Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Wenyeviti wa Bodi na kumpangia kituo cha kazi Balozi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-
(i) Jaji Latifa Alhinai Mansoor ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Mansoor alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi, Morogoro;
(ii) Jaji George Mcheche Masaju ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Masaju alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mshauri wa Rais, Sheria;
(iii) Jaji Dkt. Deo John Nangela ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Dkt. Nangela alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga;
(iv) Jaji Dkt. Ubena John Agatho ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Dkt. Agatho alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam;
Pia soma: Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais
(v) Balozi Dkt. Stephen John Simbachawene amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil. Balozi Dkt. Simbachawene anachukua nafasi ya Balozi Prof. Adelardus Kilangi ambaye amepangiwa majukumu mengine;
(vi) Bw. Uledi Abbas Mussa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kipindi cha pili; na
(vii) Prof. Zacharia Mabubu Mganilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE). Prof. Mganilwa anachukua nafasi ya Prof. Wineaster Anderson ambaye amemaliza muda wake.
Aidha, uapisho wa Majaji wa Mahakama ya Rufani walioteuliwa utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu