Uteuzi wa Job Masima kuwa Balozi Israel ni ishara ya Rais Magufuli kuinoa na kuiimarisha TISS



Aisee safi sana kwahiyo mfumo wa kutuma na kupokea pesa kwa njia ya kieletroniki yaani TISS utaimarishwa safi sana hivi pesa ya Israel inaitwaje
 
Aisee safi sana kwahiyo mfumo wa kutuma na kupokea pesa kwa njia ya kieletroniki yaani TISS utaimarishwa safi sana hivi pesa ya Israel inaitwaje
Pesa zangu naweka chini ya godoro, kwa hiyo kutuma na kupokea so ajenda kwangu. Endeleeni
 
M16 not M15.
 
Awa tiss Ndo watoa kucha
Idara HII ni muhimu ila kwa nchi yetu imegeuka na kuwa idara ya WAHUNI, mbaya zaidi UHUNI wenyewe unaonekana kama vile unafurahiwa na WATAWALA..

Hadhi ya idara hii kwa nchi yetu imeshuka sana, na sidhani kama waliopo wana UWEZO wa kuihuisha.. Nafikiri wanachoweza kukifanya ni kuiboresha na kuwa ya KIHUNI ZAIDI..

Kwa sababu, wamedhihirisha kuwa ni WATAWALA wenye kupenda uhuni..
 

Mkuu, ni vitu gani unadhani vinaifanya idara hii ionekane imegeuka kuwa idara ya WAHUNI?

Funguka mkuu.
 
Mkuu, ni vitu gani unadhani vinaifanya idara hii ionekane imegeuka kuwa idara ya WAHUNI?

Funguka mkuu.
Brother Richard, I do believe, you have a very sound thinking capacity....

Sasa hivi ni KAWAIDA kabisa, kuwaona watumishi wa idara hiyo wakitumia nafasi zao kwa mambo ya kihuni mitaani..

Mfano mwepesi, siku chache zilizopita, tumewashuhudia pale protea hotel wakifanya uhuni dhidi ya Nape..... Wameonekana kwa huyo kwa sababu tu jamaa aliyefanyiwa ana title...

Matukio mangapi kwa mfano huo yanatokea mitaani kwa wananchi wasio na majina?????

Ile TISS ya akina Mzee Mzena imeondoka na wenyewe.

Sasa hivi bila hata soni, wanajinasibu kwa nafasi zao jambo ambalo lilikuwa haliwezekani kabisa kwa kipindi kile. Wengine hata wake zao walikuwa hawajui kama wanafanya kazi hiyo.

Kwa kweli ukizingatia nature ya kazi zao, na jinsi walivyo sasa, ni uhuni mtupu.

Na nionavyo, si rahisi kuirejesha ilipokuwa kutokana na watumishi wenyewe kutojitambua au tamaa na kujikurubisha sana kwa wanasiasa, kiasi cha kuwa watumwa wa wanasiasa, hivyo kulazimika kupokea na kutii maelekezo ya kipuuzi...

NAITAMANI TISS YETU ILIYOKUWA NA WELEDI, HADHI NA HESHIMA YA HALI YA JUU, SIO TZ TU, BALI DUNIANI KOTE........ NASIKITIKA SIIONI...
 

My friend Gryulka, ahsante kwa appreciation yako kutokana na michango yangu.

Ni kweli kabisa baada ya mzee Mzena kuondoka basi idara imeharibika kimaadili.

Maadili mahali popote ndiyo yanajenga taasisi imara.

Tatizo ni kule juu na mfumo mzima kwamba kuna mahali palikosewa baada ya Mwalimu.

Kurudisha maadili, nidhamu na kuondoa uhuni kazi kubwa inayoikabili tiss.

Kwa mfano mdogo tu ni tukio la Clouds na baada ya hapo kinachofuatia watu wanaodaiwa kufanya kazi tiss wanaanikwa picha zao mitandanoni.

Hii haiwezi kutokea katika tiss imara.

Naungana na wewe kabisa.
 
MUNGU IBARIKI TANZANIA..
 
Mkuu, ni vitu gani unadhani vinaifanya idara hii ionekane imegeuka kuwa idara ya WAHUNI?

Funguka mkuu.


Mkuu Richard nina mfano mwingine hai wa (someone I know) kuhusiana na suala la kukiuka maadili kulikopitiliza, kwa hii idara ya kipindi hiki.
Hii ilitokea chini ya tawala za nyuma kidogo, ambapo huyu mfanyakazi wao alikuwa akizidisha kilevi mara kwa mara na wakaogopa angeweza kutoa nyaraka nyeti za Serikali.
Ingawa alikuwa mmoja wa Vichwa muhimu sana ktk Idara, na pia mkuu wa kitengo alichokuwepo, wakubwa wa wakati ule hawakusita kumsimamisha kazi "kwa manufaa ya umma"
As opposed to now ambapo kuna kila aina ya drama, na watu bado wanajidai na kazi zao na kuendelea kutisha watu.
 


Mkuu Richards,
Hivyo vifungu viwili hapa vinahitaji uvipitie upya, binafsi naona kama vinajichanganya.
 

