Uteuzi unaotia shaka - Ukanda na Ukabila mtupu!

...ukiwa unafikiria kitu katika minajili ya ukabila jua wewe ndio mkabila namba moja!!!!
 

Nimependa ulivyoonyesha uzuri na manufaa ya diversity.Mchanganyiko mara zote huleta faida kubwa.Ndiyo maana nchi za wenzetu hutilia mkazo sana hili jambo.America wana mpaka Diversity Lottery ili kualika vipaji kutoka mataifa mengine kwa vile wanajua maana yake.Huku kwetu tutaishia kubaguana kwa misingi ya udini, ukabila, jinsia,nk na tutabaki mikia siku zote.
 

NImefurahishwa sana na namna ulivyoandika

Mwalimu alisema, "Hatumchagui mtu kwa kabila lake wala dini yake".
Mi nadhani uwezo wao umezingatiwa zaidi kuliko kitu kingine chochote.

Tume/Kamati zikiundwa kwa kubalance dini, makabila n.k bila kujali utaalam zaidi hatutafika. Tusubiri ili tuwapime kwa kazi yao.
 

Kampa shemeji yake? Hapa vilevile kuna tatizo.
 

WomenofSubstanc, August, et. al. tuko pamoja. Nilianzisha hii thread nikiwa na lengo la sisitiza diversity. Namfahamu vizuri Msolwa na nawafahamu vizuri wengi (90%) ya wajumbe wa kamati aliyounda. Ni rahisi sana kuona motives za uteuzi huu.

Ninachoona hapa ni nepotism ya hali ya juu. Naweza kusema kwa uhakika kwamba kama Msolwa angekuwa anatoka Kigoma au Musoma angeibuka na tume tofauti kabisa.

Hili tatizo aliloundia tume ni la kitaifa. Sasa sielewi ni kwa nini tume isiwe ya kitaifa! Naona umuhimu wa kuwepo kwa watu wanaofahamu hands on matatizo ya mtoto wa kike wa dini zingine (pamoja na kwamba mimi ni mkristo) ; sehemu mbalimbali za nchi, n.k.
 

Si kweli hata kidogo. Fanya research utakubaliana na mimi.
 

That was then! siku hizi si vigumu kuunda tume/kamati kwa kubalance dini, makabila n.k na ujali utaalam pia.
 
wewe kama wamekunyima uteuzi, usilete hasira zako hapa, usijemalizia hasira zako hapa ukatufanya sisi wanaJF tuungane na wewe kumbe wewe una vita nao. jamani, huyu jamaa hana point. hii kitu ingeondolewa kabisa. ulitaka wakuchague wewe na wamekutosa kwasababu hauna sifa hizo, sasa unalilia nini? hivi kuna udini unaweza kuongelewa hapa tz kweli? kama tukianza hivyo mbona mawaziri wengi tu wangebadilishwa kwasababu mkuu wa nchi kawapendelea sana watu wa dini fulani. lakini sisi tunaojiamini hilo halitutii shaka, kwasababu elimu tunayo na tutaishi kwa namna zozote zile. period.
 
"cynic" kwa level yako ya kufikiri na kutoa solution, hebu tupatie majina ya Tume yako ambayo ungeunda. Acha mawazo yaliopitwa na wakati.
 

Nilizungumzia diversity na siyo "kuondolewa udini tz"
 
"cynic" kwa level yako ya kufikiri na kutoa solution, hebu tupatie majina ya Tume yako ambayo ungeunda. Acha mawazo yaliopitwa na wakati.

I never questioned level ya kufikiri ya mtu yeyote. Nilikuwa nazungumzia diversity/utaifa. Kwa kifupi tume yangu ingekuwa na sura ya kitaifa, period!
 
