Katika gazeti la Citizen la tarehe 16/3 kuna makala inayoelezea shuhuri za Ocean Road cancer Institute. Nilipata mshangao mkubwa sana pale niliposoma kuwa yule aliyekuwa msaidizi mkuu wa dr. Ngoma aliyestaafu ndio ameteuliwa kuchukua nafasi yake.!! Itakumbukwa kuwa viongozi wawili hawa yaani Dr Ngoma na Dr. Msemo ndio waliokumbwa na kashfa na malalmiko mengi toka kwa wadau enzi za uongozi wa Dr. Noma na huyo msaidizi wake Msemo; malalamiko ya wadau hasa yalitokana na conflict of interest waliyokuwa nayo wawili hawa kwa kumiliki hospitali zao binafsi zilizokuwa zinashuhurikia magonjwa ya saratani zikiwa Mwenge ya Dr. Ngoma na Dr. Msemo akiwa na hospitali yake kule Kigogo!! Madawa na vifaa muhimu vilikuwa havipatikani ORCI lakini wagonjwa walikuwa wanapata reference kwenda kwenye hospitali za hawa mabwana ambako madawa yalipatikana!! Kulikuwa pia na tuhuma za ubadhirifu wa fedha toka kwa wafadhili mbali mbali zilizowahusu wawili hawa!!!
Nilitegemea kuwa serikali ingelichukulia malalamiko haya ya wadau kwa uzito wake na kuteua daktari wa kuongoza hii taasisi ambae hana conflict of interest na ORCI kama aliyokuwa nayo Dr. msemo. Umuhimu wa kuwa na kiongozi muadilifu katika taasisi hii cannot be emphasized kwa vile siku hizi maradhi ya sararani yameongezeka sana katika jamii hivyo umuhimu wa kuwa na kiongozi wa ORCI amabaye atatumia muda wake mwingi pale hospitalini ni wa kupewa kupaumbele. Juu ya yote haya ili kupata kiongozi bora nafasi za namna hii ni vyema zingekuwa zinatangzwa na wananchi wapate nafasi ya kuomba na kushindanishwa na pale mshindi anapopatikana ni vizuri matokeo ya vetting processes yakaheshimiwa badala ya kutumia vigezo vya kujuana na kujipendekeza kuteua watu katika nafasi mbali mbali za serikali. Dr. Msemo hana sifa za kuongoza hii taasisi na haya ndio mapungufu ya uongozi wa serikali ya Kikwete [ kutokuheshimu maadili ya kazi].