Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma
Prof. Makubi anachukua nafasi ya Dkt. Alphonce B. Chandika ambaye amemaliza muda wake
Kabla ya Uteuzi, Makubi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Ubongo, Muhimbili (MOI) Awali, amewahi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Afya
PIA SOMA
-
Prof. Makubi afanya kikao cha kimkakati na Madaktari Bingwa/bobezi ndani ya MOI
LEO WAFANYAKAZI MOI WAMLILIA NA KUMPONGEZA PROF. MAKUBI
Simanzi na pongezi zilitawala ndivyo unavyoweza kusema wakati wa hafla fupi ya Menejimeti na wafanyakazi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) walipoagana na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wake Prof. Abel Makubi ambaye ameteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Makao Makuu ya Nchi jijini Dodoma.
Katika hafla hiyo iliyofanyika leo Juni, 7, 2024 katika ukumbi wa MOI Mpya wajumbe wa Menejimenti kwa niaba ya wafanyakazi walishindwa kuzuia hisia zao za huzuni kwa uhamisho wa kiongozi wao ambaye ndani ya miezi 11 ya uongozi wake ameleta mabadiliko makubwa katika taasisi hiyo, hata hivyo hawakusita kumpongeza.
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Mifupa Dkt. Antony Assey kwa niaba ya wafanyakazi amemshukuru Prof. Makubi kwa uongozi wake mahiri na kufanikisha mageuzi makubwa ndani ya kipindi cha miezi 11.
Kwa upande mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi TUGHE tawi la MOI, Privatus Masula amempongeza Prof. Makubi kwa kuboresha maslahi ya watumishi na kuongeza ari ya uwajibikaji na kutoa huduma bora kwa wateja.
Prof. Makubi ametumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyakazi wa MOI kwa kuonesha ushirikiano na kufanikisha kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kwamba ni jukumu lao kuendeleza Ari hiyo.
“Binafsi naomba niwashukuru kwa kunipokea na kunikubali, Muendeleze mazuri hasahasa ubora wa huduma hilo ndiyo kipaumbele cha wizara na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan...ni jukumu lenu kuendeleza miradi tuliyoianzisha” amesema Prof. Makubi