UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka...


Naona tumeamua rasmi kuingilia uhuru wa mahakama....sijui sheria inasemaje may be kwakuwa tunatumia avatar kwenye social media ....Anyway muhishimiwa ruta naona leo umejitosa kumtetea lulu....Well ni haki yako pia ila nadhani kilichofanyika jana ni kumuondoa lulu pale oyesterbay na kumpeleka Segerea kwakuzingatia kuwa saa 24 zilishapita.... Usishangae hayo mashitaka yakabadilishwa na kuwa manslaughter. Pia ni vigumu kujua walicho nacho wapelelezi mkononi so far.

Uzuri hata mazungumzo ya Lulu na kanumba kwa siku kadhaa zilizopita hadi siku alokuwa anakwenda kwake tayari wanayo. Hayo yatathibitisha kuwa alikuwa "akijilinda " dhidi ya "ubakaji" ama la. Pia yataonesha chanzo cha ugomvi ninini?? Hata alichozungumza Lulu na mashosti zake baada ya "kujilinda" dhidi ya ubakaji nacho ni sehemu muhimu kwenye hii kesi...Mkuu Allien amekukumbusha pia kuna ripoti ya mkemia inasubiriwa.


Kwa maoni yangu (ingawa si mwanasheria kama wewe) ni mapema mno kuhitimisha jambo hili na kwakuwa hatuna information za kutosha tuupe mda nafasi.
 

lulu hahitaji kuthibitisha kuwa alibakwa bali mwendazake alitaka kumbaka inatosha na hao taarifa ya hao madaktari hawahitajiki
 

Muhimbili wamesema ni kifo cha kawaida....................haya yote wala hayana maana yoyote.........
 

Alipokuwa anaoga alikuwa pia ameingia bafuni na kinywaji? Be serious bana.

Jack daniel na sprite aliviacha room.

So, subiri ushahidi kwanza Mwanasheria. DPP is not stupidi kuanzisha mashtaka bila kuwa na ushahidi wa awali wa kutosha.
 

tatizo la dunia ya sasa ni idolatry...................and idol worshiping........................mtu akiwa celebrity basi yuko kwenye mstari lakini akiwa kapurwa basi sheria huitwa ni msumeno.........
 
lulu hahitaji kuthibitisha kuwa alibakwa bali mwendazake alitaka kumbaka inatosha na hao taarifa ya hao madaktari hawahitajiki
jUST BY SAYING? Yaani akisema alitaka kubakwa ndiyo maana akamsukuma (or sumthing) unadhani itahalalisha innocence?
Mkuu, it's more than what u think.Ila inaonyesha kuwa una ubishi wa aina fulani.
 
Muhimbili wamesema ni kifo cha kawaida....................haya yote wala hayana maana yoyote.........

Mkuu acha uongo? Mbona hujibu hoja zangu pale juu? Brain Concusuion ina Cause. Cause yake ilikuwa ni nini? Dont rush into simple answers!

Wewe una Agenda yako maana toka day one Kanumba nafariki mara ooh alimkashfu mungu kupitia movie yake, mara ooh Kanumba anaumwa . . . na bado unaendelea with no proof at all. And u call yourself a lawyer just kwa kulazimisha kuwa Lulu was a minor. If you dont come with strong arguments, I am adding you up in my Ignore List,

Najua una highest posts hapa JF, but please leta hoja usilazimishe.
 
Ni vigum kuamin kama ni wewe!
 
