Utitiri wa vitambulisho Tanzania

Utitiri wa vitambulisho Tanzania

Rumanyika Donatus

New Member
Joined
Aug 3, 2021
Posts
4
Reaction score
2
Kwanza napenda kuipongeza Wizara ya Tamisemi kwa kuja na mfumo mpya wa kadi za kieletroniki katika vituo vya mabasi ya mwendo kasi.

Sambamba na pongezi hizi bado kuna changamoto ambazo ni mzigo kwa raia.

1. Ili upate kadi hiyo utalazima kuwa na aidha kadi ya mpiga kura, pasi ya kusafiria, leseni ya udereva kitambulisho cha Taifa nk.

2. Kuna haja ya kuwa na mzigo wa vitambulisho vyote ili wananchi wapate kadi hiyo?

3. Je, Wizara imewafikiriaje wale ambao wapo chini ya umri wa miaka 18 ili waweze kutumia usafiri huo?

4. Je, Wizara haioni kwamba inawahitaji wananchi wawe na mzigo mkubwa wa kubeba kadi.

Nilimaanisha mtu ana kadi ya mpiga kura, kadi ya kuingia kwenye gari za mwendo kasi, kadi za benki, kitambulisho cha NIDA, pasi ya kusafiria, kadi ya bima, kadi za vyama kadhalika.

Soma Pia: Matumizi ya vitambulisho vingi, kwanini kisitumike kitambulisho cha NIDA pekee?

Napendekeza kwamba kungekuwepo na uwezekano wa kuwepo kwa kadi moja ambayo imebeba majukumu yote ili kupunguza mzigo kwa raia.

Tuna watehama magwiji na nguli katika nchi wa kuratibu haya mambo.

Nasema haya kwani NIDA ndiyo imebeba taarifa zote za raia na nafikiria ndiyo inaweza kubeba taarifa zote ikiwemo na kadi ya kuingia kwenye mabasi ya mwendo kasi.

La sivyo raia tutakuwa na ulazima wa kutembea na mabegi kwa ajili kubeba vitambulisho.
 
Back
Top Bottom