SoC01 UTENZI: Kuipenda Tanzania, Ni Corona Kuzuia

SoC01 UTENZI: Kuipenda Tanzania, Ni Corona Kuzuia

Stories of Change - 2021 Competition

ROJA MIRO

Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
52
Reaction score
56
1.Kila mtu anajua,
Kiloikumba dunia,
Huruma itakujia,
Habari ukisikia,
Kwa kubwa asilimia,
Wengi wakiangamia,
Tuwaze na kuwazua, Corona kuizuia.


2.
Vifo vinavyotokea,
Afrika na eshiaa,
Italia na India,
Kote wanaugulia,
Kikubwa kilobakia,
Tahadhari kuchukua,
Na tusione udhia, Afya zetu kuokoa.

3
.Maji ya kusafishia,
Mikono tiririshia,
Na pua kuikingia,
Chafya inapokujia,
Hapo itasaidia,
Na wengine kuokoa,
Kujilinda yangu nia, Wengine na sote pia.


4.
Mikono kutokutoa,
Twaweza tukiamua,
Kikohozi kitokea,
Pembeni kukoholea,
Hayo na mengine pia,
Corona kuizuia,
Mwenye sikio sikia, Mwenye macho angalia.


5.
Mikusanyiko huria,
Ni bora kuepukia,
Zisizo salama pia,
Safari kuzizuia,
Magari ya abiria,
Levo siti zingatia,
Hata tunaowajua, Si vyema kukumbatia.


6.
Zilizuka dhahania,
Ambazo tulisikia,
Za mtoto kuzaliwa
Na kisha akaongea,
Eti dawa kausia,
Ya watu kuitumia,
Tusifate dhahania, Mtanzania tambua.

7.
Wapo walioongea,
Ukweli kupotoshea,
Na chai ni dawa pia,
Ya rangi ukijinywea,
Eti utajikingia,
Corona kukuingia,
Mzaha tukifanyia, Usaha tutatumbua.


8.
Na za mwanzo nadharia,
Zile zilizotokea,
Weusi rangi sawia,
Rahisi kujiponea,
wengine kuongezea,
Joto litatuokoa,
Maneno ya kusikia, Mbayuwayu ongezea.


9
.Kitu cha kuzingatia,
Tuache kupuuzia,
Wataalamu afiya,
Ushauri wakitoa,
Tukijifanya kujua,
Jua litatuwakia,
Tupange na kuchagua, Kabla ya jua kutua.


10.
Habari kufatilia,
Zile zinazotokea,
Kwa luninga aminia,
Magazeti jisomea,
Radio ukisikia,
Tega sikio sikia,
Elimu ukiijua, Na wenzako elezea.


11.
Ukingoni karibia,
Mengi nimeelezea,
Tunapeana wosia,
Muhimu kukumbushia,
Hili suala hatia
Utani kulifanyia,
Corona imeingia, Si utani nakwambia.


12.
Cha mwisho kumalizia,
Sote tuwe moja nia,
Nyumba yetu Tanzania,
Fito tusijegombea,
Mawazo kusaidia,
Viongozi na raia,
Kuipenda Tanzania, Ni Corona kuzuia.







ROJAMIRO.

rajabumrope18@gmail.com

0626496734

Utenzi huu ni mali ya mtunzi hairuhusiwi kuiga,kukopi au kunakili bila ruhusa ya mhusika.

NAOMBA KURA YAKO TUENDELEZE NA KUBORESHA TAALUMA YA UANDISHI WA MAUDHUI YENYE TIJA MTANDAONI.
 
Upvote 0
KARIBU KUNIPIGIA KURA PIA TOA MAONI YAKO JUU YA CORONA HAPA
 
Back
Top Bottom