Mwana JF,
Awali ya yote, nikupongeze kwa kuanza jumjengea Lulu hoja za utetezi dhidi ya kesi inayomkabiri. Mimi pia kwa mtazamo wangu, ningependa binti huyo awe huru kwani kwa mujibu wa umri wake, kwa wakati huu inampasa awe shule kujiandalia maisha yake vizuri kulingana na kipaji chake kama kinavyoonekana machoni kwa wanajamii. Kutokana na mazingira ya kesi yalivyoonekana kwa hatua za awali, na kwa kuzingatia tafsiri ya "mtoto ni nani" kisheria, DPP imempasa kumshtaki binti huyo kama unavyosema ni mdogo, yaani ana miaka chini ya 18. Hata hivyo, ushahidi wa awali wa kielectronia (electronic testimony) unathibitisha kwamba Lulu alishakuwa mpenzi wa Marehemu Kanumba toka muda mrefu kabla ya siku ya tukio. Ushahidi huohuo wa kielectronia unathibitisha kuwa Lulu alishaanza kugawa pipi yake toka miaka kadhaa iliyopita hivi kuendelea na hako kamchezo kwake ni jambo la kawaida. Aidha sheria ya makosa ya jinai ya Tanzania haimzuii mtoto kutoshtakiwa isipokuwa kinachoangaliwa ni kwamba ni kwa kiwango gani mtoto huyo anauelewa juu ya kosa alilolifanya (inteligence vs knowlege on the fact in issue ya mstakiwa). Endaapo ikibainika kuwa wakati akifanya kosa hilo mtoto huyo alikuwa akijua anachokifanya kuwa ni kosa kisheria, hapo bila chembe ya shaka mahakama humtia hatiani mtu huyo bila kujali umri wake kuwa ni mdogo kama unavyomtetea binti Lulu. Kwa mantiki hii ningependa urejee yafuatayo ili ujiridhishe na ujengaji wako wa hoja dhidi ya utetezi wa Lulu.

1.Sheria ya makosa ya jina (Criminal Law) na mwenendo wa makosa ya jinai (Criminal Procedure Act) za nchi yetu (Tanzania) zinamtafsiri vipi mtoto?
2. Mahusiano ya Lulu na Kanumba kimapenzi yalianza lini?
3. Rejea uzito wa kosa na hali halisi ya maisha ya Lulu na Marehemu masaa 10 kabla ya kifo chake
 
tatizo la dunia ya sasa ni idolatry...................and idol worshiping........................mtu akiwa celebrity basi yuko kwenye mstari lakini akiwa kapurwa basi sheria huitwa ni msumeno.........

Unachofanya sasa ni UBISHI kama mdau moja alivyosema. Huna hoja za kisheria wala huna focus ya kuona hoja zingine ukazipima. Such a great thinker!
 

Kama wewe ukiwa hakimu naamini huyu unayemuita mtoto hatakuwa na kesi ya kujibu. Na kama hakimu atakuwa mwingine yeyote yule isipokuwa wewe basi huyu binti atakuwa na kesi ya kujibu. Na ikienda mahakamani then Jaji kama utakuwa wewe huyu mtoto atakuwa innocent otherwise, imekula kwake. Atachezea miaka kadhaa ndani she can't walk. Atakutwa na kesi ya Manslaughter (kuua bila kukusudia).

Mimi sio mwanasheria ila nimesikia wanasheria wazuri kadhaa wanaongelea hii issue inaonekana huyu binti hana pa kutokea unless uchezwe mchezo. Ni lazima akae ndani kumnusuru na mob justice. Kama huyu angekuwa mwana CCM basi hayo unayoongea wewe Mhe. Ruta yangewezekana kabisa kwa hali na mali
 
jUST BY SAYING? Yaani akisema alitaka kubakwa ndiyo maana akamsukuma (or sumthing) unadhani itahalalisha innocence?

Mkuu, it's more than what u think. Ila inaonyesha kuwa una ubishi wa aina fulani.


Mkuu si tu ubishi wa aina fulani, inaonekana jamaa kasomea na kufuzu ubishi. Haoni hoja nyingine yoyote zaidi ya kulazimisha miaka. Ndio Wasomi wetu wa leo.

Let me do something else now. Kishaniboa. Hana hoja.
 
Kwaiyo atoke kwake aende kwa mwanaume sa sita usiku aingie chumbani kwake xpctn what?tuition or?ok kashabakwa kwnn asipige kelele kuomba msaada?ok kakimbia kwanini asikimbilie straight police kutoa mashtaka..watu wasimchuuze uyu mtoto aseme ukweli coz hakuua kwa kukusudia that one is wide n clear ila asichanganye watu jamii itazidi kumhaunt..itakulaje kwake uko mitaani..kabakwa?!he
 
Kama katika kesi suala la umri ni critical, then ni wazi upande wa upelelezi/mashitaka utalifanyia kazi zaidi suala hili.

Wengi mnaweza kuwa mnafahamu utaratibu wa kupata vyeti vya kuzaliwa. Binafsi siamini sana hivi vyeti vya kuzaliwa kwa sababu nafahamu watu kadhaa ambao waliweza kupata hivyo vyeti vikionesha umri wanaoutaka wao na sio ule halisi.....angalau siku hizi kuna utaratibu mzuri zaidi ingawa bado sio fogery proof. Kwa hiyo kwa kuzingatia mkanganyiko juu ya umri wa Lulu inawezekana upande wa upelelezi ukataka kwenda zaidi ya cheti cha kuzaliwa katika kuestablish umri halisi wa Lulu.

