Utitiri wa One za point 7: Je, wa zamani tulikuwa vilaza au elimu imekuwa rahisi?

Utitiri wa One za point 7: Je, wa zamani tulikuwa vilaza au elimu imekuwa rahisi?

Satoshi Nakamoto

Senior Member
Joined
May 28, 2017
Posts
110
Reaction score
464
Mtakua mmeshuhudia kwamba kuna shule karibia asilimia 90 wamepata 1.7, means karibia darasa zima kila mtoto ana A masomo yote.

Nimejiuliza maswali kadhaa nimekosa majibu:

1. Je, zamani tulikua vilaza? Kiasi kwamba nchi nzima div. 1 point 7 unakuta hazifiki hata 20, na utazikuta chache Ilboru, Mzumbe na Kibaha.

2. Au mitihani ya zamani na ya sasa hivi imekua tofauti kiasi kwamba watoto this time wanatusua sana?

3. Au mitoto ya siku hizi mingi ni mi jiniaz?

4. Au janja janja imekua nyingi especially kwenye shule za private kiasi cha watoto wengi kupata A karibia masomo yote?

Screenshot_20220115-211730.png
 
Jibu unalo

 
elimu ya kukariri vitini na kupata As, Bongo bado sana

hao vipanga wakimaliza 'chuo' wanaishia kua TAs, ni ujinga ujinga tuu ndiyo umetawala,
 
Elimu elisha shuka walivo anza kubebana kiudini, watu 100 hawawezi kua na maximum point niujinga na aibu
 
5. Au mitihani ya siku hizi imekuwa rojo rojooooo sanaaa

6. Ama watunzi wa mitihani nao wamekuwa wakirudia sana maswali hawana mbinu mpya za kumfikirisha studentiii

Anyway kila kitu na zama zake
 
Kinachoniuma watoto hawafundishwi skills bali kukalili watu wenye skills wanaoleta changes ni average perfomers. Tuache mambo ya kukallii kids should learn more in practical. more of being creative and critical thinking

Sisi tulikuwa tunafeli lakini the way we think and we do things was different, tulijua kulima, tumefundishwa biashara na pia tulikua tunajua what was going on in the world

Todays kids wanapata one anaenda chuo anagraduate na hajui chochote zaidi ya iphone 11 shit
 
Zamani A ilianzia 81, hivi sasa A inaanzia 75

Wapo wengi zamani walipata hizo 75 -80 wakapewa grade B. Maanake kwa sasa wenye 75-kuendelea ni grade A, happ lazima kuwe na utitiri wa hizo one za 7.

Zamani ukiwa na F ya hesabu, unapigwa penalt unaangukia div three!
 
technolojia imekuwa sana kusoma kwa kuona videos inakaa sana kichwani kuliko kukalili kwenye vitabu tu.
 
Kwani zikiwa nyingi zinakupunguzia nini? Mbona zaidi ya nusu ya Watoto wamepata div.4 .Lipi ni tatizo Kati ya 4 au 1?
 
nikikumbuka mwaka wetu watu walivyofeli mapaka matokeo kurudiwa,alafu nikiskia matokea haya nasema daaah
 
Kusoma kutumia internet imekua rahisi Sana Mfano twishen dot kom, sehem tofauti nyingine , ni muda tu na jitihada za walezi
 
Swali kama hilo hupaswi kuuliza, Kwani wakati wenu mlihitimu wangapi? Kwani hujui watanzania wameongezeka kwa kuzaliana? Tulipata uhuru tupo milion 9 na sasa tupo zaidi ya million 60,
 
Back
Top Bottom