Kinana katibu wetu anaajiri hata wazungu, naye si ni myonge kama sie wanachama wenzie?

Hilo pendekezo la muda lina maana sana. Ni vizuri kila ICD wakati wa kupewa reseni wakapewa na masharti kuwa inabidi waoparate kwa masharti yanayofanana kwa kiasi fulani na TPA.
Lakini chama chetu ccm ndicho kinatusababishia matatizo yote haya!

 
Pole sana mkuu.
Mimi tatizo Kama hilo lilinikuta hapo TALL mwaka jana mwishoni. Niliagiza usafiri kutoka Japan na kukubaliana na kampuni husika wapakie magari kwenye shipping line yoyote lakini sio itakayopeleka magari TALL kwa kuwa najua Nyodo za huyo Mzungu hapo.
Meli (ONYX ACE) iliingia Tanzania Kama ilivyotarajiwa,lakini bahati nzuri au mbaya kulikuwa kuna Meli inashusha mbolea kwa hiyo Meli ya ONYX ikachelewa kushusha magari Kama siku tatu. Nilipowasiliana na Shipping line Company (Inchcape shipping services) wakanihakikishia ya kwamba gari zitapelekwa ICD ya FARION (maarufu Kama mchicha). Kila kitu kilikuwa nimeshalipia nasubiri gari zifike ICD nizitoe.

Kwa mshangao wangu na wateja wengine Yale magari yote yaliyoshuka kwenye ONYX ACE yakapelekwa TALL ICD kwa amri ya kigogo fulani. Prior to that,TALL ilikuwa imefungiwa kwa muda Fulani. Kwa hiyo ONYX ACE ndio ilikuwa Meli ya kwanza kupeleka magari pale TALL. Gari zilifika pale TALL na process za utoaji zikaanza. Mind you mteja unatakiwa kuchajiwa storage fee siku Saba (7) baada ya Meli kufunga dock. Lakini wale majangiri wa TALL walikuja kunichaji mimi zile siku tatu ambazo Meli ilikuwa nje ya Dock ikisubiri nafasi ili ifunge Dock na kushusha magari.

Nililipa Kama milioni hivi kwa gari zote mbili kwa ajili ya storage fees ambayo ililazimishwa na Huyo Meneja Mzungu.
Kulikuwa kuna jamaa wametoka Zimbabwe walipata shida sana na kwa mujibu wa maongezi Yao.
Mwanzoni sikujua Kama huyu bwana Kinana anahusika na hii TALL ICD. Ila nilishangaa Huyu Meneja Mzungu kiburi anatoa wapi!?
Wadau kuweni makini na hiyo TALL ICD ni MAJANGIRI wa kutupwa na mchezo wao wa kulazimisha Storage Fees.
 
tumefanya kosa kubwa sana kuwapa wageni ikiwa ni pamoja na watanzania wasio waaminifu kwa nchi yao na kukosa uzalendo. Hawa watu walihitaji kudhibitiwa ili kuleta unafuu kwa wananchi wa kawaida lakini kinachotokea ni kinyume chake.

Ukienda kwenye hizi ICDs unakuta katatizo kadogo tu ka kumaliza mara moja wanakakuza alafu mzigo unalala ili waongeze storage ambapo ndipo ulaji wao ulipo hapo. Na ndio maana imekuwa ni kitu cha kawaida ukienda kwenye ICDs utasikia wanakwambia sijui system down lakini wakati huo huo system hizo hizo ziko up mipakani kote na bandarini kwenyewe (TPA).
Tuombee kuwa ukija utawala mwingine uweke jicho la ziada katika hili japo wamiliki wake ndio hawa hawa waliotufikisha hapa
 
Guys,

Thanks for all your comments and contibutions toka kwa dist111,Borat69,Omujubi,Lukindo na wengineo. Michango yenu ni ya thamani sana. Sikuwahi kujua kuwa kumbe inawezekana kupitia kwa shipping line kuinfluence gari iende ICD ipi ikifika Dar.

It's very bad namna ambavyo wanasiasa wanavyotaka kuipeleka hii nchi kusiko. Kiburi na jeuri ya mzungu wa TALL ni kwa sababu ya kinana na si vinginevyo. Mimi ni mdogo sana may be ukinilinganisha na kinana but I'm going to do something about this thing. Tembo watuibie, watucharge storage charges zisizo na sababu na bado tuake kimya? No way lazima tufanye kitu tusipofanikiwa its ok tutasema at least we tried.
 
mkuu Bobby, this on red sounds so promising and courageous.
Kuna watu ambao tunadhani ni wakubwa lakini tunasahau kuwa ujanja wao ni kama samaki kwenye maji, ukimtoa tu, ujanja wote kwisha. Hawa watu wanadhani wanafaidi na kuona ufahali wa wanayoyafanya na hawajali au hawajui kuwa matokeo ya matendo yao yanashusha hadhi ya bandari yetu na nchi kuwa ujumla.

Unaweza ukadhani ni mdogo lakini your good deed if is supported by another smaller like you and another, will finally have positive impact to these economical and political hooligans.
Hata mbuyu ulianza kama mchicha japo lifespan ya mchicha ni fupi ukilinganisha na mbuyu but tusipofanya chochote hakutatokea chochote pia, lakini tukifanya hata kidogo vipi ni lazima matokeo yawepo then tupate pa kuanzia

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…