Suala la umri hasa kwa watu waliozaliwa miaka ya karibuni (kama kina Lulu) sio vigumu kivile kulithibitisha...wengi wa hawa watoto wamezaliwa hospitali au vituo vya afya hivyo sio vigumu kupata records. Pia, kuna records za shule, hospitali alikokuwa anatibiwa, pasipoti, driving licence nk zitaonesha umri....ingawa kujaribu ku corroborate records hizi pia kunaweza kuzua makosa mengine ya kughushi nyaraka (kwa Lulu ama wazazi/walezi wake!).
 
Mbona wa-tz tuna hara hivi? Tungoje tuone kesi itaendeshwaje maana mpaka sasa hakuna hata m2 mmoja anayejua hasa kilitokea nini zaidi ya kuhisi na kusikia kuwa marehemu alisukumwa. Huenda kweli alihisi wivu kwa kimwana akataka kukipa adabu, on the process akateleza akaanguka au kweli alisukumwa akaanguka vibaya. All in all ili m2 awe na hatia ya kosa la mauaji lazima idhibitike kuwa alikuwa na kitu kinachoitwa kitaalamu "MALICE AFORETHOUGHT", yaani alikuwa na kusudio la ama kumsababishia majeraha makubwa marehemu au kumsababishia kifo, kitu ambacho mi naoma kwa Lulu hakikuwepo.
Zaidi anaweza kupatikana na hatia ya kuuwa bila ya kukusudia, yaani Killing in self defence.
 


1. Nikuongezee mwaka jana kama sijakosea alifanya bonge laparty la kufikisha miaka 18 na alishaojiwa na Ramaradi wa Clouds TV na Salama wa EATV kuhusu maisha yake na alisema kuwa tayari amefika miaka 18 na yuko huru sasa kusaini mikataba mbalimbali yeye mwenyewe kwakuwa sheria inamruhusu hana wakumkataza kwani ni mtu mzima anaelewa jema na baya, tena salama nakumbuka alimchomekea kuhusu kuwa na boyfrien akasema hana kwani she is just 18yrs so anasubiri kwanza aangalie upepo.

2. kama ni 17yrs alifuata nini usiku kwa Kanumba, haya kama ulipigiwa simu kuhusu kazi ya filamu huwa zinafanyika usiku wa zaidi ya saa 6????
ok ni masuala ya kikazi ilikuaje ukaingia chumbani kwake anapo lala na wakati unajua mazungumzo hufanyika sebuleni ama barazani ikiwa uko nyumbani kwa mtu ama Kanumba alimwambia kule chumbani ndio studio waende wakaongee..... narudia tena jana nilisema anayemshauri Lulu anamshauri vibaya kwani wanajifunga wenyewe, ushaidi wa picha hata video za uchafu w lulu zipo, picha za party ya miaka 18 na interview alizohojiwa zipo atatokea wapi??
 
Alipokuwa anaoga alikuwa pia ameingia bafuni na kinywaji? Be serious bana.

Jack daniel na sprite aliviacha room.

So, subiri ushahidi kwanza Mwanasheria. DPP is not stupidi kuanzisha mashtaka bila kuwa na ushahidi wa awali wa kutosha.

una ushahidi wa ya kuwa aliingia bafuni na kumwacha Lulu chumbani mwake?

hili la sumu hata DPP hana na haiwezi kuwa sababu au ushahidi ambao aliutumia katika kumfungulia kesi hii ya mauaji...............kwa hiyto lipo nje ya huu mjadala.

Ninachojaribu kufanya hadi hivi sasa ni kutafakari utendaji wa DPP na wala siyo mahakama kama baadhi ya wachangiaji wanavyodhani.........na swalli hadi kesho halina majibu............ni je DPP alikuwa na ushaidi wa kutosha wa kumkamata Lulu na hata kumfungulia kesi ya mauaji? Ni kuwa hana na hata ule alionao unamsafisha Lulu..............sasa kwani anakuza mambo ambayo hayapo.................ninadiriki kusema DPP is just a victim of mob justice just like Lulu is............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…