Wadau, dogo kaniuliza swali ambalo hata mimi limenigonga hivyo ningependa kupata ufafanuzi toka kwa wadau. Eti, pamoja na kwamba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ndie anateua majaji lakini hana uwezo wa kuwafukuza!!!!Sikutaka kumbishia dogo manake ningeweza kumbishia halafu akaniletea ushahidi mzee mzima nikaumbuka hasa ukizingatia ndo kwanza dogo mwenyewe ni Form III!!!! Je, jambo hili ni kweli au si kweli? Naomba ufafanuzi!!!
Technically Rais anaweza kumfukukuza Judge. Ila ni kazi NENE SANA kiasi kuwa inaonekana haiwezakani. Hii ni kutokana na kipengele cha "independence of Judiciary" ambapo moja ya mambo yanayotakiwa kwa independent judiciary ni uhakika wa tenure of office, na marupurupu kadhaa... Kwa ufupi, ile Rais amfukuze Judge, lazima tume iundwe ya majudge wasiopungua watatu kutoka nchi nyingine za Jumuiya ya Madola, wachunguze tuhuma za huyo Judge anayetakiwa kufukuzwa, wazihakikishe, halafu WAPENDEKEZE kuwa afukuzwe. Hapo ndipo Rais atashusha Rungu lake. Sasa ukiangalia mlolongo huo inaonekana Haiwezakani kumfukuza Judge. Judge ni mtu mkulu sana.
Nafahamu tu kuwa ni kweli lakini sina maelezo yenye references. Tusubiri wakuu watufafanulie.
Duh!!!! am 34 years with no law background!!! Is it too late for me kurudi class ili niwe judge some years future?! Manake ni bonge la flag mkuu !!