Uteuzi wa ma DC na ma RC unazingatia sifa gani?

Uteuzi wa ma DC na ma RC unazingatia sifa gani?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Watu wote nchini wako wilayani na wanaishi wilayani. Wilaya ndio uti wa mgongo wa taifa na uti wa mgongo wa maisha yote ya watu. Ukikosea kwenye wilaya utakosea kwenye taifa pia. Hivyo kiongozi mkuu wa wilaya lazima awe mwenye elimu, ujuzi na uzoefu wa kuongoza watu badala ya kuchagua kwa kubalance mambo fulanifulani.

Je, ili kuwa DC ni vitu gani vinaangaliwa?
 
Siamini kabisa mtu ambae hajawahi kuwa hata class monitor darasani anaweza kuwa DC. Ndio maana wananchi wanawasubiri viongozi wakuu, Rais, Makamu au Waziri Mkuu kwenda kuwatatulia shida zao badala ya DC na RC wao. Mabango meeeengi wakati wa ziara za viongozi wakuu majimboni kwao. DC hawezi kutatua hata kero ndogo kabisa ya wananchi wake. DC anashindwa kuwashawishi watu wake wamfuate kwenye mipango yake badala yake analazimika kutumia mamlaka yake ya kikatiba kulazimisha watu wafanye anavyosema.

Kuna baadhi ya maDC ambao hata wakuu wa vyombo vya ulinzi wilayani wanajisikia kichefuchefu kuwapigia salute.
 
Kwanza ni lazima awe kificho, kipenyo au mbeya wa kitengo anayejulikana!
Kuwa kada ni ziada tu...
 
Uwezo wa kukata mauno mbele ya hadhara wakati wa mikutano ya kampeni ya ccm.
 
Kwanza ni lazima awe kificho, kipenyo au mbeya wa kitengo anayejulikana!
Kuwa kada ni ziada tu...
Uteuzi wa aina hiyo unazalisha mabango mengi sana kwenye ziara. Uteuzi wa hivyo unamlazimisha DC atumie vyombo vya dola kutiisha wananchi.
 
1. Uwe ni mwana CCM hasa hasa
2. Ukiwa TISS Agent ni an added advantage
3. Uwe na Sifa za Unafiki na Uwongo
4. Uwe Mshirikina wa kutoa Kafara
5. Ujue Kuiba Kura katika Chaguzi zetu
6. Uwe 'Snichi' wa Kuwachuuza Watu
7. Ujue Kuwakuwadia Viongozi Waandamizi kwa Wanaume na Kuhonga Kitufe Kitamu cha Baiolojia kwa Wanawake.
 
Nyota tu..na connection ndo Kila kitu mujini
DC kwa wenzetu ni mtu mwenye sifa na hadhi ya kuweza kuwa Rais. DC wetu hapa anaweza kutukana hadharani, anaweza kubambikia mtu kosa, anaweza kunyang'anya mke au mume wa mtu, anaweza kulewa chakali, anaweza kufanya uhalifu kama mtu mwingine tu.
 
Ndo ivo ndg yangu
DC kwa wenzetu ni mtu mwenye sifa na hadhi ya kuweza kuwa Rais. DC wetu hapa anaweza kutukana hadharani, anaweza kubambikia mtu kosa, anaweza kunyang'anya mke au mume wa mtu, anaweza kulewa chakali, anaweza kufanya uhalifu kama mtu mwingine tu.
 
Watu wote nchini wako wilayani na wanaishi wilayani. Wilaya ndio uti wa mgongo wa taifa na uti wa mgongo wa maisha yote ya watu. Ukikosea kwenye wilaya utakosea kwenye taifa pia. Hivyo kiongozi mkuu wa wilaya lazima awe mwenye elimu, ujuzi na uzoefu wa kuongoza watu badala ya kuchagua kwa kubalance mambo fulanifulani.

Je, ili kuwa DC ni vitu gani vinaangaliwa?
Ukada wa CCM na ujasiri wa kuwatukana Chadema
 
Back
Top Bottom