Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Asante kwa elimu, nitatafuta hizo materials nitoe yangu nitaleta mrejesho.
 
NINAHITAJI MATERIAL YOTE HAYO ILI NIJARIBU KUTENGENEZA, SASA JE, NITAPATA WAPI HIZO MALI GHAFI ULIZOTAJA HAPO?
Kariakoo, kule gerezani ukitokea pale roundabout ya uhuru kama unaelekea kamata, barabara ya tatu kushoto unashuka na hiyo barabara ukiuliza duka la vifaa vya ujasiliamali utaonyeshwa yako kama mawili ninayoyafahamu maeneo ya kule gerezani.
 
Tembelea u tube, kuna elimu nying sana kuhusu iko kitu, na nirahisi sana kuelewa bila ht ya kuingia darasan.
Nimeingia You Tube, wanaelezea vizuri sana na ni mambo marahisi kabisa, unapata sabuni very natural. Nimeamua kuanza kutengeneza sabuni za kuogea kwa ajili ya familia yangu na sio kununua tena madukani.
 
Asante saana.
Mkuu mie naomba break down ya Sabuni / dumu Moja la mafuta, yaani margafi ninazohitaji pamoja za uzito wake. Shukran
 
Tatizo kubwa ni soko, unapambana na MO, Azania, Murzah, Wachina, Wakenya

Hao kushusha bei ni dakika 0
 
Ukija na sabuni zako za kuundaunda ujipange ndugu kwani nakukabizi dekio litakate ndio nakuungisha.
 
Ukija na sabuni zako za kuundaunda ujipange ndugu kwani nakukabizi dekio litakate ndio nakuungisha.
Wajasiliamali tunafeli kwenye matangazo tu kiongozi Kama bidhaa unakuta tuna bidhaa nzuri mno
 
Wajasiliamali tunafeli kwenye matangazo tu kiongozi Kama bidhaa unakuta tuna bidhaa nzuri mno
Sio matangazo pekee

Tunafeli kwenye Distribution pia

Tunafeli kwenye packaging

Tunafeli kwenye finishing, mashine za SIDO zafaa kujifunzia tu na si kupeleka bidhaa dukani

Tunafeli pia kwenye ubora endelevu, kwamba leo pH ya sabuni batch hii itatofautiana na batch nyingineyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…