Utenguzi wa Nape, Rais ameongea kwa vitendo

Utenguzi wa Nape, Rais ameongea kwa vitendo

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
RAIS SAMIA, alikuja na falsafa ya 4Rs. Nape akampinga Rais kwa kauli isiyo ya wazi moja kwa moja. Lakini Nape ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri, ambalo kazi yake ni kumsaidia Rais. Baada ya kauli yake ya hivi karibuni, haikuwa wazi kama Nape anamsaidia Rais kutekeleza 4Rs au anamsaidia Rais kuzifuta 4Rs.

Kwa kumwondoa Nape kwenye baraza la Mawaziri, japo hajanena kwa kauli, amenena kwa vitendo kuwaambia wananchi kuwa kauli ya Nape ilikuwa ni ya kwake Nape, siyo kauli ya Serikali, siyo ya Rais na wala siyo ya Baraza la Mawaziri, na kwamba Rais hajaifuta falsafa yake kimya kimya kama baadhi tulivyoanza kufikiria.

Kiuongozi, Rais amefanya kilicho sahihi kabisa maana haiwezekani kwenye uwajibikaji wa pamoja, Serikali moja iwe na falsafa tofauti tofauti kwenye jambo moja.

Wakati tunampongeza Rais kwa hatua sahihi za kiuongozi, tunamshauri alitizame jeshi la Polisi, Waziri Mambo ya ndani na hawa wanaoitwa wasiojukikana. Vitendi vyao vya kuteka watu haviendani kabisa na falsafa ya 4Rs. Rais asidanganyike kuwa eti utekaji ni drama.

Pia soma=> Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
 
Tuangazie uhamisho wa slaa kuchukua nafasi ya nape. Mi naona kule ardhi kulimfaa sana. Au kuna vigogo wameguswa huko na biashara zao za viwanja?
 
Wewe umepewa cheo kikubwa.alafu bado unaongea ongea ujinga.
Mwanakulipata
 
RAIS SAMIA, alikuja na falsafa ya 4Rs. Napè akàmpinga Rais kwa kauli isiyo ya wazi moja kwa moja. Lakini Nape ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri, ambalo kazi yake ni kumsaidia Rais. Baada ya kauli yake ya hivi karibuni, haikuwa wazi kama Nape anamsaidia Rais kutekeleza 4Rs au anamsaidia Rais kuzifuta 4Rs.

Kwa kumwondoa Nape kwenye baraza la Mawaziri, japo hajanena kwa kauli, amenena kwa vitendo kuwaambia wananchi kuwa kauli ya Nape ilikuwa ni ya kwake Nape, siyo kauli ya Serikali, siyo ya Rais na wala siyo ya Baraza la Mawaziri, na kwamba Rais hajaifuta falsafa yake kimya kimya kama baadhi tulivyoanza kufikiria.

Kiuongozi, Rais amefanya kilicho sahihi kabisa maana haiwezekani kwenye uwajibikaji wa pamoja, Serikali moja iwe na falsafa tofauti tofauti kwenye jambo moja.

Wakati tunampongeza Rais kwa hatua sahihi za kiuongozi, tunamshauri alitizame jeshi la Polisi, Waziri Mambo ya ndani na hawa wanaoitwa wasiojukikana. Vitendi vyao vya kuteka watu haviendani kabisa na falsafa ya 4Rs. Rais asidanganyike kuwa eti utekaji ni drama.
Umenikumbusha, eti mtuhumiwa, (mlalamikaji), alijiteka
 
Tuangazie uhamisho wa slaa kuchukua nafasi ya nape. Mi naona kule ardhi kulimfaa sana. Au kuna vigogo wameguswa huko na biashara zao za viwanja?
Huwa najiuliza ,Mama hataki mtu aupige mwingi? Atamzidi Cv? Au anampeleka mtu kwingine akapige mzigo Kwa ustadi Kama ule wa upande aliotoka?
 
Mheshimiwa @dorothygwajima eti haya yasemwayo humu ni ukweli 😃
 
Hii meseji ya SSH itawafikia/ishawafikia-let it sink in- na wengine. Wakaze buti sasa. SSH amedhamiria.

Kazi iendelee.
 
Back
Top Bottom