KWA HISTORIA TU.
sheria ya mapitio ya katiba, 2011 the Constitutional Review Act, 2011, (HAPO AWALI KABLA YA MABADILIKO )ilikuwa na vifungu vifuatavyo kuhusu uteuzi wa wajumbe wa kamati ya katiba:-
SEHEMU YA TATU
6.-(1) Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa
Zanzibar atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajul11bewa Tume.
(2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (3),
muundo wa Tume utazingatia msingi wa kuwepo kwa uwakiUshi ulio
sawa kwa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.
(3) Katika kufanya uteuzi wa wajumbe wa Tume, Rais
atazingatia masuala yafuatayo: (a) uzoefu katika kufanya mapitio ya katiba na sifa za
kitaaluma za wajumbe kwenye mambo ya katiba, sheria, utawala, uchumi, fedha na sayansi ya jamii;
(b) jiografia na mtawanyiko wa watu katika JamtlUri ya Muungano wa Tanzania;
(c) umri, jinsia na uwakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii; na
(4) Bila ya kuathiri ibara ndogo ya (3), mtu hatoweza kuteuliwa kama mjumbe wa Tume mpaka mtu huyo awe na uaminifu
wa hali ya juu ya tabia isiyo.tiliwa shaka na jamii.
(5) Bila ya kujali kifungu kidogo cha (3), mtu hatakuwa na
sifa za kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume endapo mtu huyo:-
(a) NI MBUNGE, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar, diwani au kiongozi wa chama cha katika ngazi .
zote; (b) ni mtumishi katika vyombo vya usalama; (c) ni mtu aliyewahi kuhukumiwa kwa kutenda kosa, au ni mtuhumiwa katika shauri lililopo mahakamani linalohusu
shitaka la kukosa uaminifu au maadili; au (d) si raia wa Tanzania. Wadau wakalalamika sana akiwemo na LISSU akapiga kelele sana sana, wakabadili hicho kifungu Bungeni Lissu akasema:- MUSWADA NA JEDWALI LA MAREKEBISHO LA SERIKALI Mheshimiwa Spika, Sasa naomba, kwa ruhusa yako, niwasilishe uchambuzi wa Muswada wenyewe pamoja na Jedwali la Marekebisho lililowasilishwa na Serikali, nikianzia na mapendekezo ya marekebisho ya vifungu mbali mbali vinavyohusiana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. TUME YA MABADILIKO YA KATIBA Mheshimiwa Spika, Ibara ya 2 ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho katika kifungu cha 6(5)(a) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kufuta maneno au kiongozi wa chama cha siasa wa ngazi yoyote. Jedwali la Marekebisho la Serikali lililowasilishwa sambamba na Muswada linapendekeza marekebisho sio tu ya ya kifungu cha 6(5)(a), bali pia kinapendekeza kuongezwa masharti ya ziada katika kifungu cha 6 cha Sheria. Kwanza, inapendekezwa kwamba maneno , diwani au kiongozi wa chama cha siasa katika ngazi zote yafutwe na badala yake yabaki maneno Mbunge na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Mheshimiwa Spika, Ili kuelewa maana ya marekebisho yanayopendekezwa, ni muhimu kurejea katika kifungu cha 6(5) kinachopendekezwa kurekebishwa na Muswada huu. Kifungu hiki kinaweka masharti ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuwaondolea sifa za kuteuliwa Wabunge, Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, madiwani na viongozi wa vyama vya siasa wa ngazi zote. Kwa mapendekezo ya Muswada huu na Jedwali la Marekebisho la Serikali, watu pekee ambao sasa hawatakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ni Wabunge na Wawakilishi wa Zanzibar. Kwa maneno mengine, madiwani na viongozi wa vyama vya siasa wa ngazi zote watakuwa na sifa za kuteuliwa ili mradi tu wanazo sifa za kitaaluma na nyinginezo zilizotajwa katika kifungu cha 6(3) cha Sheria.
Mheshimiwa Spika, Katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakati wa mjadala wa kupitishwa kwa Sheria hii tarehe 15 Novemba mwaka jana, tuliliambia Bunge lako tukufu kwamba, kwa kukataza viongozi wa vyama vya siasa kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume, kifungu cha 6(5)(a) k(i)naondoa kwenye mchakato wa Katiba Mpya kundi kubwa la watu wenye utaalamu na uzoefu katika masuala mbali mbali ya kisiasa, kikatiba, kisheria, kiuchumi, kiutawala, kifedha na kisayansi jamii. Vile vile, viongozi wa vyama vya siasa wanawakilisha makundi makubwa ya kijamii yenye mtawanyiko wa watu na wa kijiografia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wanawakilisha watu wa umri na jinsia zote kama inavyopendekezwa katika Muswada Mpya.
