Uteuzi Agosti 6, 2024: Rais Samia afanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali

Uteuzi Agosti 6, 2024: Rais Samia afanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

(1) Prof. Faustin Rweshabura Kamuzora ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTTAMIS. Prof. Kamuzora ni Katibu Tawala wa Mkoa Mstaafu, anachukua nafasi ya Bw. Casmir Kyuki ambaye amemaliza muda wake;

(ii) Prof. Joseph Andrew Kuzilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP). Prof. Kuzilwa ni Profesa Mstaafu, Chuo Kikuu cha Mzumbe; na

(iii) Prof. Ahmed Mohamed Ame ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kwa kipindi cha pili.

Uteuzi huu umeanza tarehe 04 Agosti, 2024.


1722971760528.png
PIA SOMA
- Uteuzi Julai 31, 2024: Rais Samia aunda Tume ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms)
 
Kizilwa pia si yuko Open University kwa nafasi kama hiyoe?
 
Oooh Prof Kuzilwa I can remember those days at Mzumbe University. Hongera na Mungu akusimamie katika majukumu mapya
 
Back
Top Bottom