Utenzi- Hatunae Tena Majuto

Utenzi- Hatunae Tena Majuto

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
HATUNAE MAJUTO.


1.Kila nafsi duniani
Taingia kaburini
Sote yupo safarini
Twapita kwenye dunia.


2.Imendikwa vitabuni
Siyo tungo za kubuni
Kifo kipo karibuni
Hakuna wakubakia.


3.Ila Mumba wa mbinguni
Kwake twende kutubuni
Toba iwe ndo dhumuni
Tena tufanye kwa nia.


4.Ulazwe pema peponi
Twahisi tupo ndotoni
Siku yetu hatuoni
Nani atatangulia.


5.Majonzi pia huzuni
Na machozi mashavuni
Umefika hatimani
Kuwayo kwenye dunia.


6.Kuonana tena lini
Tutakutia machoni
Tulikupenda fwadini
Ila umetangulia.


7.Twaisoma talqini
Na dua nyingi za dini
Mauti hayana kani
Sote tutayapitia.


8.Hata uwe himayani
Mbali kama Marikani
Kifo hakina utani
Huko kitakuchukua.


8.Ni huzuni kwenye fani
Mashabiki mtaani
Wakwombea Athumani
Majuto me tangulia.


9.Uhai huna thamani
Tujiandae jamani
Kifo kwetu darasani
Mengi pakujifunzia.


10.Hijalishi ni angani
Nchi kavu na porini
Mlimani baharini
Kifo kitatufikia.


11.Na pesa kiasi gani
Uwe nacho mfukoni
Mbele yake masikini
Kifo hatokuelewa.


12.Burudani jukwaani
Hata kule runingani
Ulikuwa ni makini
Sana ki kuitendea.


13.Ilikuwa burudani
Tamu iso na kifani
Ni kweli siyo utani
Nyota imeshapotea.


14.Wa kuliziba ni Nani
Pengo lako pa nchini
Sote tuna kaa chini
Huku twakombea Dua.


15.Futuhi sa hatarini
Kufutika runingani
Iwapi yako thamani
Serikali kulindia.


16.Wala hukwenda chuoni
Ni uwezo wa manani
Na ubunifu kichwani
Mola alokujalia.


17.Wa kukuenzi ndi Nani
Mbona bado tumuoni
Ulipokua kazini
Mzaha hukufanyia.


18.Hata filamu za dini
Tuliona majumbani
Leo taicheza Nani
Nawe umeshapotea.


19.Nyingi Dua kwa manani
Uwe wanja wa peponi
Chumba chako mwanandani
Rabi apate jalia.


20.Amini rabi amini
Taqabal rahmani
Waja wako waumini
Ipokee yetu dua.


SHAIRI -HATUNAE MAJUTO.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
 
Steve nyerere Mzee wa kuiba rambirambi namuona ananyapia nyapia
 
Back
Top Bottom