Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa viongozi kama ifuatavyo:
i) Amemteua Mhe. Jaji Winfrida Beatrice Korosso kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT). Mhe. Jaji Korosso ni Jaji wa Mahakama ya Rufani.
ii) Amemteua Bi. Bibiana Joseph Kileo kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Kabla ya uteuzi huu Bi. Kileo alikuwa Mkuu wa Mashtaka Mkoa (RPO), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Mwanza.
iii) Amemteua Bi. Alice Edward Mtulo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Bi. Mtulo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Kesi na Udhibiti Ubora, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
iv) Ametengua uteuzi wa Bi. Catherine Michael Mashalla, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manisapaa ya Sumbawanga.