Lameck Ezekiel
New Member
- Sep 14, 2022
- 4
- 3
Bila shaka sote tumekuwa mashahidi wa udhihirisho wa ukweli kuwa‘’siku zote mwanadamu anapambana kupunguza maumivu na kuongeza furaha’’ hususani kwenye nyakati za leo za maendeleo ya sayansi na teknolojia. Jambo hili limechochea biashara na utengengenezaji wa pesa kupitia haki za miliki bunifu (intellectual propertyrights), miongoni mwa mataifa.
Lakini ni ukweli pia kuwa faida halo za miliki bunifu hutegemea sana sheria ambazo nchi husika imejiewekea katika kuzilinda.
Hii ni kwa sababu ulinzi wa kisheria wa miliki bunifu ni wa kimipaka (territorial protection).
Swali kwa Tanzania ni je, ni kweli kwamba haki za miliki bunifu zinalindwa kikamilifu kupitia sheria zilizopo kiasi cha kuwawezesha wamiliki kupata faida tarajiwa?
Na je, ni upi mchango wa serikali katika kuhakikisha kuwa miliki bunifu zinalindwa kiasi cha kuendana na kasi ya kidunia ya maendeleo?
Kwa kuzingatia maswali haya, ni madhumuni ya andiko hili kumulika ulinzi wa miliki bunifu uliopo, na jinsi ya kuuboresha zaidi ili kuifanya Tanzania pia kuwa miongoni mwa nchi zinazonufaika na faida itokanayo na miliki bunifu. Kimsingi kwa mtu aliyewahi kufuatilia muundo wa sheria za Tanzania juu ya ulinzi wa haki za miliki bunifu nchini mwetu, atakubaliana na mimi kuwa haujawekwa kwenye hali halisi ya kuchochea utengenezaji wa pesa kwa wamiliki wa haki za miliki bunifu. Hii ni tofauti na sheria zingine kama sheria za kodi amabazo serikali na bunge limeangazia macho yake kila kukicha. Kwa mfano, sheria za Tanzania ziko kimya juu ya ulinzi wa baadhi ya miliki bunifu hivyo kufanya ulinzi wakekutegemea sheria za nje, mfano mzuri ukiwa siri za biashara (trade secrets).
NI NINI KIFANYIKE SASA ILI KUCHOCHEA MANUFAA YA MILIKI BUNIFU NCHINI TANZANIA?
Elimu ya kutosha itolewe kwa umma; Kampeni iliyoanzishwa na wizara ya katiba na sheria ya
utoaji wa elimu ya kisheria kwa wananchi, inatakiwa pia iambatane na utoaji wa elimu juu ya haki za miliki bunifu kwa umma. Ni ukweli usiopingika kuwa jamii ya watanzania wakiwemo na wamiliki wa haki za miliki bunifu wenyewe hawana uelewa wa kina juu ya namna ambavyo mali zao zinaweza kulindwa na jinsi ambavyo wanaweza wakawashughurukia wale wanaozichezea mali hizo bila idhini yao.
Leo tunaona jitihada za wamiliki wa hati miliki (copyrighty) hususani wasanii chipukizi zikigonga mwamba kutokana na kwamba hawana elimu juu ya ulinzi wa mali zao.
Pia, kuna wafanyabiashara wengi ambao wana biashara alama nzuri (trade marks)
lakini unakuta bado hazijasajiriwa. Kukosekana kwa uelewa huu unafanya biashara zao kutochanua kwa haraka. Hii ni kwa sababu uwekezeji pekee wa biashara alama unaweza ukamfanya mtu kupata mamilioni ya pesa.
Taasisi za kusimamia sheria za miliki bunifu lazima zitengezwe na zilizopo kuimarishwa katika
ufanisi wake. Kuna miliki bunifu ambazo pamoja na uwepo wa sheria zinazozilinda lakini hakuna
taasisi za kuzitekeleza sheria hizo. Kwa mfano, ni Jambo la kushangaza kwamba pamoja na kupamba moto kwa mkakati wa ‘’Tanzania ya viwanda’’ bado mpaka leo Tanzania haina ofisi ya kusajiri miundo ya kiviwanda (industrial designs).
Lakini pia ni wakati sasa wa taasisi ya kulinda hati miliki yaani COSOTA, kuimarishwa hasa kwenye suala la ukusanyaji na ugawaji wa mirahaba kwa wasanii. Pia COSOTA inatakiwa itafute namna ya kuhakikisha kazi za wanasanaa chipukizi hazihujumiwi na kuibiwa bila idhini yao, ili kuwafanya wafaidi jitihada za jasho lao maana, utumiaji usiohalali wa kazi hizo umekithiri sana nchini.
Sheria inayojitegemea inatakiwa itungwe kulinda sanaa za jadi (folkrole) na ujuzi asilia(traditional
knowledge) wa kitanzania. Tanzania kimsingi tumefanikiwa kuwa na sanaa za jadi pamoja na ujuzi tofauti tofauti asilia kwenye jamii zetu ambao umekuwa ukitusaidia toka enzi za mababu zetu. Na hizi ni moja ya miliki bunifu ambazo kama zingelindwa vizuri zingeliingizia taifa letu pesa za kutosha kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa mengine kama Nigeria.
Kwa sasa hakuna sheria maususi ya kulinda ujuzi asilia badala yake unalindwa chini ya sheria ya hati miliki (The Copyright and Neighbouring Act). Kitendo cha sanaa za jadi na ujuzi asilia kulindwa ndani ya sheria ya hati miliki kimesabisha ujuzi huu usilete matunda tarajiwa kwa taifa. Mataifa ya kigeni badala yake yamekuwa yakitumia ujuzi huu kwa manufaa yake binafsi na kutuacha mikono mitupu.
Hii inasababishwa na kwamba ulinzi ndani ya sheria ya hati miliki unafungwa ndani ya muda, na wakati sanaa za jadi na ujuzi asilia unatakiwa kulindwa muda wote.
Na pili, ulinzi ndani ya sheria hii unalenga kumunufaisha mmiliki binafsi amabaye kimsingi awe anatambulika, wakati ujuzi asilia ni wa jamii nzima.
Mfano kupitia sheria mahususi ya kulinda miliki bunifu hizi, mapato ya mikoa yenye utalii kama vile Arusha yataongezeka kwa maana kwamba sanaa za jadi pamoja na ujuzi asilia utapata soko kwa wateja si tu wale wa ndani bali hata wa nje ya nchi. Na kwa maana hiyo milango ya ajira itafunguka na hivyo kupunguza wimbi la umasikini kwa wananchi.
Kwa ujumla, kunatakiwa kufanyike mapitio ya sheria za haki za miliki bunifu na kutengeneza sheria nyingine maususi ili kupanua wigo wa ulinzi wa kisheria wa haki hizi. Lakini pia utoaji wa elimu kwa watanzania ni muhimu sana ili kuwafanya watu wajue kiundani jinsi wanavyoweza wakatengeneza pesa kupitia miliki bunifu.

Upvote
1