Uteuzi wa majaji - katiba inayopendekezwa

gwamaka aswile

Senior Member
Joined
Mar 26, 2015
Posts
186
Reaction score
106
Uteuzi wa Jaji wa Mahakama ya Juu
Uteuzi wa Jaji Mkuu
175.-(1) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka orodha ya majina ya watu watatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.
(2) Jaji Mkuu ndiye atakuwa Mkuu wa Mhimili wa Mahakama katika Jamhuri ya Muungano.
(3) Mtu ataweza kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu endapo atakuwa amefikisha umri wa miaka arobaini na tano au zaidi na mwenye sifa ya uadilifu na uaminifu katika utekelezaji wa majukumu yake na awe:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika Jamhuri ya Muungano; na
(i) amefanya kazi ya ujaji katika Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar; au
(ii) amefanya kazi ya utumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano au ana utaalamu akiwa na sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka ishirini.
Uteuzi wa Naibu Jaji Mkuu
176.-(1) Naibu Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka orodha ya majina ya watu watatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.
(2) Mtu atateuliwa kuwa Naibu Jaji Mkuu endapo atakuwa na sifa zilizoainishwa katika Ibara ya 175.
(3) Naibu Jaji Mkuu atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Jaji Mkuu katika utekelezaji wa majukumu yake.
Uteuzi wa Jaji wa Mahakama ya Juu
177.-(1) Jaji wa Mahakama ya Juu atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa majina yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.
(2) Mtu ataweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu endapo atakuwa amefikisha umri wa miaka arobaini na tano au zaidi na mwenye sifa ya uadilifu na uaminifu katika utekelezaji wa majukumu yake na awe:

(i) awe amefanya kazi ya ujaji katika Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu; au
(ii) awe wakili, mtumishi wa umma au mwana taaluma akiwa na sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano.
 
HOJA Ni Ipi Hapa.

ACHA BANGI ZA ASUBUHI
 
Good Katiba inayopendekezwa inaonyesha mfumo wa kuwapata watendaji wakuu wa Mahakama ya Tanzania, hiyo imekaa poa sana! I like it.
 
Back
Top Bottom