Elections 2010 Utenzi kwa wana wa nchi

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,290
Reaction score
2,468
Japo mie mgeni
Kunako jamvini
Si wa fikra asilani
Hilo nataka mbaini

Enyi wana wa nchi
Nchi yenu i uchi
Mabedui wanaisachi
Toka enzi i bichi

Wameishika pabaya
Waichezea ka' malaya
Mwasikia enyi wa kaya
Chonde muyaelewe haya

Ndipo ikaja sauti
Thamani yake Yakuti
mwanamapinduzi wa dhati
Wote tumpigie saluti

Sauti ya jasiri jukwaani
Inatufuata vyumbani
Inatusonga mtimani
Inawatesa kwa yakini

Mengi yake tumeyasikia
Pande zote Tanzania
Anayo dhati na nia
Kwa jinsi alivyojifunua

Wa Mtwara hadi Musoma
Kigoma hadi Mchambawima
Hima hima hima hima!
Tuungane Tanzania nzima

Kikosi kamili kazini
Chama cha watu makini
Hakika tupo vitani
Nchi kuidizaini

2010 hatudanganyiki!
Si kwa bia si kaniki
Twasema dhulma kafariki
Naisikia harufu ya haki
2010 HA-TU-DA-NGA-NYI-KI
 
Asante kwa utenzi mzuri ila nakuwa na wasiwasi manake na ugeni wako huo umeweza kuingia na Avatar!!!!!!!!!!
 
Asante kwa utenzi mzuri ila nakuwa na wasiwasi manake na ugeni wako huo umeweza kuingia na Avatar!!!!!!!!!!
mkuu inategemea na spidi ya mtu kujua mambo. Ninafahamiana na wadau humu jukwaani hivyo usione ajabu. wamenipa shule ya kutosha
 
Wameishika pabaya
Waichezea ka' malaya


Mwisho wao umefika... Dr. Slaa and his Team with our support will take of them!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…