Unadhani mtaepuka gharama na kusevu kwa sana mkijitengenezea wenyewe?...ni ya kuuza?
Well, ukipata mahitaji toka kwa wanajamvi anzia kwenye karatasi kwanza, piga cost-benefit analysis, ndipo uwashashauri wenzio...Uko kikundi cha WAWATA nini?
Mkuu unachohitaji ni mashine za kutengenezea mishumaa au ujuzi wa jinsi ya kutengeneza mishumaa??. Anyway huenda unahitaji vyote. Nimewahi kufanya kazi SIDO kama Engineer kwenye workshop iliyoko Moshi. Tulikuwa tunatengeneza mashine za kutengenezea mishumaa. Mashine husika zilikuwa na uwezo wa kutoa mishumaa minnne mpaka 16 kulingana na unene wa mshumaa. Challenge kubwa ni jinsi ya kupata raw material. Wasiliana kwa namba 0754 399922 kwa maelezo zaidi. Nakumbuka tumewahi kuuza katika vikundi vingi hasa hapa Dar na makanisani.
Raw material ya kutengenezea mishumaa inapatikana sana nadhani maeneo ya Kariokoo kuna wahindi walikuwa wanaagiza kutoka India. Hata locally kuna watu wana process hasa maeneo ya Dodoma na Singina au Tabora sehemu ambazo kuna ufugaji wa nyuki ili kupata nta ambayo hutumika kuzalisha mishumaa. Wasiliana na ofisi yoyote ya SIDO iliyokaribu nawe wanaweza kukupa network ya kupata raw material.
Asante mkuu kwa ushauri wako
nitafanya hivyo,
kila la kheri mkuu wangu.