JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kifungu cha 70(1) cha Taratibu za Uchaguzi 2020 kinaeleza kuwa:- Kila Chama cha Siasa ambacho kinashiriki Uchaguzi wa Wabunge ambao utafanyika baada ya kuvunjwa kwa Bunge kitapendekeza na kupeleka kwenye Tume Majina ya wagombea stahiki Wanawake kwa ajili ya Uteuzi kama Wabunge Wanawake wa Viti Maalum
Aidha kifungu kidogo cha 2 kinasema kwamba:- Vigezo kwa ajili ya kukusanya majina yaliyopendekezwa kwa ajili ya viti maalum kama ilivyoelezwa katika Sheria hii vinatakiwa viwekwe kupitia Tume au msimamizi mkuu kwa Fomu ya Uteuzi kwa ajili ya kugombea Ubunge viti maalum (Fomu No. 8D) iliyokamilika kama ilivyoelekezwa katika taratibu hizi, na fomu itapatikana kutoka Tume au msimamizi mkuu
Na kifungu kidogo cha 3 kinaeleza kuwa :- Majina ya wagombea yaliyopendekezwa na kukusanywa kwa Tume yanatakiwa kuzingatia Sheria ya Gharama za Uchaguzi
Upvote
0