Pendekezo letu kwamba Wabunge na Wawakilishi wa Zanzibar nao wawe na sifa za kuteuliwa wajumbe wa Tume halipo katika mapendekezo ya Muswada huu na Jedwali la Marekebisho la Serikali. Hata hivyo katika kuendeleza moyo wa maridhiano na give and take Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaridhika na kuunga mkono mapendekezo ya marekebisho ya kifungu cha 6(5)(a) ili kuwapa madiwani na viongozi wa vyama vya siasa sifa za kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume.
(Wabunge wa CCM wakapiga makofi na kushangilia sana)
MABADILIKO HAYO YAKAPITISHWA YOTE.
Leo hii:-
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
(Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83, Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7) ______________________________
13. Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 100"]
[TR]
[TD="colspan: 3"] GENERAL
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Salutation
[/TD]
[TD] Honourable
[/TD]
[TD="width: 42%"]
Member picture
[/TR]
[TR]
[TD] First Name:
[/TD]
[TD] Al-Shaymaa
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Middle Name:
[/TD]
[TD] John
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Last Name:
[/TD]
[TD] Kwegyir
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 20%"] Member Type:
[/TD]
[TD="width: 38%"] Special Seat
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Constituent:
[/TD]
[TD] No Constituency
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Political Party:
[/TD]
[TD] CCM
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Office Location:
[/TD]
[TD] Box 61530, Dar Es Salaam
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Office Phone:
[/TD]
[TD] +255 773 238804/+255 713 238804
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Ext.:
[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Office Fax:
[/TD]
[TD] -
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Office E-mail:
[/TD]
[TD] akwegyir@parliament.go.tz
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Member Status:
[/TD]
[TD] Current Member
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Start date:
[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] End date:
[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Date of Birth
[/TD]
[TD] 8 April 1960
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 100"]
[TR]
[TD="colspan: 5"] EDUCATIONS
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 35%"] School Name/Location
[/TD]
[TD="width: 27%"] Course/Degree/Award
[/TD]
[TD="width: 15%"]
Start Date
[TD="width: 13%"]
End Date
[TD="width: 10%"]
Level
[/TR]
[TR]
[TD] Agha Khan Primary School
[/TD]
[TD]
Primary Education
[TD]
1968
[TD]
1971
[TD]
PRIMARY
[/TR]
[TR]
[TD] Forodhani Primary School
[/TD]
[TD]
Primary Education
[TD]
1972
[TD]
1974
[TD]
PRIMARY
[/TR]
[TR]
[TD] Forest Hill Secondary School
[/TD]
[TD]
O-Level Education
[TD]
1975
[TD]
1975
[TD]
SECONDARY
[/TR]
[TR]
[TD] Forodhani Secondary School
[/TD]
[TD]
O-Level Education
[TD]
1976
[TD]
1978
[TD]
SECONDARY
[/TR]
[TR]
[TD] College of Diplomacy
[/TD]
[TD]
Diploma (Law)
[TD]
2006
[TD]
-
[TD]
DIPLOMA
[/TR]
[TR]
[TD] University of Dar es Salaam
[/TD]
[TD]
LLB
[TD]
2008
[TD][/TD]
[TD]
GRADUATE
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 100"]
[TR]
[TD] CERTIFICATIONS
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Je hii ni sawa kweli?, hasa ukizingatia RAISI katika kiapo chake cha uraisi anasema:- . ataitunza na kuilinda katiba ya nchi. Na Katiba inaelekeza kuwa nchi ya Tanzania itaendeshwa kwa kuzingatia matakwa ya katiba, sheria na taratibu zilizopo.
Sina ubaya wala kinyongo na Mh. Aliteuliwa namweshimu sana kama mtu makini na hodari kwa kupigania haki na maslhai ya watu wanyonje kwenye jamii lakini kuwepo kwake hapa kwa mtazamo wangu ni kinyume na sheria ambayo serikali iliilazimisha iwe hivyo kwa nguvu sana licha ya kupingwa na wadau mbalimbali.
IKIWA hili limefanyika kinyume cha sheria, je wasaidizi wa raisi katika masuala ya sheria wanafanya nini? Au aliwakaidi? Je kwa kutokuzingatia matakwa ya sheria ya mabadiliko ya katiba kama ilivyobadilishwa,2012 KATIBA iliyopo imelindwa na kutetewa, na pia ujumbe gani unapelekwa kwa wananchi wa kawaida kuhusu utawala wa sheria?. Na nini kifanyike sasa kama kunatatizo? Tulitazame na kuliangalia hili kwa upana ili tudumishe demokrasia na utii wa sheria katika nchi hii.