Mkuu Richards,
Hivyo vifungu viwili hapa vinahitaji uvipitie upya, binafsi naona kama vinajichanganya.


Ilikuwa ni tarehe 28 October 2015 Mkuu, raisi wa awamu ya nne Jakaya Kikwete alimkaribisha bwana Yahel Vilan.

Siku hiyo JK aliwapokea mabalozi wa kutoka nchi za Misri, Singapore, Israel na Ufilipino.

Kumbuka baada ya uchaguzi bado raisi wa awamu ya nne Kikwete alikuwa madarakani na raisi Magufuli likuwa akisubiri kuapishwa.

Baada ya raisi Magufuli kuapishwa balozi Vilan akaja tena tarehe 20 mwezi January 2016 kujitambulisha.

Soma link hii ya figganigga -https://www.jamiiforums.com/threads/rais-magufuli-akutana-na-balozi-wa-israel-nchini-ikulu-leo.1000540/page-6

Sasa nadhani utaelewa hapo.
 

Kwa kuwa DG mpya yupo, nadhani si sehemu ya wale ambao labda kwa namna moja au ingine wameingia humo kwa bahati mbaya.

Moja ya misingi muhimu kabisa ni kuhakikisha watu hawachukuliwi kwa bahati mbaya.

Sasa kwa miaka karibu 20 kuna watu wasostahili ambao waliingia humo na hawa ni wa kuwachuja huko tuendako.
 
Ilikuwa ni tarehe 28 October 2015 Mkuu, raisi wa awamu ya nne Jakaya Kikwete alimkaribisha bwana Yahel Vilan.

Siku hiyo JK aliwapokea mabalozi wa kutoka nchi za Misri, Singapore, Israel na Ufilipino.

Kwa hiyo mpaka hapo unataka kusema tayari kulikua na ubalozi wa Isirael!
Sawa.

Baada ya raisi John Magufuli kuingia madarakani mwezi January mwaka jana Balozi Vilan alimtembelea raisi Magufuli na kumhakikishia uhusiano huo kwamba upo na kusisitiza kwamba Israel itafungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania.

Na hapo alipokutana na Magufuli alisema Israel itafungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania, ina maana huyo balozi alikuwa anawakilisha nchi yake hapa Tanzania bila ofisi?

Rudia kuyasoma maelezo yako katika bandiko lako la kwanza.katika aya mbili zinazomtaja huyo balozi na Marais wetu Kikwete na Magufuli.
Hayo maelezo hayapo sawa, yaani hayajakamilika.

Hint: Huyo balozi alikuwa mwakilishi wa Israel nchini Tanzania au nchi jirani na Tanzania?

 
Hapo umeingiza ubashano wa kidini sasa. Ambao ktk namna ya kuelewa mambo utachemka. Kitu kikiwa halisi ni halisi tu, kama Israel wapo vizuri kwenye ulinzi wanakuwa hivyo tu haijalishi hutaki kukubaliana na hilo na kuthibitisha hilo US taifa ambalo linaongoza ktk masuala ya kujali ulinzi wa nchi wanawatumia hawa wa Israel kila siku. Vitu vingine ni dhahiri kabisa yani ni sawa mtu kwa sababu ni mweusi basi akatae kwamba wafanyabiashara wakubwa hapa nchini ni wahindi haitamsaidia kubadilosha uhalisia. Mambo mengine unakubaliana nayo tu then inachapa raba.
 
Sisi huwa tunaenda enda tu. Sijui ni kwa sababu ya kuwaacha watu wenye true passion na kazi fulani km jeshi na ku recruit watoto wa mjomba na shangazi?! Watu wanashindwa kufanya kazi zao wanabaki kusema tu usicheze na mimi unanijua?anatoa kitambulisho chake ate nae ni afisa wa TISS, kweli! Hilo neno INTELLIGENCE hapo linakuwa na maana gani sasa? Anyway tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa wenzetu km CIA coz mbali na kuangalia usalama wa nchi zao wameenda mbali zaidi kwa kuangalia na kucontrol masuala ya uchumi kwa interest za nchi yao
 
Hivi ukilaza mtaacha lini watanzania? Lumumba inaingiaje hapa? Huu ni mjadala wa kichama huu?

Acha wivu kijana
Ukombozi wa kwa kutoka kwa mkolono ulishafanyika mwaka 1961. Sasa sijui huu unaohusu akili ambao ni mkubwa kuliko ule wa kwanza utafanyika lini? Maana taifa linaangamia kwa kuwa na vijana wasiojelewa.
 
Mkuu huyu Jamaa kadanganya huwezi kwenda sehemu kwa kazi nyeti usipokewe na mwenyeji wako,
 
Mkuu huyu Jamaa kadanganya huwezi kwenda sehemu kwa kazi nyeti usipokewe na mwenyeji wako,

Ndiyo maana, nami nimejiuliza maswali mengi na kusikitika sana kuwa kama tumefikia hapo basi. Tunahitaji miujiza ya mbinguni ili tuponye Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…