kALEnga kidamali
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 542
- 735
Ukiachana na ile michezo ya ku bet kwa wahindi na kampuni nyingine kwa njia za mitandao ambayo kwa sasa jamii kubwa ni kama imeelewa na kuondoa ile hali ya kuwa na matumaini makubwa ya kushinda na hivyo kucheza kwa kiasi na tahadhari kubwa na hii imekuja baada ya wengi kupigwa pesa bila kupata kile walichokuwa wakikitarajia kwa muda mrefu.
Sasa baada ya jamii yetu kuizoea na kuelevuka juu ya hizo kamari za wahindi na makampuni mengine(sport betting) kumezuka aina nyingine ya kamari zinazotangazwa kwa nguvu kubwa na redio zetu hapa nchini yaani unakuta kila baada ya dakika mbili au tatu mtangazaji wa redio ni lazima ahamasishe watu wacheze kamari kwa kutoa matumaini ya kushinda mamilion ya pesa hayo matangazo ni kwenye vipindi vyote masaa 24 yaani hadi imekuwa kero.
Athari kubwa ya hizi kamari za maredioni ni kutuletea kizazi ambacho kitakuwa hakiwazi kujishughulisha (uvivu) kwenye kazi nyingine za uzalishaji za kujipatia kipato halali zaidi ya kuwaza kushinda kamari ambayo kiuhalisia ni vigumu kushinda kwa kila mtu. Hapa pia kuna hatari ya kuongeza tabia za ukibaka,utapeli na ukabaji kwa wale watakaokuwa wametumia akiba kucheza kamari na hawajapata kitu ikiwa mahitaji mengine yanawasubiri.
Yawezekana sheria zetu zinaruhusu hayo yote lakini kwanini wasiangalie namna ya kudhibiti huu utitiri wa hizi kamari maredion kwa Sasa ambazo zinashawishi watu kwa nguvu wacheze kwa matumaini hewa? Wapo watu ambao pesa zao hazikai kwenye mitandao ya simu wao kila uchwao ni kutuma mikeka ya bukubuku ili wajishindie mamilion.
Ushauri wangu Kama ni sheria zinaruhusu haya Basi zirekebishwe ili kuwe na muda maalumu kuanzia saa tano usiku ndipo hayo matangazo yawepo na washindi watangazwe huko isiwe muda wote ni matangazo ya kamari tu kana kwamba hii ni nchi ya wacheza kamari.