Achraf Hakimi
JF-Expert Member
- Mar 3, 2010
- 943
- 1,944
Kumekuwepo taarifa nyingi katika siku za hivi karibuni kuhusu wanafunzi kufukuzwa na wengine kukataliwa kujiunga darasa la kwanza au kufanya mitihani kwa kushindwa kulipa michango.
Mfano hai ni ule ulioripotiwa kutokea Shinyanga mwezi uliopita, ambako katika hali isiyokuwa ya kawaida robo tatu ya wanafunzi katika Shule ya Sekondari Uhuru iliyoko Manispaa ya Shinyanga, inadaiwa kuwa walizuiwa kufanya mitihani ya muhula wa pili, kwa madai ya wazazi wao kushindwa kulipia michango ikiwamo ya mlinzi.
Pia awali huko Nachingwea kulikuwa na malamiko ya baadhi ya wazazi na walezi wa watoto waliokuwa wanasoma katika baadhi ya shule za msingi wilayani humo, kufukuzwa kwa kutolipa michango mbalimbali shuleni.
Baadhi ya watoto hao walitimuliwa shuleni kwa kutowasilisha michango ikiwamo ya bidhaa kama vile mahindi na fedha taslimu, licha ya wazazi wa baadhi ya wanafunzi kuomba kulipa kwa awamu kutokana na hali ngumu ya kiuchumi iliyokuwa ikiwakabili.
Licha ya Serikali kutamka kuwa elimu ya msingi ni bure pia imesema kutakuwa na mchango wa Sh 20,000 kwa elimu ya sekondari. Lakini pia imeruhusu kamati na bodi za shule kutoza michango, nadhani kwa kuwa fedha za ruzuku na maendeleo zinazotolewa na Serikali kuziendesha shule hizo hazitoshi au hazifiki kabisa shuleni.
Hali hii imezifanya shule kubuni mbinu mbalimbali za kujiendesha. Hii imetoa mwanya kwa kamati na bodi za shule kujipangia michango zitakavyo. Kukithiri kwa wingi na ukubwa wa michango inayodaiwa na shule, umekuwa ni mzigo mkubwa kwa wazazi na sasa imekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya elimu.
Baadhi ya michango inayotakiwa kulipwa kabla mwanafunzi hajaingia shuleni, ni pamoja na fedha kwa ajili ya vitambulisho, tahadhari, madawati, sare za shule, mlinzi wa shule, nembo ya shule, kurudufu mitihani, kutembelea sehemu za utalii na mingine mingi. Ni kweli kuwa michango hii ni midogo lakini ukiijumlisha ni zaidi ya Sh 100,000. Kwa mwananchi wa kawaida aliye katika lindi la umaskini, michango hii ni mzigo mzito sana kwake.
Ni wazi kuwa hili la kuongezeka kwa michango linazidi kukwaza hatua za kuwapatia elimu watoto kutoka jamii hizi, jambo ambalo litazidi kukwaza maendeleo ya nchi yetu kwani ujinga na maendeleo abadani havitangamani.
Ripoti ya Uwezo kuhusu kusoma na kuandika kwa wananchi wenye umri kuanzia miaka 15 miongoni mwa nchi za Kiafrika iliyotolewa hivi karibuni, inaonyesha kuwa hali siyo nzuri kwa upande wa Tanzania.
Katika nchi 50 zilizoorodheshwa, Tanzania inashika nafasi ya 19 ikiwa na asilimia 69.4 tu ya wananchi wanaojua kusoma na kuandika.
Ingawa kujua kusoma na kuandika siyo kipimo kamili kuhusu hali ya elimu katika nchi, umuhimu wa elimu katika nchi yoyote uko wazi. Kiwango cha chini cha kujua kusoma na kuandika na elimu kwa jumla, inaweza kuzorotesha maendeleo ya kiuchumi ya nchi katika dunia ya sasa inayobadilika kupitia teknolojia.
Siyo vibaya wananchi kuchangia maendeleo ya shule, lakini Serikali inapaswa kutoa mwongozo kuhusu michango ipi ichangwe na kwa kiwango gani. Hii itaondoa mkanganyiko wa kila shule kujipangia yenyewe aina na viwango vya kuwatoza wazazi kama ilivyo sasa.
SOURCE: mwananchi.co.tz