Cynic yuko sahihi kuileta hii ishu. Mara ngapi sisi wamisheni tumeona udini katika teuzi mbali mbali? Kama vile tunavyotilia shaka pale ambapo muislamu anateua waislamu watupu basi nasi bila shaka ni lazima tutiliwe shaka tunapoteua wamisheni wenzetu peke yake! Hivi kweli kwenye tume yenye TOR zilizo general kama hii kweli tumekosa muislamu wakumweka humo? Nani katika tume atakaewakilisha constituency ya waislamu? Kama kweli tunataka kuwavuta wote basi ni lazima constituency (si za kisiasa bali za kijamii) ziwakilishwe. Kama vile tunavyotegemea wanawake watakua na uelewa zaidi wa kwa nini wengi wao hawamo katika fani hizi basi vile vile navyo naamini muislamu atakuwa na uelewa zaidi wa namna gani ya kuwavuta vijana wa kiislamu. Na wamisheni vile vile kwa wamisheni. Ni kwa kufanya hivi tu ndiyo tunaweza kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya jamii itaguswa. Bahati mbaya kwa jinsi ilivyo, sidhani kama pana nia dhabiti ya kupata mafanikio. Inawezekana nimekosea, lakini ndivyo ninavyoona.

Amandla.........
 
Hatuwezi kuupiga vita ukabila na udini kwa kukataa kuuzungumzia. Tutafanikiwa tu kwa kuuweka mezani na kuujadili kwa uwazi. Si Cynic mwenye matatizo bali ni nyinyi mnaokimbilia kumkebehi badala ya kuangalia hoja aliyoileta.

Amandla........
 
Kampa shemeji yake? Hapa vilevile kuna tatizo.

Ni kweli, huyu mama ni shemeji yake.

Binafsi sina tatizo kama mtu ana ujuzi unaotakiwa. Ndio maana huu mjadala ungeonekana una mwelekeo iwapo ungeangalia kama walioteuliwa wote wana sifa za kuwa kwenye kamati. Suala la udini na ukanda visingekuwa na maana sana kwa sababu hawatafuti technolojia ya kuendesha misikiti au makanisa wala mkoa. Tunapoteza sana muda wetu kujadili mambo ambayo hayana tija.
 

Unaweza kuwa na hoja ya msingi lakini hata hivyo umoonyesha shaka yako kwenye udini tu na ukaacha kujenga hoja kutokana na kichwa cha habari ulichotoa "Ukanda na Ukabila mtupu!".

Tunaomba pia uthibitishe kuhusu hoja nyingine ya Ukanda na ukabila hapo; naamini kabisa unayo hoja pamoja na wadau kukujia juu kuhusiana na suala la udini. Mdau mmoja ameshangaa kuwa amemteua na shemeji yake (Mke wa Dk Mshindo Msolla!), hata mimi nimeshangaa maana naamini unapokuwa kiongozi lazima uwe sensitive na baadhi ya vitu kama vile kuteua ndugu yake kwenye post za uongozi.
 

Kuna wale waliosema kuwa haki si kuwa itendeke tu bali ionekane inatendeka. Kwa kumpa shemeji yake nafasi hii kunamweka wazi kwa shutma za nepotism. Sidhani kuwa kuna utaalamu wowote alionao shemeji wake ambao unafanya kuwa ni lazima yeye aweko. Suala la dini na ukanda ni nafasi yake maana kinachotafutwa ni njia ya kuwavuta vijana kusomea fani hizi. Vijana hao wana dini, jinsia na kabila. Vyote hivi vinatutofautisha katika mtizamo wetu wa masuala ya kijamii. Sasa ukitaka kuwavuta ni lazima uwe makini na namna gani hizi imani identity zao zinavyoweza kutumika katika kufanikisha adhma yako. Kwa mfano, wote tunajua kuwa kuna maaneo ya nchi yetu yako nyuma kielimu kuliko kwengine. Basi itakuwa vizuri kama mmoja wa wajumbe atatoka katika moja ya sehemu hizo. Pale panapowezekana kupata uwakilishi, uwakilishi huo upatikane. Pale panapokuwa pagumu kupata uwakilishi kama vile makabila ( hatuwezi kuwa na mwakilishi kutoka kila kabila) basi njia mbadala itafutwe.

Sidhani kama tunapoteza muda kuvijadili maana tutajuaje havina tija kama hatuvijadili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…