Uteuzi wa wajumbe tume ya mabadiliko ya katiba ngazi ya kata

Uteuzi wa wajumbe tume ya mabadiliko ya katiba ngazi ya kata

Daniel Muhina

Member
Joined
Jun 16, 2012
Posts
38
Reaction score
12
Ndg wana JF, kumekuwa na mkanganyiko mkubwa juu ya uteuzi wa wajumbe wa tume ya mabadiliko ngazi ya kata kuwa wajumbe wanaostahili kupiga kura ni kina nani? Wataalamu hawaruhusiwi kupiga kura, je kama mkiti amegombea na ameshinda/ameshindwa haruhusiwi kupiga kura,wagombea hawaruhusiwi kuwepo eneo la uteuzi?

Binafsi nimefatilia hata kwenye Mwongozo uliotolewa na tume hautamki mambo hayo kibaya zaidi hata baadhi ya wadau ngazi ya wilaya walioteuliwa kuratibu shughuli hizi hawana uelewa wa kutosha.

Naomba yeyote mwenye taarifa sahihi juu ya nilichokiuliza hapo juu anijuze kwa chanzo sahihi za taarifa zake NB Tovuti yao haijitoshelezi kupata majibu kwa muda muafaka
 
Kwenye ngazi ya kata ndo kuna chujio la CCM hapo, hapo ni chama shika hatamu! labda maeneo ambayo kuna madiwani wa Upinzani ndo kutakuwa na tofauti!
 
Back
Top Bottom